Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 013 (CHAPTER THREE: AXIOMS OF FAITH)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU

SURA YA TATU: NGUZO ZA IMANI


Uislamu unafundisha kwamba kuna nguzo sita za imani ambazo lazima kuziamini ili kuwa Muislamu na nguzo tano za faradhi za kutenda. Mafundisho haya kwa hakika hayapo kwenye Qur’an, kitabu kitukufu ambacho Waislamu wanaamini kiliamuriwa kwa Muhammad na Mungu, badala yake yanatoka kwenye Hadith, makusanyo ya maneno ya Muhammad yaliyopokelewa kwa njia ya simulizi kisha yakawekwa katika maandishi kwa ajili kumbu kumbu. Kuna makusanyo kadhaa ya Hadith, kila moja imeitwa kutokana na jina la mtu aliyezikusanya na kuziandika, huku makusanyo mingine zikizingatiwa kwa kuaminika zaidi kuliko zingine. Nguzo sita za imani na tano za faradhi za kutenda zote zinatoka katika mkusanyiko mmoja wa Hadith ambazo zilikusanywa na kuandikwa na mtu aliyeitwa Muslim, Mmojawapo wa wakusanya Hadith anayeheshimika sana na ambaye Hadith zake zinakubaliwa na Waislamu wa madhehebu ya Wa- Sunni wote. Ingawa kumbuka kwamba Waislamu wa madhehebu ya Sh’ia hawakubali Hadith zozote zilizokusanywa na Wa-Sunni, wao wanayo yao wenyewe. Waislamu wanasimulia kwamba siku moja Muhammad alipokuwa amekaa pamoja na kundi la wafuasi wake, mgeni mmoja aliyekuwa amevaa mavazi meupe alikuja kwa Muhammad na kumuuliza amwambie juu ya Uislamu; Muhammad akamjibu kwa kuorodhesha kinachojulikana leo kama nguzo za faradhi kutenda za Uislamu. Mgeni aliuliza pia juu ya Imani, na Muhammad akamjibu majibu ambayo leo yanajulikana kama nguzo sita za imani.Kulingana na Waislamu, mgeni huyo alithibitisha ukweli wa alichokisema Muhammad, kisha akaondoka, wakati huo, Muhammad akafichua kwa kundi ya wafuasi wake waliokuwa pamoja naye kwamba yule mgeni alikuwa ni Malaika Gabriel.

Sura hii itaangazia nguzo sita za imani, na sura inayofuata itaeleza mukhtasari wa nguzo tano za Uislamu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 08, 2024, at 06:15 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)