Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 073 (Was there only one version of the Qur’an?)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
13.1. Imani juu ya kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili

13.1.3. Je Kume kuwako na toleo moja tu ya Qur’an?


Kukuza madai kwamba kumekuwako na toleo moja tu ya Qur’an haina miguu katika ushahidi wa kihistoria. Kiyume chake, tunachokijua kutoka kwenye vyanzo vya Kiislamu ni kwamba hatukuwa na toleo moja tu ya Qur’an lakini tulikuwa nazo saba. Matoleo haya yanajulika kama “ahruf” –maneno alifabeti. Maana halisi ya neno “ahruf” kama ilivyokusudiwa katika mazingira haya haiko wazi na imetafsiriwa katika namna mbali mbali tofauti (mbinu, mtindo au aina, tofauti na kadhalika). Kwa jumla inakubalika kwamba inamaanisha matoleo tofauti yenye maudhui tofauti ama angalau maneno tofauti. Hizo saba zilikuwa tofauti sana kwa kiasi ambacho baadhi ya masahaba wake Mtume hawakuwezza kuzitambua kama zinatoka kwenye Qur’an. Bukhari anaandika ugomvi baina ya Umar ibn al-Khattab na Hisham bin Hakim wakati wa uhai wa Muhammad. Hisham alikuwa akisoma Sura katika Qur’an: Umar akasema

“Nimesikia kusoma kwake, nikagundua kwamba anasoma kwa namna tofauti ambayo Mtume wa Allah hajanifundisha Nilikaribia kumrukia wakati wa Salat (Sala). Lakini nikadhibiti hasira yangu. Alipomaliza Salat (Sala yake). Nikachukua vazi lake la juu na kuizungusha shingoni na kumkamata na kusema “Nani aliyekufundisha Sura niliyokusikia ukiisoma? Akajibu “Mtume wa Allah ndiye aliyenifundisha”! Nikamwambia ‘Umedanganya” ‘Kwa sababu Mtume wa Allah amenifundisha kwa namna tofauti ya nilivyosikia ukisoma’. Basi, Nikamburuta hadi kwa Mtume wa Allah na kusema (Kwa Mtume wa Allah) ‘Nimemkuta huyu akisoma Surat al-Furqan kwa namna abayo haujanifundisha. Hapo Mtume wa Allah akasema (Ewe Umar) Muachie, Ewe Hisham soma! Kisha akasoma kwa namna ile ile niliyomsikia akisoma! Kisha Mtume wa Allah akasema, ‘Ilifunuliwa kwa namna hii’ Akaongeza Soma Ewe Umar, ‘nikasoma kama ailivyonifundisha! Kisha Mtume wa Allah akasema ‘ilifunuliwa namna hiyo’. Qur’an hii ilifunuliwa kusomwa kwa namna saba tofauti, hivyo isome kwa namna (njia) ambayo ni rahisi kwako (Soma kwa kadiri ambavyo inaweza kuwa rahisi kwako) (Sahih Bukhari)

Njia hizo zilikuwa tofauti hadi Umaer alitaka kumshambulia Hisham kwa sababu alichokuwa anakisoma haikutambuliwa kulinganisha na Qur’an aliyojifunza.

Bhukari anasema kwamba Muhammad alithibitisha baadaye juu ya tofauti saba kama anavyoeleza jinsi ambayo Malaika Gabreil alimfundisha kila moja wapo.

Hivyo kuna wakati mmoja, ambapo hasa kulikuwa na zaidi ya toleo moja iliyothibitishwa na Muhammad. Hata hivyo, wakati wa utawala wa Khalifa Uthman (Mrithi wa tatu wa Muhammad), tofauti za usomaji zilisababisha matatizo kiasi kwamba aliagiza kila toleo ya Qur’an iliyoandikwa au sehemu zake zikusanywe; Akathibitisha toleo inayokaribiana na lahaja inayokaribiana na kabila ya Muhammad, Wakuresh, akaagiza zingine zote zichomwe. Nakala zikatolewa ya toleo moja na kutawanywa kote katika jamii za Kiislamu. Hivyo kwa ubora ni kusema toleo moja kati ya saba imebaki.

Lakini leo japo kumekuwa na toleo moja imebaki tangu wakati wa Uthman- Bado tuna tofauti ya matoleo tofauti. Waislamu wanaambiwa kwamba hizi tofauti ni katika mitindo ya usomaji tu, na bado katika mazingira megine tofauti ya lahaja zinaongeza au kuacha maneno au kubadilisha inayomaanisha kinyume kabisa kila moja.

Kwa mfano,kuna namna mbili tofauti ya kusoma Qur’an 19:19. Katika sehemu zingine, hii aya inasema:

قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَب لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا

“Akasema: mimi mjumbe kutoka kwa Mola wako Kukupa (Kiarabu: li-’ahaba) (habari) za mwana aliyetakasika.”

Matoleo mengine yamebadilisha neno moja na aya inasema:

قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِيَهَب لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا

“Akasema: mimi mjumbe kutoka kwa Mola wako Atakupa (Kiarabu: li-yahaba) (habari) za mwana aliyetakasika.”

Badiliko hili la neno moja inabadilisha mtoaji kutoka kwa malaika kwenda Allah.

Au katika Qur’an 30:2 tuna neno غُلِبَت ghulibati,” inayomaanisha “Wameshindwa” katika usomaji mwingine imeandikwa غَلَبَتِ “ghalabati” inayomaanisha “wamekuwa washindi”! Yaani kubadilisha irabu tu inabadilisha maana kabisa.

Mfano mwingine ni Qur’an 40:20. Baadhi ya usomaji vina “AW An” (Ikimaanisha: AU ile), ambapo usomaji mwingine vina “WA An” (Ikimaanisha: NA ile).

Kuna mifano mingi sana kama hiyo. Kwa mjadala kamili kuhu hili Angalia Maandishi ya Keith Small Textual Criticism and Qur’an Manuscripts.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:17 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)