Previous Chapter -- Next Chapter
13.1.4. Je nakala zote za Qur’an zinafanana na hakuna tofauti?
Madai kwamba nakala zote za Qur’an zinafanana na hakuna tofauti kabisa inamaanisha mambo mawili tu: ama huyo mtu ameona toleo moja tu ya Qur’an ya Kiarabu hivyo basi hajui ukweli wa wanachokiongea au wameamua tu kudanganya.Leo hii tuna matoleo tofauti ya Qur’an katika nchi tofauti. Mimi binafsi nina matoleo tofauti 5! Angalia sura ya kwanza ya Qur’an ya Moroko na ya Saudia. Katika ya Moroko aya ya “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwenye rehema na mwingi wa kurehemu haihesabiwi kama mojawapo ya aya za sura, lakini katika ya Saudia inahesabika kama aya ya kwanza. Aya ya saba katika toleo ya saudia “Njia ya wale uliowaneemesha, sio ya wale uliowaghadhibikia au ya wale waliopotea inahesabika kama aya ya 6 na Moroko aya ya 7. Hili inaweza kuonekana kama sio jambo la muhimu kwa wasio- Waislamu lakini ni muhimu sana kwa Waislamu, Kwa ssababu Waislamu wanachukulia yoyote anayekataa hata ya moja ya Qur’an kwamba sio Muislamu, japo wanatoa udhuru kwa aya ya kwanza kwa sababu Wanazuoni wa Kiislamu wa zamani na wa sasa hawakubaliani kama ni aya ya Qur’an au ufunguo tu wa wa kila sura ya Qur’an. Wanazuoni wa Kiislamu wa maoni matatu tofauti:
Hiyo ina maana ama tuna aya 111 zimeongezwa kwenye Qur’an, au 112 zimeondolewa au 1 tu imeongezwa. Hiyo ni kusema madai kwamba hakuna tofauti ni uongo kamili. Baadhi ya Wanazuoni wamejaribu kuzunguka na kusema:
Hata hivyo hiyo haijibu tatizo kabisa maana bado inabaki kwamba hatuna Qur’an moja kabisa iliyoungana ya Kiarabu ambayo haina tofauti.