Grace and Truth

This website is under construction !

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 085 (Rejection by family)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA SITA: FAHAMU WAONGOFU KUTOKA UISLAMU
SURA YA KUMI NA NNE: SHIDA ZA KIJAMII WANAZOKU TANA NAZO WAONGOFU WAPYA

14.1. Kukataliwa na familia


Labda hii ndio changamoto kubwa wanayokutana nayo kila, waongofu kutoka Uislamu na kuingia Ukristo dunia nzima. Familia watawatenga, watakataa kushirikiana nao tena, baba yangu mimi mwenyewe alienda polisi kutoa taarifa dhidi yangu kwa kuwa kwangu Mkristo, na miaka mingi baada kufa kwake, na mie kuwa nimeondoka nchini kwangu, niliporudi kwa kudhani mambo yamebadilika, mara kaka yangu tena akatoa taarifa tena Polisi.

Utamaduni wa Kiislamu umejengwa katika heshima/ aibu, mahali ambapo jambo jema la kijamii lina uzito unaovuka wa mtu binafsi, heshima ya familia ni kila kitu. Kuacha Uislamu ndio aibu kuu sana ambayo mtu anaweza kuipa familia yake. Hivyo kurejesha heshima hiyo mbele ya macho ya jamii, Familia itavunja ushirikiana wote na katika baadhi ya mazingira (Kwa huzuni sio mara chache kama ambavyo tungependa kufikiri) kumuua mwanafamilia aliyeitia aibu familia hiyo.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 02:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)