Previous Chapter -- Next Chapter
10.1. Hisia danganyifu za usalama
Waislamu kwa ujumla wanaamini Qur’an kuwa kitabu pekee kitakatifu kilichotunzwa, hata kama imani ya namna hii haina thibati yoyote ya Kihistoria. Kama matokeo ya imani ya namna hii, Waislamu kwa ujumla wao hawataki wala kujisikia kusoma vitabu vya imani nyingine. Hata Muislamu msomi kupindukia hawezi kusoma Biblia kwa sababu wanaamini kwamba imechafuliwa (hivyo ni kusema Maandishi yake yamebadilishwa) au imetanguliwa (ndio kusema nafasi yake imechukuliwa ufunuo wa Mungu wa baadaye kama mbadala). Kwao, Muhammad ndiye nabii wa mwisho, vitabu vya dini zote kabla ya Uislamu haviwezi kuaminika. Hata pale Muislamu anaposoma Uislamu kwa undani na kukuta mambo ya kupingana kwa kugongana na yasiyofuata mpangilio, ni bora kwao kuwa wakana Mungu kuliko kuiamini Biblia. Walishaaminishwa kwamba Uislamu ndio dini pekee na ya kweli, wanapogundua kwamba si ya kweli hawatatafuta nyingine kama Uislamu walioamini kwamba ndio dini iliyotunza usahihi zadi na ndio ya kweli inageuka ya uongo, basi hakuna kingine chochote kile kinachoweza kuaminika tena.