Grace and TruthThis website is under construction ! |
|
Home Afrikaans |
Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 101 (Don't confuse culture with religion)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?
Previous Chapter -- Next Chapter 17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA SITA: FAHAMU WAONGOFU KUTOKA UISLAMU
SURA YA KUMI NA TANO: USHAURI KWA KANISA
15.10. Usichanganye mila na diniMwongofu kimsingi amepoteza mahusihano yote na maisha yake ya nyuma, hata - ikitokea kama inavyotokea mara chache sana akaendelea kuwasiliana na familia na marafiki zake, au kubaki na kazi zao au nyumba zao. Vyovyote vile, namna yao ya maisha mapya yana machache sana yanayofanana na maisha ya zamani. Kama ilivyoonyeshwa juu, hii inaweza kupelekea huzuni na kujisikia kupoteza. Lakini si kila kitu kinatakiwa kuachwa nyuma. Wamisionari wa Magharibi wa zamani walikuwa na tabia ya kuchanganya mila na dini, mara nyingi walidai kwa waongofu wapya wafate tabia na mazoea ya Magharibi ambayo hayahusihani kabisa na dini na imani ya Yesu. Wakati tunatakiwa kuwa waangalifu sana kutokuruhusu kupunguza imani, lakini pia tunatakiwa kujilinda sana tusije tukahimiza mabadiliko yasiyo ya lazima. Lazima tuwafunze waongofu wapya na kuwatia moyo wakue na kukomaa kiroho, lakini hili lazima lifanyike huku tukikubali tofauti za mila zetu. Sio kila walichokiishi kilikuwa ni dini kwa asili (Hata kama ilivyo katika maisha yetu pia). Lazima tutofautishe tabia za Biblia na matendo ya mila. |