Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 074 (Are all current copies of Qur’ans identical with no variants?)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
13.1. Imani juu ya kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili

13.1.4. Je nakala zote za Qur’an zinafanana na hakuna tofauti?


Madai kwamba nakala zote za Qur’an zinafanana na hakuna tofauti kabisa inamaanisha mambo mawili tu: ama huyo mtu ameona toleo moja tu ya Qur’an ya Kiarabu hivyo basi hajui ukweli wa wanachokiongea au wameamua tu kudanganya.Leo hii tuna matoleo tofauti ya Qur’an katika nchi tofauti. Mimi binafsi nina matoleo tofauti 5! Angalia sura ya kwanza ya Qur’an ya Moroko na ya Saudia. Katika ya Moroko aya ya “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwenye rehema na mwingi wa kurehemu haihesabiwi kama mojawapo ya aya za sura, lakini katika ya Saudia inahesabika kama aya ya kwanza. Aya ya saba katika toleo ya saudia “Njia ya wale uliowaneemesha, sio ya wale uliowaghadhibikia au ya wale waliopotea inahesabika kama aya ya 6 na Moroko aya ya 7. Hili inaweza kuonekana kama sio jambo la muhimu kwa wasio- Waislamu lakini ni muhimu sana kwa Waislamu, Kwa ssababu Waislamu wanachukulia yoyote anayekataa hata ya moja ya Qur’an kwamba sio Muislamu, japo wanatoa udhuru kwa aya ya kwanza kwa sababu Wanazuoni wa Kiislamu wa zamani na wa sasa hawakubaliani kama ni aya ya Qur’an au ufunguo tu wa wa kila sura ya Qur’an. Wanazuoni wa Kiislamu wa maoni matatu tofauti:

1) Ni sehemu ya Qur’an isipokuwa sura ya 9,
2) Ni sehemu yake lakini kwa sura ya kwanza tu, au
3) Sio sehemu ya sura yoyote ile.

Hiyo ina maana ama tuna aya 111 zimeongezwa kwenye Qur’an, au 112 zimeondolewa au 1 tu imeongezwa. Hiyo ni kusema madai kwamba hakuna tofauti ni uongo kamili. Baadhi ya Wanazuoni wamejaribu kuzunguka na kusema:

“Inapaswa kutambuliwa kwamba Uma kwa wingi wao umekubaliana kwamba sio anayeikubali au anayeikataa achukuliwe kama asiyeamini, kwa sababu ya tofauti ya maoni ya wanazuoni kuhusu hilo. Hii ni tofauti na mtu anayekataa neno ambayo kwayo kuna ridhaa au anayekubali kitu ambacho hakuna aliyekisema; huyo anatakiwa kuchukuliwa kama asiyeamini kulingana na makubaliano ya wanazuoni” (Ash-Shawkaani, Nayl al-Awtar, volume 2, Ukurasa 215).

Hata hivyo hiyo haijibu tatizo kabisa maana bado inabaki kwamba hatuna Qur’an moja kabisa iliyoungana ya Kiarabu ambayo haina tofauti.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:19 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)