Previous Chapter -- Next Chapter
6.5. Kristo alinyakuliwa kwenda mbinguni
Mafundisho ya kiislamu juu ya mwisho wa maisha ya Kristo duniani yanachanganya. Qur’an inasema:
Wanazuoni wa Kiislamu hawako wazi na hawana uhakika kuhusu kipi kinachomaanishwa na Qur’an kwa kutumia neno lililotafsiriwa kama “Nitakufisha”, neno la Kiarabu linalotumika, “mutawaffeeka” inamaanisha kifo kama kusulubiwa ni mojawapo ya kweli kadhaa zilizothibitishwa uhalisia wake wa kihistoria na wanazuoni wa Kiislamu wamejaribu kupatanisha mafundisho ya Qur’an kuhusu kifo chake na uhalisia wa kusulubiwa kwake kihistoria. Neno mutawaffeeka lina utata kuhusu inamaanisha nini hasa hii imefanya kuwa na tafsiri nyingi tofauti kuhusu aya yenyewe. Wanazuoni wachache wanaamini kwamba aya hii inamaanisha Kristo alikufa na kufufuka (Kama Wakristo wanavyoamini) lakini wengi wao hawaamini hivyo. Baadhi husema hilo la kufa haijatokea lakini itatokea badaye: Atakuja kufa na kufufuka kutoka kwa wafu. Wengine husema Allah atakuja kumzawadia Kristo, wengine wanasema atainuliwa kwa hadhi ya juu kuliko mtu yoyote Yule, na bado wengine wanasema alinyanyuliwa juu mbinguni kimwili kabisa na atarudi tena.