Grace and Truth

This website is under construction !

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 071 (Did Mohammed memorise the Qur’an at the point of revelation?)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
13.1. Imani juu ya kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili

13.1.1. Je Muhammad alikariri Qur’an wakati wa kufunuliwa?


Kulingana na vyanzo vya Kiislamu vyenyewe, Muhammad hakuwa na kumbu kumbu kamili kama Waislamu wanavyodai. Alisema:

“Mimi ni mwanadamu kama nyie, Nasahau kama nyie.Kama nikisahau, mnikumbushe.” (Sahih Bukhari)

Kwa kweli, Muhammad wakati mwingine alisahau Qur’an mpaka mtu mwingine alipomkumbusha:

“Imepokelewa na Aisha : Mtume wa Allah alimsikia mtu akisoma Qur’an usiku, na akasema, “ Allah ajaalie rehema juu yake, maana amenikumbusha aya fulani na fulani na sura fulani, ambayo nilisababishiwa kusahau” (Sahih Bukhari)

Muhammad pia alisema Qur’an inasahaulika

“Kwa namna alivyo duni yule asemaye nimesahau aya fulani na fulani.’Badala yake aseme nimesababishiwa kusahau. Jaribu kukumbuka Qur’an, maana ina mtego wa kuponyoka kutoka kwenye mioyo ya watu kuliko ngamia kwenye kamba” (Sahih Muslim)

Hivyo dhana ya Muhammad kuwa na kumbukumbu kamili haiungwi mkono na vyanzo vya Kiislamu hata kama ni maarufu kiasi gani miongoni mwa Waislamu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:09 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)