Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 006 (Hanifs (Hunafā'))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU MWANZO WA UISLAMU
SURA YA KWANZA: DINI KABLA YA UISLAMU

1.4. Hanifa (Hunafa’)


Kuna pia ushahidi wa dini iliyoamini katika Mungu mmoja, Inawezakana wali- athiriwa na Wayahudi na wa Wakristo wenyeji, japo hatuwezi kusema hivyo kwa uhakika. Wale waliofuata dini hiyo walijulikana kama Hanifa (au Kwa kiarabu, Hunafa’); hawakuunda jamii moja ya waaminio ya waabudu au kushika fundisho maalumu iliyoagizwa, lakini badala yake ilikuwa ni jina kama kifuniko cha utambulisho kwa watu wasiofanana lakini wanaamini imani inyoendana sawa.

Mmoja wa mshairi maarufu alkuwa Umaiya ibn Abi-Salt. Umaiya alikuwa akisema kwamba kila dini itakataliwa na Allah siku ya mwisho, isipokuwa dini ya Hanifa. Vyanzo vya Uislamu vinasema Umaiya alidai kwamba yeye ni Mtume mda kidogo kabla Muhammad hajatangaza utume wake; simulizi zinazohadhithiwa juu yake zinafanana sana na zile zinazosimuliwa na Waislamu kuhusu Muhammad, Kama vilemalaika kupasua moyo wake ili kuutakasa, na uwezo wake wa kuongea na wanyama. Muhammad alikuwa na uelewa kuhusu Umaiya na maandishi yakeinawezekana yalia-thiriwa naye; aya ya Qur’an “Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye kukhasiri” (Qur’an 3:85) inafanana sana nukuu ya Umaiya mwanzoni mwa ayah ii.Inasemekana Umaiya alikutana na Muhammad na kukataa ujumbe wake, Iliyomchochoea Muhammad kusema “Mashairi yake yanaamini,lakini moyo wake hauamini”

Mwingine alikuwa ni mhubiri aliyeitwa Quss bin Saida, ambaye Kipaji chake cha kuzungumza iliwavutia miongoni mwa jamii za Kiaarabu kabla ya ujio wa Uislamu. Quss alikufa kabla ya MUhaamd kutangaza utume wake. Lakini Muhammad alikuwa na uzoefu na mafundisho yake. Tunajifunza zaidi juu ya athari ya ushawishi wa Quss juu ya Muhammad kutoka wana historia Ibn Hisham na Ibn Kathir. Ibn Hisham anasimulia mazungumzo kati ya Muhammd (Wakati huu alishajitangazia utume) na wafuasi wake ikimjuisha mshairi aliyetwa Jarud:

"Muhammad aliuliza ‘Kuna yoyote anayemjua Quss bin Saida?’ Jarud akajibu ‘bila shaka’ Ewe Mtume wa Allah: Wote tunamjua. Mimi namjua zaidi kwa sababu kila mara nafuata njia yake. Hapo, Mtume wetu Mtukufu (SAW) akajibu: Hutuba aliyoisoma Quss bin Saida juu ya ngamia wakati wa Suq Uqaz ambako alisema “Mwenye kuishi atakuja kufa, na Mwenye kufa atahisi majuto makubwa. Vyovyote livyomaanishwa kutukia, itatokea” haijawahi kuondoka akilini mwangu. Alisoma maneno mengine mageni na kwa ufasaha wa ajabu ambayo najikuta siyakumbuki” (Ibn Hisham, Sirah).

Ibn Kathir, anaendelea kusimulia:

“Wakati Muhammad aliposikia hutuba ya Quss ambayo dani anasema” Yu wapi anayeonea na kudhulumu watu,anayekusanya pesa na kuzitandaza juu, akisema “ Mimi bwana wenu Mkuu?” Hawakuwa matajiri kuliko nyinyi, waliishi mda mrefu kuliko nyinyi? Ardhi yenye unyevunyevu imewazika chini bila huruma na kuwararua mbali kwa dharau. Tazama! Mifupa yao inaoza. Nyumba zao zimeharibiwa, zikikaliwa na mbwa mwitu wabwekao,’ Muhammad akasema ‘Allah na arehemu roho yake; Quss alikuwa ni mtume kati kati yangu na Yesu” (Tarjamat ya Quss bin Sai’da katika al-Bidaya wal- Nihaya na Ibn kathir)

Wengine wenu ambao mna uzoefu na uelewa wa Qur’an mnaweza kutambua kufanana kwa hutuba ya Quss na shemu za Qur’an, Vyote kwa namna ya muundo wa sauti yake laini laini, na maneno halisi. Kwa hakika tunaweza kusema kwamba Quss alikuwa na ushahiwishi wenye athari katika muendelezo wa ujumbe wa Muhammad.

Wa Hanifa wengine walikuwa na imani zisizopishana na Uislamu. Mfano wa mmoja wapo, na mtu aliyeitwa Zayd Ibn Amr, alikuwa akiionya na kuikanya dini ya Quraysh (Kabila la Muhammad): “Enyi wa Quraysh hakuna miongoni mwenu anayefuata dini ya Ibrahimu ila mimi.” Zayd alirekebisha lishe yake, alikuwa hali nyamafu, damu, kilichochinjwa ili kitolewe sadaka kwa sanamu, alipinga mauaji ya watoto wachanga kama kafara kitu ambacho ilikuwa ni mazoea katika jamii kubwa ya Waarabu, na aliandika mashairi mengi, akikana kuabudu sanamu na kuhubiri imani yake kama vile:

“Je mimi nimuabudu bwana mmoja au maelfu?
Kama wapo wengi kama mnavyodai,
Ninamkataa al-Lat na al-Uzza, wote,
kama ambavyo yoyote mwenye akili timamu angefanya.
Sitamuabudu al-Uzza na binti zake …
Sitamubudu, japokuwa alikuwa ni bwana wetu
katika siku ambazo nilikuwa na akili kidogo”

Wana Hanifa wengine walikuwa na mamlaka ya Kisheria, kama vile Aktham bin Saif ambaye alizingatiwa kama kama mmoja wa watalawa wenye hekima sana Uarabuni kabla ya Uislamu. Hukumu zake nyingi sana ziliigwa na kupitishwa na Muhammad. Imesimuliwa kwamba wakati Aktham alipoona watoto wa Abd al- Muttalib ( babu yake Muhammad), alisema “ Kama Allah akitaka kuanzisha himaya ya utawala, hao ndio watu atakaowachagua, hao ni mbegu ya Allah sio mbegu za wanadamu”

Waislamu wanazingatia kwamba Wa Hanifa, kwa kule kukataa ibada za sanamu iliyokuwa imezoeleka sana miongoni mwa jamii za Kiarabu, Ndio wale waliotunza usafi wa imani ya Mungu mmoja ya Ibrahim. Kabla ya Uislamu, kama tulivyoona, ilikuwa ni nadra sana kuwataja Wayahudi au Wakristo; hata hivyo; Qur’an inajaribu dini hizi mbili zinazoamini katika Mungu mmoja kwa pamoja, ikitumia jina hilo kwa Wakristo na Wayahudi mara moja (Qur’an 98:5), Waislamu mara moja (Qur’an 22:31), na Ibrahim mara kumi. Imependekezwa kwamba japokuwa hili ni zao la matamanio ya fikra za Muhammad akitaka kuupa uhalali madai yake ya kuwa mtume wa miwsho katika mlolongo wa mitume kuliko maelezo halisi ya kuamini mfumo wa imani moja. ( ambavyo kama tulivyosema hapo awali, haikuwa hivyo).

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 03, 2024, at 06:13 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)