Previous Chapter -- Next Chapter
15.6. Fuata Maandiko matakatifu sio mitazamo yako
Usikwepe mambo ya msingi kwa sababu ya shauku ya kutokumkwaza mtu au kuumiza hisia zake, Kinyume chake zinahitaji kushughulikiwa.Miongoni mwa matatizo tunayokutana nayo maishani ni kwa sababu tumekuwa sana watu kujali ubinadamu sana. Mara nyingi tunafikiri kwamba tunajua namna maisha ynavyotakiwa kuwa kuliko Mungu. Ebu angalia kanisa linaloonekana leo. Tunajitahidi kudharau mafundisho ambayo tunadhani hayawezi kupokelewa katika jamii, na saa zingine kwa vitendo kabisa tunaweza kwenda kinyume nayo. Hii inaweza kumpa mwongofu mpya kibali cha kufanya hivyo hivyo, Bila kujirekebisha na kuendelea na matendo yasiyo ya Kibiblia ambayo wametoka nayo kutoka maisha yao ya zamani, au kudharau mafundisho wasiotaka kuyapokea. Mtume Paulo anasema: