Previous Chapter -- Next Chapter
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
Katika sura hii, tutalenga tofauti za kitheolojia za Kiislamu na Ukristo. Hii lazima ndio itakuwa ndefu zaidi katika sehemu hii. Na pia bado haitatoa upana kamili wa mjadala huu, lakini ni matumaini kwamba itakusadia katika matarajio ya kushughulika na baadhi ya mapingamizi ya kawaida dhidi ya ujumbe wa Ukristo.
Nyingi katika mapingamizi haya ni rahisi kushughulika nazo na zinaangukia mbali na misingi sahihi ya uchambuzi. Wakati mwingine tunahitaji kumuuliza tunayewasiliana naye kama yupo tayari kutumia njia hiyo hiyo ya kupinga kwa dini zote mbili Uislamu na Ukristo, maana kupinga kitu katika Ukristo na huku unakikubali kitu hicho hicho katika Uislamu ni kukosa msimamo wa wazi kabisa na haina mantiki (Kama vile kupinga vita vya Msalaba lakini kukubali mauaji ya watu wa Armenia, au Muhammad kuwauwa Wayahudi kule Madina). Nitajaribu kutoa majibu juu ya baadhi ya mambo ya kawaida wanayopinga Waislamu kuliko kuorodhesha baadhi ya mapingamizi ya kawaida tunayopata kutoka kwa watu wasio Wakristo, kama vile dhana ya kuto-kuwepo kwa Mungu, au kufanana kwa baadhi ya mafundisho ya Ukristo na yale ya kipagani.
Waislamu wanatakiwa kujadiliana mambo ya dini na Wakristo kwa namna ambayo imeelezwa ndani ya Qur’an:
Hiyo ni kusema:
- Wanapaswa kujadiliana kwa maneno mazuri na kwa tabia nzuri.
- Wanapaswa kuamini katika vitabu vilivyokuja kabla ya Muhammad.
- Wanapaswa kuamini kwamba wanamuabudu Mungu mmoja na Wakristo na Wayahudi na sote tunapaswa kumtii.
Kama mazungumzo yakipamba moto, basi, unatakiwa kuwakumbusha kinachofundishwa na Qur’an.
Sasa basi, mapingamizi ya Waislamu kwa ujumla yanaangukia katika mojawapo ya makundi haya, ambayo tutarudi kuyajadili.
- Imani juu ya Kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili.
- Changamoto juu ya uhalali wa Biblia maana wanaamini imekwisha tenguliwa (Imefutwa na kubadilishwa).
- Mapingamizi juu ya Utatu.
- Mapingamizi juu ya Kusulubiwa kwa Kristo.
- Madai ya Unabii juu ya Muhammad katika Biblia.