Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 030 (Christ’s Miraculous Birth)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TATU: FAHAMU KRISTO MUISLAMU
SURA YA SITA: KRISTO KATIKA UISLAMU

6.2. Kuzaliwa kwake Kristo Kimuujiza


Qur’an inafafanua mazungumzo ya Mariamu na Malaika Gabriel, na mengine juu ya Mariamu na mtoto Isa kuhusu kutungwa mimba kwake na kuzaliwa kwake. Yote haya yanatolewa katika sura moja ndani ya Qur’an:

“Na (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamungu. (Malaika) akasema :Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliyetakasika. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanadamu hajanigusa. Wala mimi sio kahaba? (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ishara kwa watu, rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lililokwisha hukumiwa. Basi akachukua mimba nayo mpaka mahali pa mbali. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina ya mtende; akasema laiti ningelikufa kabla ya haya na nikawa niliye sahaulika kabisa! Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejalia chini yako kijito kidogo cha maji! Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yoyote basi sema : Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga kwa hivyo leo sitasema na mtu” (Qur’an 19: 18-26)

Kwa njia maalumu Qur’an inamuita Kristo “Mwana aliyetakasika” kama alivyosema Muhammad:

“Hakuna mtoto anayezaliwa lakini, Shetani anamgusa anapozaliwa ambapo anaanza kulia kwa nguvu kwa sababu ya kuguswa na shetani, isipokuwa Mariamu na Mwana wake” (Sahih Bukhari).

Kulingana na Muhammad, kila mwanadamu anaguswa na Shetani hilo ikimjumuisha Muhammad hivyo alitakiwa kutakaswa kama tulivyoona hapo awali- isipokuwa Kristo. Hivyo Kristo hana dhambi kulingana na Uislamu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 12:22 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)