Previous Chapter -- Next Chapter
9.6. Ukosefu wa Kujiamini
Katika nchi nyingi leo, Wakristo wanaoiamini Biblia ni wachache sana. Katika nchi nyingi za Kiislamu, Wakristo ni chini ya 10% ya idadi ya watu. Katika mzingira mengine idadi ya Wakristo haivuki hata 1000 (Kama vile Somalia, ambapo Waamini wa Kikrsto wanatengeneza idadi ndogo sana ya 0.01% ya idadi ya watu).
Hii inafanana sana na mazingira yaliyoelezwa katika kitabu cha Hesabu:
Wakristo wanajiona namna hiyo leo, Wanashughulika sana madhaifu yao wenyewe, wakisifu dhahiri nguvu za wengine. Wanachosahau ni sehemu ya kwanza ya amri kuu ya utume “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo 28:18). Kinachohitajika leo ni ufanisi wa wachache, wale ambao wanatenda kama chumvi au nuru; bila kujali uchache wa kilichopo, itabadilisha kila kitu.