Previous Chapter -- Next Chapter
14.5. Tishio la Kisheria
Katika nchi za Kiislamu, Kuacha Uislamu ni jinai na inaadhibiwa kwa kifungo cha jela; katika nchi chache, adhabu yake ni kifo. Hii kwa kawaida ni jambo la kuogofya sana! Kama muongofu mpya amejiunga na kanisa lako, Ni vizuri kujua hatari wanazochukua kwa kushirikiana na wewe, kuwa makini na hofu ya muongofu, na kuchukua tahadhari zote za kiusalama zinazowezekana. Hii haina maana kwamba tuwahimize Wakristo wapya kutokuchukulia maanani imani yao, Lakini kuna hatari fulani ambazo zipo na hazitakiwi kupuuzwa, Kwa namna yoyote tutaomba pamoja namuongofu na kumuombea pia, na kumsaidia kimwili (mwanafamilia wao) ikiwa wataishia kukamatwa na kufungwa.
Ikiwa ndio au la kwamba kanisa lako lina muongofu aliye hatarini, unaweza kutakiwa kufuatilia, kuchangia, au kujihusisha na kazi ya Mashirika ya Kikristo kama vile Barnabas Fund, Open Doors, na Voice of Martyrs ambao wanafanya kazi ya kulinda na kusaidia kanisa linaloteswa na watu binafsi. Mashirika hayo yana sehemu muhimu sana ya kufanya.