Grace and Truth

This website is under construction !

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 026 (PILLAR 6: Jihad (holy struggle))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA NNE: NGUZO ZA UISLAMU

4.6. NGUZO 6: Jihad (vita takatifu)


Wakati baadhi ya wanazuoni hawachukulii Jihad kuwa miongoni mwa nguzo za Uislamu, wengine wao wanaichukulia kama nguzo ya tano ya Uislamu badala ya Hija, huku wengi wao huichukulia kama nguzo ya ziada ya sita. Kwa siku hizi imepewa uzito na wasiokuwa Waislamu kwa sababu ya vuguvugu za Kivita zinazohusishwa na Uislamu. Pia ni mada inayojadiliwa zaidi na wanazuoni wa Kiislamu, pia mojawapo ya mada ambayo tunapata shida sana kuelezwa Jihad ni kitu gani na kitu gani sio jihad. Watetezi wa Kiislamu wanajaribu kuifafanua, ya kwamba kwamba neno “Jihadi” inamaanisha “Kujitahidi” na sio vita takatifu kama inavyotafsiriwa mara kwa mara, wakisistiza kwamba kujitahidi huko sio lazima kutumia nguvu. Hii kwa uhalisia wa neno ni kweli; Jihad inaweza kumaanisha “mapambano ya kiroho ya ndani ya mtu au kujitahidi. Hata hivyo, Kwa mjibu wa vyanzo vya Kiislamu, mara zote na kwa sana imetafsiriwa kwamba ni kujitahidi kwa njia za vita ili kusimika Uislamu kuwa dini rasmi ya nchi na sheria za Kiislamu kuwa sheria za nchi.

Kujua umuhimu wa Jihad katika Uislamu, turejee HADITH na Qur’an. Muhammad anafafanua umuhimu wa Jihad kwa kusema:

“Mjue kwamba pepo iko chini ya vivuli vya mapanga (Kupigania njia ya Allah)”. (Hadith ya Bukhari, 2818)

Mahali pengine katika Hadith, Muhammad anafafanua kwamba Jihad ndio sababu ya yeye kutumwa kwake:

“Nimeamurishwa kupigana na watu hadi washuhudie kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na kuniamini mimi na nilichokileta. Na wakifanya hivyo, damu zao na mali zao vitalindwa dhidi yangu, isipokuwa kwa sababu zingine za haki, na hesabu yao itakuwa kwa Allah” (Imepokelewa na Muslim na Bukhari).

Wanazuoni wa Kiislamu wanaona kwamba lengo kuu la Jihadi ni kuwafanya watu kumuabudu Allah and kumfuata Muhammad. Qur’an pia inasisitiza lengo hilo hilo:

“Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu”. (Qur’an 2:193)

Mahala pengine amenukuliwa akiweka wazi kuwa Jihad inahusihana na utumiaji wa vurugu:

“Ninaapa kwake yeye ambaye anayo nafsi yangu mikononi mwake, nilitumwa kwenu bila chochote isipokuwa kuchinja” (Sahih Ibn Haban),

na

“Nilitumwa kwa upanga kuitangulia siku ya hukumu na riziki yangu ipo katika kivuli cha mkuki wangu na unyonge na kushindwa viko kwao wasionitii mimi.” (Musnad Ahmad)

Muhammad aliunda Jihad kama lengo la kudumu na kuwaonya Waislamu wasije kuiacha, kwa kusema:

“Ukiingia katika shughuli ya Inah, shika mkia wa ng’ombe, mkiridhika na kilimo, kisha mkaacha kupigana Jihad (Kupigana katika njia ya Allah), Allah atafanya fedheha iwe juu yenu, na hataiondoa mpaka mrudie katika asili ya dini (ya Kiislamu).” (Sunan Abi Dawud)

Inah ni jina linalotolewa kwenye biashara yenye riba. Kimsingi alichokuwa anasema Muhammad ni kwamba riziki ya mtu haitokani na kazi za asili kama kilimo lakini kutoka kwenye Jihad, ambayo haitakoma mpaka dunia nzime iwe ya Kiislamu.

Kwa hiyo tumeona anachosema Muhammad juu ya Jihad, kama ilivyoandikwa kwenye Hadith. Je Qur’an inasema nini juu ya Jihad? Katika Qur’an, kupigana kumekuja hatua kwa hatua. Kwanza kwa ajili kujilinda, kisha kuwashambulia wengine. Tunaona hili katika nadharia ya maendeleo ya Jihad katika aya zifuatazo:

“Piganeni katika njia ya Allah na wale wanaopigana nanyi, Wala msianze uadui, maana Allah hawapendi waanzao uadui” (Qur’an 2:190)
“Wauweni popote mwakutapo, muwatoe popopte walipokutoeni, kwani fitina ni mbaya zaidi ya kuuwa” (Qur’an 2:191)
“Piganeni nao mpaka isiwepo fitna (Kutoakuamini na ushirikina, i.e. kuabudu wengine kinyume na Allah) na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Allah. Lakini wakiacha, basi hakika Allah anayaona wanayoyatenda.” (Qur’an 8:39)
“Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachosha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho kheri kwenu. Na huenda mnapenda kitu nacho ni shari kwenu, na Allah anajua na ninyi hamjui.” (Qur’an 2:216)
“Basi na wapigane katika njia ya Allah wale ambao wanauza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anayepigana katika njia ya Allah, kisha akauliwa au akashinda, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.” (Qur’an 4:74)
“Basi wakamateni na wauweni popote mnapowapata. Wala msifanye rafiki katika wao wala msaidizi.” (Qur’an 4:89)
“Allah amewatukuza kwa cheo wale wanaopigana kwa mali zao na nafsi zao kuliko wale wanaokaa tu nyumbani.” (Qur’an 4:95)
“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari kwa ajili ya vita,ili kuwatisha maadui wa Allah na maadui zenu, na wengine ambao hamuwajui,lakini Allah anawajua. Mkitoa chochote katika njia ya Allah, mtarudishiwa na wala nyinyi hamtadhulumiwa.” (Qur’an 8:60)
“Ewe nabii! Wahimize waumini waende vitani. Wakiwapo kati yenu ishirini wanaosubiri watawashinda mia mbili, wakiwako kati yenu mia, watawashinda elfu moja katika waliokufuru: Kwa sababu wao ni watu wasio fahamu.” (Qur’an 8:65)
“Piganeni nao. Allah atwaadhibu kwa mikono yenu, na atawafunika kwa aibu, na atakunusuruni muwashinde, avipoze vifua vya waumini.” (Qur’an 9:14)
“Piganeni na wasio muamini Allah wala siku ya mwisho, wala hawaharamishi alivoviharamisha Allah na Mtume wake, wala hawashiki Dini ya haki, miongoni mwa watu wa kitabu, mpaka watoe kodi ya Jizyah kwa khiari yao, hali wametii.” (Qur’an 9:29)
“Sema: hivyo mnatutazamia litupate lolote isipokuwa moja katika mema mawili (Kufa kishahidi au ushindi)? Na sisi tunakutazamieni Allah akufikishieni adhabu itokayo kwake, au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi.” (Qur’an 9:52)
“Basi ikiisha miezi mitukufu, basi wawuweni washirikina popote mwakutapo na washikeni,na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia (ya vita); lakini wakitubu, wakashika sala,na wakatoa zaka, basi waachilieni. Hakika Allah ni mwenye kusamehe na mwenye kurehemu.” (Qur’an 9:5)

Hivyo tunaweza kuona kwamba vyote Qur’an na Hadith vinawaagia Waislamu kupigana ili kuanzisha ufalme wa Allah duniani kwa namna yoyote ile inayowezekana. Waislamu wanaona suala hili kama mchezo wa duara ambayo lazima washinde na wasiokuwa Waislamu lazima washindwe. Baadhi ya wanazuoni wa Ki- Suni wanasema Jihad ni takwa la lazima kwa kila Muislamu mpaka Uislamu ukubalike kama sheria rasmi ya nchi kwa kila taifa duniani. Hii haimaanishi kwamba kila mtu lazima awe Muislamu, lakini inamaanisha kwamba kila nchi laima itatii na kutawaliwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Kwa wasio waislamu hatima yao imeelezwa katika aya tulizozinukuu hapo juu. Wakristo na Wayahudi wataruhusiwa kubaki na imani zao ili mradi watalipa kodi ya Jizya, kodi inatozwa kwa mwaka kwa mtu mzima, mtu huru, aliye timamu, na mwanamme kwa wasio Waislamu kama ilivyoelezwa katika aya za juu. Hakuna kiwango maalumu cha kodi ya Jizya, na kihistoria nchi zilizokuwa chini ya himaya ya Kiislamu kodi hii ilitozwa kutokana utashi wa mtawala na kulingana mahitaji husika. Kwa waliokuwa na imani za kidini nje ya Ukristo na Uyahudi, kuna chaguzi mbili tu: kuwa Muislamu au kufa. Wanazuoni pia wanasema Waislamu wanaweza kuwa na mkataba wa amani na wasio Waislamu ikiwa tu Waislamu ni dhaifu na hawawezi kuwashinda maadui zao. Katika mazingira kama haya wanaruhusiwa kuingia mkataba wa amani hadi pale watakapokuwa na nguvu zaidi hatua ambayo inawapasa kuvunja mkataba huo wa amani na kuanza vita vya Jihad.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 06:53 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)