Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 072 (Did Mohammed immediately dictate the Qur’an to his companions who wrote it down without any editing?)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
13.1. Imani juu ya kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili

13.1.2. Je Muhammad pale pale aliiamuru Qur’an kwa masahaba wake walioiandika chini bila kuihariri?


Muhammad kuamuru pale pale kwa masahaba wake pia haiungwi mkono na vyanzo vya kihistoria vya Kiislamu. Tunaambiwa pia kwamba Muhammad mwenyewe ali-hariri Qur’an alipokuwa akiisoma kwa dharura:

“Imepokelewa na Zaid bin Thabit kwamba Mtume alimsomea: ‘Hawalingani waamini ambao wanakaa (nyumbani) na wale wanaojitahidi na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu’…. Zaid akaongeza ‘Ibn Umm Maktum akaja wakati Mtume alipokuwa akinisomea na kusema “Ewe Mtume wa Allah. Naapa Kwa Allah, kama ningekuwa na uwezo wa kupigana (Katika njia ya Allah) ningefanya” na alikuwa ni kipofu. Hivyo basi Allah akafunua kwa Mtume wake wakati paja lake lilikuwa juu ya paja langu, na paja likawa nzito mpaka nikaogopa ingeweza kuvunja paja yangu. Kisha hali ya Mtume ilipoisha na Allah akafunua “Isipokuwa wale wasiojiweza (Wenye majeraha, au vipofu, au vilema).”

Baada ya Muhammad kufa, Masahaba wake wake walisema kwamba sura za Qur’an kamili zimepotea na hatuko nazo. Mmoja wa masahaba wa Muhammad, Abu Musa Al-Ashari alitumwa kwenda kwa waliokuwa wamekariri kwa watu wa al-Basrah, na watu mia tatu waliokuwa wamehifadhi Qur’an wakaja kumuona. Akasema:

“Nyinyi ndio watu bora wa jamii ya al-Basrah na wenye kukariri wao, hivyo mkariri na kusoma, lakini msiache maisha marefu yasababishe mioyo kuwa migumu kama ilivyokuwa mioyo ya waliowatangulia. Tulikuwa tukisoma Sura ambayo tuliifananisha kwa urefu na nguvu kama Sura ya A-Bar.aah ( Kwa leo inaitwa at-Tawbah), halafu nilisababishiwa kuisahau lakini nakumbuka sehemu yake (maneno). ‘Kama mwana wa Adamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali, angelitamani ya tatu, lakinia hakuna kitakachojaza tumbo ya mwana wa Adamu isipokuwa ni mavumbi’. Na tulikuwa tukisoma sura tuliyoifananisha na Musabbihât, Lakini nilisababishiwa kuisahau lakini nakumbuka sehemu ya maneno yake: ‘Enyi mnaoamini! Kwa nini mnasema msioyatenda, itaandikwa kama ushahidi kwenye shingo zenu, na mtaulizwa juu yake siku ya ufufuo” (Sahih Muslim)

Sura hii kwa sasa haina sehemu yoyote ndani ya Qur’an ya leo, Hivyo tuna sura inayokosekana, au Sahih Muslim (Ambaye Waislamu wanamchukulia kama mkusanya hadith wa pili kwa usahihi zaidi) amekosea kuhusu kukusanya Qur’an na hivyo basi hawezi kuaminika (ambacho itasababisha kila aina ya matatizo).

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:12 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)