Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 014 (AXIOM 1: Belief in the existence and oneness of God (Allah))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA TATU: NGUZO ZA IMANI

3.1. IMANI 1: Imani katika uwepo na umoja wa Mungu (Allah)


Kama ilivyosimuliwa kwenye sura ya awali, mafundisho mengi ya Muhammad ya mwanzo hayakupingana kwa kiwango kikubwa na mafundisho ya Wakristo na Wayahudi waliomzunguka (Ingawa ikumbukwe kwamba Wakristo wengi katika Ghuba ya Uarabuni walifuata mafundisho ya uzushi), na kwa kweli Uyahudi ulishawishi na kuathiri kwa kiwango kikubwa sana machakato wa awali wa Uislamu. Hadi leo, tunaona kulingana kwingi kati ya hizi dini mbili, ingawa nyingi katika mambo haya yamechukuliwa kinyume na maudhui halisi na yaliyokusudiwa ya Agano la Kale na pia hayana uwiano ndani ya muk’tadha wa Uislamu. Na hivyo tunaona kwamba ingawa dhana ya mwisho ya Mungu katika Uislamu ni tofauti kabisa na ile ya Mungu wa Biblia, Muhammad awali alidai kumfuata Mungu Yule Yule wa Wayahudi na Wakristo. Wakati alipokuwa akijaribu kuwashawishi wamuamini yeye, amenukuliwa katika Qur’an akisema:

“Wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja.Na sisi ni wenye kusilimu.” (Qur’an 29:46)

Na ingawa pia dini mpya ya Muhammad haikuwavutia Washirikina wa Maka, kwa hakika kulikuwa na baadhi ya vipengele alivyochukua kutoka kwao.

Kwa mfano jina Allah, ilikuwa ikitumika kabla ya Uislamu. Kwa hakika, ilikuwa sehemu ya jina la baba yake Muhammad, Abdallah (mtumwa wa Allah). Kuna mjadala kiasi kuhusu jina hili hasa inamaanisha nini na inamrejea nani; nadharia mojawapo ni kwamba inamrejea mungu mwezi, wakati wapo wanaoshikilia dhana ya kwamba ilitumika kumpwekesha sanamu maalumu ya washirikina. Bado nadharia nyingine inasimulia kwamba jina hili lilitumika kumweleza, mungu mkuu na muumbaji aliyewazidi hadhi miungu mingine yote ya Wapagani, Mara ya kwanza, Muhammad alijaribu hata kuwashawishi wenyeji kwamba Allah hakuwa mungu mpya lakini ni Yule wanayemjua na ambaye wamekuwa tayari wakimuabudu. Hii haimaanishi kwamba Muhammad alikubaliana na kila kitu kilichotendwa kabla yake na Waarabu, Wakristo au Wayahudi- alionekana kuchukua kwa kuchagua kutegemeana na mazingira ya wakati husika- kwa hakika dhana ya mwisho ya Allah kama inavyotolewa ndani ya Qur’an ni tofauti kabisa na Mungu wa Biblia, lakini mawazo ya mtume ya mwanzoni ya Allah kwa kiwango fulani yalichangiwa na imani za watu waliomzunguka.

Ili kufahamu mtazamo wa Uislamu juu ya Allah, tunalazimika kwanza kufahamu misingi ya mafundisho ya kiimani ndani ya Qur’an: Hana umbile, hafungwi na mpangilio wa uumbaji na yu kinyume nayo. Haya yanaweka msingi wote wa ufahamu wa Muislamu juu ya asili ya Allah.

Katika Uislamu, Allah ameondelewa kutoka katika uumbaji wake ya kwamba hakuna chochote kinachofanana naye. Wanazuoni wa Kiislamu wanasema kwamba chochote kinachokuja kwenye akili yako wakati unapomfikiria Allah, yeye ni kitu kingine kabisa kinyume na hicho ulichofikiria. Fundisho hili la imani inajulikana kama “tanzih” au iliyo kinyume na maumbile yoyote. Hii ni muhimu sana, ikimaanisha kwamba kusema jambo lolote kuhusu Allah ni suala lisilowezekana kwa maana haitakuwa kweli kuhusu yeye na yeye atadumu kuwa namna nyingine. Hii kwa msingi inamfanya Allah kutokujulikana kabisa. Katika simulizi mojawapo ya Hadith, Muhammad inasimuliwa kuwahi kusema kwamba: “Fikiria juu ya uumbaji wa Allah lakini kamwe usimfikirie Allah mwenyewe.” Hii, bila shaka, ni kinyume kabisa na kinachofundishwa na Biblia juu ya Mungu, Inayotaja wazi kabisa kwamba tuliumbwa kwa ajili ya kuwa na mahusiano pamoja na Mungu, kwa lengo kuu ya Kumjua.

Fundisho la pili, ni kwamba yeye yuko kinyume na uumbaji (au mukhaalafa), inafundisha kwamba hakuna kufanana kokote baina ya Allah na uumbaji wake. Haiko wazi katika elimu ya dini ya Uislamu kama hii inajumuisha kila kitu pamoja na kuwa Allah ana matendo yake, au inaongelea tu asili ya Allah. Kwa mfano, tukisema ya kwamba Allah anasikia maombi, je tunafahamu hili namna tunavyofahamu kwa kawaida neno kusikia? Wanazuoni wa Kiislamu wanatofautiana kama tunapaswa kuhoji hilo au la. Hivyo basi hii inafanya iwe ngumu sana kujua taarifa yoyote itolewayo juu ya Allah.

Kwa mfano, Wanazuoni wanasema ya kwamba pindi Qur’an inapoongelea mikono ya Allah, haimaanishi Allah kuwa na mikono halisi; hata hivyo, sivyo tunavyofikiria katika muk’tadha wa mikono halisi bali kile kinachofaidisha utukufu wake kwa vyovyote alivyotaka yeye iwe. Kwa bahati mbaya hiyo haituambii lolote kuhusu Allah zaidi ya: Allah anamaanisha chochote anachomaanisha (Lakini hatujui hicho anachokimaanisha ni nini).

Tunaweza kuona kwamba matokeo ya kanuni hizi mbili za msingi ni kuwa, hatuwezi kuwa na uelewa wa mafundisho mengine ya Allah maana haiwezekani kusema lolote juu yake kwa sababu hiyo itakuwa inaenda kinyume na hizi kanuni mbili za msingi na hivyo kufanya yaliyosemwa kuwa ni uongo.

Tukikumbuka hizi kanuni mbili akilini, na tuangazie baadhi ya mafundisho mengine juu ya Allah, Katika Qur’an, tunakutana na rejea ya “majina yaliyotukuka” ya Allah (Qur’an 7:180). Kwa ujumla Waislamu wanasema kwamba anayo majina 99, lakini hakuna makubaliano ya jumla ya kuwa majina haya 99 ni yepi hasa, Kwa kweli wanazuoni wengine wamehesabu hadi kufikia idadi ya majina 276 tofauti. Muelekeo ni kwamba kila mmoja wao anakubaliana na kuaminika (Ufasaha) kwa simulizi tofauti ya makusanyo ya Hadith. Kama ilivyoonyeshwa awali. makusanyo mengine yanakubalika sana, huku meingine hayapewi uzito na Madhehebu ya Ki- Sunni (Mfano wa makusanyo hayo ni Muslim na Bukhari), lakini megine kwa ujumla wake hayakubakili kwa kiwango kikubwa. Majina ya Allah lazima yatajwe wazi wazi katika Qur’an au Hadith, na yasigawanyike Kati ya kitenzi na matendo. Kwa mfano, Waislamu wanaweza kumuita Allah “al-Qahhar” – “Anayetawala kila kitu” maana jina hii ipo ndani ya Qur’an (Qur’an 39:5), Lakini hawawezi kumuita Allah “al-Aati”- Mpaji au Mtoaji”- maana jina hilo kwa namna hiyo ya kipekee haipo ndani ya Qur’an au Hadith ingawa Allah ameelezwa kwa sifa za kuwa mtoaji na mpaji pahala pengi ndani ya Qur’an. Sababu mojawapo ya waislamu kusema majina hayawezi kuitwa kutokana na matendo ni kwamba baadhi ya matendo ya Allah hayawezi kuwakilisha asili yake ya kutobadilika badilika, matendo hayo yanaweza kutafsirika katika mazingira ambayo yalisababisha yakatendeka. Kwa mfano, Haiwezi kusemwa kwamba Allah ni mdanganyifu, ingawa inasimuliwa katika Qur’an ya kuwa aliwadanganya wanafiki (Qur’an 4:142).

Utata mwingine ni kwamba ( kama ilivyo mada katika Uislamu) hakuna makubaliano ya jumla ya wanazuoni juu ya nini inaweza na inapaswa kujadiliwa; Baadhi ya wanazuoni wanasema asili ya Allah haipaswi kujadiliwa kwa vyovyote vile, wakati wengine wanaona hakuna tatizo katika hilo.

Hivyo tunaishia kupokea katika hali ya ukinzani na yasiyoweza kujulikana tu. Allah hana umbo la Kimwili, na bado Waislamu wataona umbo lake halisi peponi, zaidi ya hapo, anakaa katika kiti cha enzi-ambacho Waislamu wanaamini ni kiti halisi cha enzi. Hajatwaa utu au mwili, lakini bado ana mikono, uso, miguu na ubavu- ambayo Waislamu wote wanaamini kuwa sehemu halisi za mwili wake. Yupo popote na anakuja mahali na kuondoka, imani kama hiyo inamkanganya mtu yoyote anayejaribu kupata mfumo fulani muhimu wa uelewa sahihi ndani yake. Matokeo yake Waislamu wengi wanaishia kukubaliana na ukinzani kama kitu kisichoweza kuelezeka.

Kwa kuweka katika matendo ufahamu wa namna hiyo juu ya Allah, utakuta kwamba, ndio sababu Waislamu wanaamini kwamba kila kitu kilishaamuliwa kabla na Allah na kwamba hakuna chochote mwanadamu anaweza kufanya kubadilisha chochote na ya kwamba hata matendo yao wenyewe yameumbwa na Allah, Uislamu ndio mfumo mbovu wa imani katika historia. Inakwamisha kiu ya maendeleo ya mwanadamu kwa sababu Waislamu wameshakubaliana kabisa ya kuwa huwezi kufanikiwa chochote zaidi au kidogo kuliko kilichoamuriwa na hatma au kudra kwa ajili yako. Bila kujali unafanya nini.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 08, 2024, at 06:35 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)