Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 024 (PILLAR 4: Zakat (almsgiving))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA NNE: NGUZO ZA UISLAMU

4.4. NGUZO 4: Zakat (Utoaji wa zaka)


Nguzo ya nne ya Uislamu ni utoaji wa zaka. Waislamu wanatakiwa kutoa kiasi cha 2.5% ya mapato waliochuma katika kipindi cha mwaka kwa kiasi kilichowekwa. Kuna mazingira machache ambapo Waislamu wanatakiwa na wanahimizwa kutoa pesa kwa ajili ya kusaidia jamii, kama vile pesa ya kulipia kosa.

Qur’an inataja kwa kipekee makundi ya watu ambao wanatakiwa kufaidika na zaka, lakini ni juu ya mtu binafsi kuamua kwamba awape wafaidika hao moja kwa moja au atoe kwenye msikiti wa mahali husika kisha msikiti huo ndio ugawe kwa walengwa. Kuna matumizi nane yanayokubalika ya zaka:

“Wa kupewa sadaka Ni mafakiri, Na masikini, Na wanaozitumia, Na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, Na katika kukomboa watumwa, Na wenye madeni, Na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu uliofaridhiwa na Mwenyezi Mungu." (Qur’an 9:60)
  1. Mafakiri. Neno la Kiarabu fuqara ni neno la jumla kwa wote wasioweza kujimudu kwa sababu ya ulemavu au uzee, au wanaohitaji msaada wa dharura kama vile yatima, wajane, na wasio na ajira na kadhalika.
  2. Masikini. Neno la Kiarabu la masakin inamaanisha wale ambao ni walala hoi na hivyo hawawezi kupata mahitaji ya muhimu ya kibinadamu.
  3. Na wanaozitumia.Hii kwa msingi inamaanisha wale wanaofanya shughuli za utawala katika kukusanya na kugawa sadaka, bila kujali ya kwamba wao wenye uhitaji wa fedha au la- ni aina Fulani ya malipo ya uendeshaji.
  4. Na wa kutiwa nguvu nyoyo zao. Sehemu ya zaka inatakiwa kutolewa kwa ajili ya kuwavuta wasiokuwa Waislamu kujiunga na Uislamu, Kwa ajili ya wasio Waislamu wanaoweza kuajiriwa na jamii ya Kiislamu katika kiuhalisia, au kwa ajili ya Waumini wapya waliojiunga na Uislamu ambapo wanaweza kurudia imani yao ya zamani kama hakuna msaada wa fedha utakaotolewa kwa ajili yao. Inaruhusiwa kuwafidia watu walioko katika makundi haya, au kuwapa kiasi cha fedha kwa lengo la kueneza Uislamu,au kuwafanya wawe watiifu,au kuwafanya maadui wasiwe na madhara. Sehemu hii kwa sasa inatumiwa zaidi katika kampeni za hadhara au kugharamia vipindi vya vyombo vya habari ili waongelee uzuri wa Uislamu. Kuna maoni tofauti kama matumizi ya fedha namna hii bado ni halali kwa sasa.
  5. Kukomboa Watumwa. Fedha za zaka zinaweza kutumika kama kikombeleo ya watumwa kwa njia mbili. Kwanza, kama msaada wa fedha kwa mtumwa kama malipo ya kikombeleo, ambapo mtumwa anaingia makubaliano na bwana wake kwamba atamwachia huru ikiwa mtumwa huyo atalipa kiasi fulani cha fedha. Njia ya pili ni kama serekali ya Kiislamu yenyewe italipa moja moja fedha kwa ajili ya uhuru wa mtumwa huyo kwa bwana wake. Wanazuoni wanakubaliana kwamba njia ya kwanza ni halali, lakini kuna maoni tofauti kama fedha inaweza kutolewa kwa serekali kununua uhuru wa Mtumwa.
  6. Kusaidia wenye mzigo wa madeni. Zaka inaweza kutolewa kwa wadaiwa ambapo wanaweza kuwa mafukara ikiwa watalipa madeni yao yote wanayodaiwa kutoka katika vitu wanavyomiliki, bila kujali kuwa wanaingiza fedha au la.
  7. Katika njia ya Mwenyezi Mungu. Japo neno hili linaweza kumaanisha jambo lolote litendwalo kwa ajili ya Allah, lakini Wanazuoni wengi wa Kiislamu wanakubaliana kwamba inamaanisha kuhangaika (Jihad) kwa lengo la kuondoa mfumo wa utawala wa kijamii, kisheria na kisiasa usiofuata misingi ya Kiislamu na kuweka badala yake mfumo wa utawala wa kijamii, kisheria na kisiasa unaofuata misingi ya Kiislamu. Hivyo basi zaka inagharamia mambo yanayowezesha kufikia lengo hilo kama vile silaha au vifaa vingine vinavyohitajika kwa ajili ya Jihad.
  8. Wasafiri. Fedha za zaka zinaweza kutolewa kwa Muislamu aliye safarini hata akiwa ni mtu mwenye uwezo nyumbani. Baadhi ya wanazuoni wanasisitiza kwamba safari yenyewe lazima isiwe ya sababu za kutenda dhambi, lakini hakuna sharti hilo katika Qur’an.

Baadhi ya nchi za Kiislamu wana wizara inayoshughulika na masuala ya dini ambayo inawajibika kwa ajili kukusanya na kutumia zaka. Maana pia Qur’an haijaweka mipaka ya kiojiografia katika kutumia zaka, baadhi ya nchi wanazitumia katika nchi za nje, aidha kwa misaada ya kibinadamu kama vile majanga, au kugharamia vita vya nchi ya Kiislamu dhidi ya nchi nyingine isiyo ya Kiislamu (Kugharamia kundi la Kiislamu la Palestina la Hamas, kwa mfano) au hata kugharamia nchi ya Kiislamu iliyoko vitani na nchi nyingine ya Kiislamu (kama vile kugharamia Iraq katika vita vyake dhidi ya Iran).

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 06:13 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)