Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 025 (PILLAR 5: Hajj (pilgrimage))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA NNE: NGUZO ZA UISLAMU

4.5. NGUZO 5: Hajj (Hija)


Hija ni nguzo ya tano ya Uislamu. Ni hija inayofanywa kwenda kuzuru miji mitakatifu ya Waislamu ya Maka na Madina katika nchi inayojulikana leo kama Saudi Aarabia, na mara zote inafanyika wakati ule ule kila mwaka kulingana na kalenda ya Kiislamu. Ni takwa la lazima kwa kila Muislamu aliye huru, mtu mzima, mwenye afya ya akili timamu, na aliyesawa kimwili na kiuchumi angalau mara moja katika maisha. Kulingana na Uislamu, ibada ya hija iliasisiwa na Ibrahimu anayesemekana kuwa ndiye aliyeijenga al-kaba baada ya kuwa ilijengwa hapo awali na Adam. Hija inaanza katika siku ya nane ya Dhual-Hijjah, mwezi wa kumi na mbili ya kalenda ya Kiislamu na inamalizika siku ya kumi na tatu ya mwezi huo huo.

Hija inajumuisha ibada mbali mbali tofauti, inaanza kwa maandalizi yanayojulikana kama Ihram. Kwa mwanamme, inatakiwa avae nguo nyeupe zisizofumwa, na moja ikiwa imevaliwa kuanzia kifuani hadi kufikia magoti, na nyingine imefungwa kutoka bega ya kushoto na ya kulia; Mwanamke anapaswa kuvaa mavazi ya kawaida ya rangi yoyote huku kichwa chake kimefunikwa lakini uso wake na mikono yake iwe wazi. Mahujaji hawatakiwi kushiriki tendo la ndoa, kunyoa au kukata kucha zao, hawatakiwi kujipuliza mafuta yenye manukato au yenye harufu nzuri, hawatakiwi kuua au kuwinda wanyama, kugombana na kubishana. Wanawake hawatakiwi kufunika nyuso zao, hata kama wanafanya hivyo katika nchi zao. Wanaume hawatakiwi kuvaa mavazi ya kushonwa. Kuoga kunaruhusiwa lakini sabauni zinazonukia haziruhusiwi.

Baada ya Ihram, Waislamu wanapaswa kutangaza nia, au Niyah. Kisha wanatembelea pembezeni mwa Mina Katika Maka siku ya nane ya Dhul Hijjah na wanabaki huko hadi machweo ya kesho yake asubuhi.Kisha wanasafiri hadi bonde la Arafat na kisha wanasimama mahala pa wazi, wakimsifu Allah. Miwsho wa siku, Wanasafiri hadi karibu na eneo la Muzdalifa kwa ajili ya mapumziko ya usiku, ambapo wanakusanya pamoja mawe madogo madodgo ya kutumia kesho yake. Asubuhi wanarejea Mina na kurusha mawe kwa nguzo zinazoitwa Jamarat. Hizi nguzo za mawe zinawakilisha shetani. Kisha wanachinja mnyama kukumbuka habari ya Ibrahimu na mtoto wake (Anayeaminika kuwa ni Ishmael, na sio Isaka kama Biblia inavyoeleza). Kukumbuka jambo hili wana desturi ya kuchinja kondoo au mwanakondoo, japokuwa kwa siku hizi mahujaji wananunua vocha wakiwa Maka kabla ya Hija kuanza, inayoruhusu mnyama kuchinjwa kwa jina la Allah siku ya 10th bila ya mahujaji wenyewe kuwepo binafsi kwenye tukio. Kivyovyote vile, nyama inagawanywa kwa masikini. Baada ya hili, Wanaume wananyoa vichwa vyao na wanawake wanakata ufungio wa nywele zao. Kisha wanarudi Maka kwa ajili ya Tawaf, ambayo ni ibada ya kuizunguka al-kaba mara saba. Kisha wanarudi Mina kwa siku 3 au 4, wakizipiga mawe nguzo zinazomwakilisha shetani kila siku.

Mwisho wanamalizia kuaga Tawaf kwenye al-kaba katika siku ya kumi na mbili ya mwezi wa Dhul Hijjah, wakimuomba Allah msamaha kwa ajili dhambi zote walizowahi kuzifanya katika maisha yao yote, na Hija inakuwa imekwisha.Waislamu wengi baada ya hapa hutembelea Msikiti alikozikwa Muhammad huko Madina, lakini hii haijaainishwa kuwa sehemu ya Hija.

Baadhi ya Waislamu siku hizi wanafanya kuhiji mara nyingi kwa mda wa maisha yao na baadhi wanakwenda kila mwaka hata kama sio takwa la kiimani kwao. Katika baadhi ya nchi ni ishara ya hadhi ya kijamii na kidini; Kila mtu anapoongeza idadi za safari za kuhiji ndivyo hadhi yake inavyokuwa juu zaidi.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 06:21 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)