Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 102 (CONCLUSION (Understanding the Ummah of Islam))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA SITA: FAHAMU WAONGOFU KUTOKA UISLAMU

MWISHO (Fahamu uma wa Kiislamu)


Uislamu unasisitiza umuhimu wa kundi kuliko mtu binafsi. Qur’an ainasema:

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu.” (Qur’an 2: 143)

Hii inasisitizwa mara kwa mara katika Qur’an na katika mafundisho ya Muhammad yote. Waislamu hivyo wanajitambua kama sehemu ya uma, ambayo kwa kulingana na Qur’an ni jamii ya Kiislamu, au Uma.

“Kwa hakika huu ni Umma wenu na umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, Kwa hiyo niabuduni Mimi.” ( Qur’an 21:29)

Hii inaweza kueleza kwa nini tunamkuta Muislamu Magharibi na ambaye hajawahi kutoka nje ya nchi yake, haongei lugha yoyote na bado anawaongelea Wasilamu wa China au Nigeria kama watu wake.

Hii inaweza kuwa sifa ya kusifiwa kwa uzuri wa umoja na mshikamano lakini ina hasara yake. Bila kujali namna Muislamu anavyowajibika, nyuma ya kila Muislamu Qur’an inasema:

“Nyinyi mmekuwa bora ya umama waliotolewa kwa watu.” (Qur’an 3:110)

Wanajiona kama sehemu ya uma wa Kiislamu kwanza na zaidi (Taifa la Kiislamu). Utambulisho wowote wa taifa ni jambo la pili. Ndio maana katika miaka ya hivi karibuni tumeona mamia ya Waislamu waliozaliwa Magharibi na wakati mwingine watu wa Magharibi waliosilimu, Wakisafiri umbali mrefu na kujiunga na makundi ya Kiislamu kupigana dhidi ya nchi yao wenyewe ya kuzaliwa. Kwa Muislamu yoyote uzalendo wake wa kwanza ni katika Uma na kama kuna chochote anachoona kati ya uma na na nchi yake, basi uzalendo wake kwanza utaenda kwa uma. Na katika utambulisho wa kila kikundi, uhuru binafsi ulishatupwa nje, kila anachofanya mtu lazima kipimwe kupitia lenzi ya kikundi na masilahi ya kikundi ndio yanachukua ukuu, na lazima aendeleze agenda ya Kikundi. Hii ndio maana utakuta katika nchi zenye Waislamu wengi au vikundi vya Kiislamu uhuru wa mtu binafsi umewekewa mipaka mingi. Ni taifa la Kiislamu sio mtu ndiye cha muhimu. Hata mwanzoni mwa Uislamu Qur’an ilichukulia kwa uzito mdogo sana wafuasi wa Muhammad kama watu binafsi. Ingawa Muhammad alikuwa na wafuasi maelfu ya mamia lakini tunakuta jina moja tu ndani ya Qur’an (33:7). Waliobaki wote wanachukuliwa kama kundi au taifa moja. Hivyo tunaposhughulika na waislamu, tunapaswa kuelewa kwamba Waislamu wanaona Uislamu kama chombo kinachopita kila mila, lugha, eneo la jiografia, nchi na kadhalika. Muislamu wa Misri atamuona Muislamu wa Indonesia ambaye wanaishi mabara tofauti, wanaongea lugha tofauti, hawajawahi kuonana ila mahusihano yao ni ya muhimu kuliko Mmisiri mwenzake wa mlango wa pili ambaye sio Muislamu. Dhana hii ni muhimu kiasi kwamba kuna ibara nzima ya mafunzo ya Kiislamu kuhusu jambo hili inayoitwa al-Wala’ wa-l-Bara ( inayomaanisha “uaminifu na kukataa) inayofundisha hili tu.

Tunapaswa hivyo kujua gharama ambayo tunawaomba waislamu kulipa ili kumfuata Yesu. Hawakutani tu uwezekano wa mateso ya nje tu, lakini na hisia za ndani kwamba wanaifanyia familia, mila, ukoo, uhaini kinyume na watu wa karibu na kuhama kabisa wao wenyewe na utambulisho wao, ambayo maisha yao yote wameambiwa hivyo:

“Hakika rafiki na mlinzi wenu ni Allah na mtume wake na walioamini, ambao hushika sala na hutoa zaka zao nao wananyenyekea. Na takayefanya urafiki Na Allah Na Mtume wake Na walioamini, na kwa hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda.” (Qur’an 5:55-56)

Wamekuwa wakiitazama dunia yote kupitia lenzi ya Qur’an, na wakichukulia kwamba kuanzisha ukaribu na mtu asiyekuwa Muislamu ni dhambi. Qur’an inasema:

“Enyi mlioamini msiwafanye Wayahudi Na Wakristo kuwa Ni marafiki zenu, wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, huyo ni katika wao na hakika Allah hawaongoi wenye kudhulumu.” (Qur’an 5:51)

Kwa Muislamu wa zamani, kisha akachukua nafasi ya kumfuata Yesu, ni ngumu kuliko tunavyoweza kufikiria. Habari njema ni kwamba maisha pamoja na Yesu katika dunia hii na ulimwengu ujao una thamani kuu kuliko gharama binafsi. Yeye ni njia ya wokovu, faida kubwa tuliyo nayo, atupaye amani ya nje na ya ndani na pekee awezaye kutoa suluhisho ya matatizo ya mtu, kwa kutaja, namna ya kuwa sawa na Mungu. Haijalishi ni ngumu kiasi gani, itakuwa rahisi maana kuteseka kwetu ni kazi ya Mungu (Wafilipi 1:29). Sio kwamba sio kazi yetu tu, kama ilivyoelezwa mwanzoni mwa kitabu hiki, lakini upendeleo wetu ni kutumiwa na Bwana kuwafikia watu kwa ajili yake.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 03:15 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)