Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 005 (Christians)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU MWANZO WA UISLAMU
SURA YA KWANZA: DINI KABLA YA UISLAMU

1.3. Wakristo


Ukristo pia ulishafika katika Ghuba ya Uarabuni wakati wa karne ya 2 na ya 3 baada ya kusulubiwa kwa Kristo.Kwa kweli, Kulikuwa na uwepo wa Waarabu Yerusalemu siku ya Pentekoste (Matendo 2:11), inawezekana kwamba walichukua Injili hadi kaskazini mwa Uarabuni, ijapokuwa ilichukuwa mda mrefu kwa Ukristo kuenea zaidi Kusini. Kwa hakika hadi wakati wa Muhammad anazaliwa, kulikuwa na jamii tofauti za Kikirsto ambao walitofauatiana mambo ya msingi ya imani na walikuwa wametawanyika katika Ghuba ya Uarabuni. Wengine walikuwa ni Waarabu wa Kiasili ambao wengine walikuwa na hadhi ya juu katika jamii.( Kama vile wafanyabiashara matajiri katika Najran hadi kusini), Lakini Wakristo wengi waliokuwa katika mji wa Maka sehemu alipozaliwa Muhammad na pembeaoni walikuwa watumwa waliokimbia kutoka majimbo ya himaya ya Rumi, au waliotekwa na wavamizi wa Kiarabu Kaskazini (Wahajemi, Watu wa Yordan, Warumi na Wayunani), zaidi ya hayo idadi ndogo ya waongofu wa Waarabu. Vile vile ulienea katika eneo kupitia jumuia za makundi ya Kikristo na waamini binafsi hivyo Waarabu walikuwa na angalaau uelewa wa imani yao. Ilikuwa ikifahamika, basi, kwamba kama vile Wayahudi walivyokuwa kwa shauku kwa ujio wa Kwanza wa Masihi, Wakristo nao walikuwa wanangojea kurudi kwa Yesu ili awachukue mbinguni. Hata hivyo, umbali wa tofauti wa imani yao ilkuwa pana kweli zikijuimuisha manyunyizo mengi ya uzushi; Tutajadilia athari ya uzushi huu katika mafundisho ya Muhammad katika sura ya ya baadaye. Kwa sasa inatosha kusema kwamba walikuwa na ushahiwishi wa maana kabla ya nadharia za dini ya Kiislamu kwenye jamii ya Kiarabu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 03, 2024, at 06:03 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)