Grace and TruthThis website is under construction ! |
|
Home Afrikaans |
Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 096 (Avoid special treatment)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?
Previous Chapter -- Next Chapter 17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA SITA: FAHAMU WAONGOFU KUTOKA UISLAMU
SURA YA KUMI NA TANO: USHAURI KWA KANISA
15.5. Epuka upendeleo maalumuWakati mtu anapokuja katika imani, hii ni miongoni mwa sababu za furaha kuu. Tunaweza kujaribiwa kufikiri kwamba anayeokoka kutoka Uislamu ni muujiza mkuu kuliko wa Yule anayetoka kwenye ukristo wa jina, ingawa badiliko la moyo ni kazi kubwa ya Bwana. Kunaweza kuwa na tabia ya kumweka muongofu mpya mahali pa juu pa weko, kumchukulia katika umaalumu kuliko kutambua kwamba Mkristo mpya bado wanahitaji kutiwa moyo, kusaidiwa, kuwa na nidhamu kama vile tu ilivyo kwa waamini waliotoka kwenye asili zingine. Kwa ungalifu mkubwa inaweza kuwa jambo lenye afya, inaweza kukaza zaidi kwenye ushuhuda wao binafsi kuliko kazi ya Yesu inayoendelea kwenye maisha yao. |