Previous Chapter -- Next Chapter
15.9. Usitumie misamiati ya Kikristo
Mara nyingi lugha na maneno wanayotumia Wakristo hayana maana yoyote kwa Waislamu, Mara nyingi zinakuwa hata za kukwaza. Nakumbuka wakati nilipokuwa mwongofu mpya na niliulizwa na mtu mmoja kanisani kama nimesafishwa kwa damu ya mwana kondoo. Sikuwa na uelewa huyu mtu alikuwa anaongelea nini! Nilifikiri ilikuwa ni kutawadha kwa Wakristo ndio kusafiswa kwa damu ya mwana Kondoo na nikajikuta imenisumbua sana. Mwongofu mpya ananyonya taarifa hizi zote kama vile Sifongo; kila kitu ni kipya kwao, kitu fulani kinaweza kisieleweke kwa kirahisi tu. Hivyo epuka kutumia misamiati migumu bila sababu za muhimu, au ambayo maana yake haitaeleweka kwa haraka kwa mtu ambaye hajakulia kanisani.