Grace and TruthThis website is under construction ! |
|
Home Afrikaans |
Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 069 (CHAPTER THIRTEEN: MUSLIM OBJECTIONS TO CHRISTIANITY)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?
Previous Chapter -- Next Chapter 17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTOKatika sura hii, tutalenga tofauti za kitheolojia za Kiislamu na Ukristo. Hii lazima ndio itakuwa ndefu zaidi katika sehemu hii. Na pia bado haitatoa upana kamili wa mjadala huu, lakini ni matumaini kwamba itakusadia katika matarajio ya kushughulika na baadhi ya mapingamizi ya kawaida dhidi ya ujumbe wa Ukristo. Nyingi katika mapingamizi haya ni rahisi kushughulika nazo na zinaangukia mbali na misingi sahihi ya uchambuzi. Wakati mwingine tunahitaji kumuuliza tunayewasiliana naye kama yupo tayari kutumia njia hiyo hiyo ya kupinga kwa dini zote mbili Uislamu na Ukristo, maana kupinga kitu katika Ukristo na huku unakikubali kitu hicho hicho katika Uislamu ni kukosa msimamo wa wazi kabisa na haina mantiki (Kama vile kupinga vita vya Msalaba lakini kukubali mauaji ya watu wa Armenia, au Muhammad kuwauwa Wayahudi kule Madina). Nitajaribu kutoa majibu juu ya baadhi ya mambo ya kawaida wanayopinga Waislamu kuliko kuorodhesha baadhi ya mapingamizi ya kawaida tunayopata kutoka kwa watu wasio Wakristo, kama vile dhana ya kuto-kuwepo kwa Mungu, au kufanana kwa baadhi ya mafundisho ya Ukristo na yale ya kipagani. Waislamu wanatakiwa kujadiliana mambo ya dini na Wakristo kwa namna ambayo imeelezwa ndani ya Qur’an: “Wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja: Na sisi ni wenye kusilimu” (Qur’an 29:46)
Hiyo ni kusema:
Kama mazungumzo yakipamba moto, basi, unatakiwa kuwakumbusha kinachofundishwa na Qur’an. Sasa basi, mapingamizi ya Waislamu kwa ujumla yanaangukia katika mojawapo ya makundi haya, ambayo tutarudi kuyajadili.
|