Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 004 (Jews)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU MWANZO WA UISLAMU
SURA YA KWANZA: DINI KABLA YA UISLAMU

1.2. Wayahudi


Tofauti na leo, Uarabuni katika nyakati za Muhammad ilikuwa na idadi kubwa ya Wayahudi na wenye uimara wa kimaisha na kwa kweli baadhi ya miji ( Kama vileYathrib –eneo inayoitwa Madina leo- kulikuwa makabila tawala kadhaa za Kiyahudi). Hili ilisababishwa na mawimbi kadhaa la uhamiaji kwa karne kwa karne nyingi; Kila mara kulipotokea mtikisiko na mateso Judea na Samaria,Wayahudi wengi zaidi walitoroka kwenda Ghuba ya Uarabuni hadi kusini. Hivyo hadi kufikia karine ya 7 BK , jamii za Kiyahudi waliweka makazi ya kudumu katika eneo hili lote. Walichangayika na kufanya biashara pamoja na makabila ya Waarabu,Lakini kwa kutunza desturi zao na za wenyeji wa eneo ambao kwa nadra walioana nao wakiwa namakazi ya kudumu huku wakiheshimika sana, hawakujiingiza katika mila za Waarabu.

Inaonekana iliaminika kwa ujumla kwamba Wayahudi kufika Uarabuni ni kwa sababu walishiriki ukoo mmoja wa zamani nawenyeji walioishi hapo kupitia watoto wa Ibrahimu, Isaka na Ishmael. Wakati ambapo hakuna ushaihi wa kweli na kamili kwa Waarabu walikuwa Kizazi cha Ishmael, Maelezo ya Kitabu cha Mwanzo ya safari ya Ishmael kusini mwa Jangwa la paran- Karibu na Kasikazini mwa Ghuba ya Uarabuni-ilisababisha dhana ya kwamba Waarabu katika Ghuba ya Uarabuni walikuwa ni uzao wake. Wakati Wahamaji wa Kiyahudi waliokuwa wanafika upya hawakuwa na nia hasa ya kuwa na mahusiano na Waarabu kwa msingi wa kudhaniwa kwamba wao ni jamaa, ilikuwa ni kwa masilahi yao kutanganza dhana hii maana inengeweza kuwafanya wamudu kiwango Fulani ya ulinzi kulingana mazingira ya heshima kutoka kwa wenyeji. Matokeo yake, hadi nyakati za kuzaliwa kwa Muhammad dhana ya undugu baina ya Waarabu na Wayahudi ilichukuwa kwa kawaida karibia na kila mtu.

Tokeo mojawapo ilikuwa ni Jamii nyingi kubwa zinazojitegemea za Wayahudi ambayo iliota mzizi kwa miaka mingi na kujenga mpangilio tofauti wa imani, ambapo mambo mengi waliyoyaamini yalikuwa kinyume kwa umuhimu wake na uhalisia wa Agano la Kale.Lingine ilikuwa ni ukweli Kwamba Waarabu wa nyakati hizi walikuwa na muingiliano wa mahusiano na jamii za Wayahudi, na hivyo angalau wangekuwa na uelewa juu imani zao. Wayahudi waliokuwa wanaishi Uarabuni walikuwa wakimngoja ujio wa Masihi, Mfalme alitabirikiwa katika Agano la Kale, Yule ambaye angewakomboa kutoka kwenye ukandamizaji na kuwarejesha katika nchi ya ahadi. Masimulizi yao juu ya ujio wa Masihi yalienea miongoni mwa jamii ya Waarabu, na wenyeji pia walianza kutarajia ujio wa Masihi au nabii ambayo ilifungua njia wa kukubalika kwa Muhammad na ujumbe wake wa imani ya Mungu mmoja.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 03, 2024, at 05:58 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)