Previous Chapter -- Next Chapter
9.9. Ukosefu wa kuamini katika kazi ya Kristo
Mara nyingi Wakristo wanaweza kusikia kuhusu mtu fulani kuongokea kuingia Uislamu. Hii inasherekewa sana na Waislamu na saa zingine vyombo vya habari vya kawaida, lakini mara chache sana tunasikia Muislamu kuongoka na kuwa Mkristo. Waislamu wanaongoka kuingia kwenye Ukristo wanakuwa kimya, ama kwa sababu ya hatari ya tishio dhidi ya maisha yao kwa ajili ya kuongoka kwao, au kwa sababu wakati mwingine hawaaminiwi. Hii inachangiwa na dhana kwamba haiwezekani kabisa kwa Muislamu kuwa Mkristo. Hii inatuonyesha wazi kwamba kuna ukosefu wa imani, na dhana inayosema kwamba hii ni ngumu sana kwa Mungu, Licha ya Biblia kujaa matukio na rejea ya watu hatari na waliofanya mambo maovu na bado waliokolewa na Mungu katika Huruma yake ( Hatukuwa wote sawa mbali na Mungu kabla hatujaamini?).