Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 021 (PILLAR 1: The Shahada (Islamic creed))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA NNE: NGUZO ZA UISLAMU

4.1. NGUZO 1: Shahada (Ukiri wa Kiislamu)


Shahada, au kauli mbiu ya imani, inasema kwamba “hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni mtume wake.” Kumbuka umakini uko kwa wote Allah na Muhammad, Inashangaza sana kwa dini inayodai kuamini kabisa katika Mungu mmoja kwamba sehemu ya kwanza ambayo inamtaja Allah pekee yake haitoshi, na sehemu ya pili lazima imujumuishe Muhammad (Kiumbe). Hii bila shaka inaongeza mshangao zaidi katika macho ya Muislamu wanaosisitiza kwamba Muhammad sio wa kipekee na maalumu miongoni mwa manabii wengine, na bado amepewa upekee na kujumuishwa katika kauli mbiu ya msingi kabisa ya imani.

Waislamu wanaamini Shahada lazima iweze kutamkwa katika lugha ya Kiarabu, hata kama hakuna chochote katika mafundisho ya Kiislamu inayosema lazima iwe hivi. Kwa mujibu wa Muhammad, Kwa kuitamka tu inatosha kumuokoa Muislamu kutoka kuzimu. Alisema:

“Hakuna yoyote ashuhudiaye kwa kumaanisha kutoka moyoni kwamba La illaha illa- Llah wa anna Muhammad Rasul Allah (hakuna apaswaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na Muhammad ni mtume wa Allah), Isipokuwa kwamba Allah atamuokoa kutoka katika moto wa Kuzimu.” (Sahih Bukhari)

Na hivyo basi hii ndio jambo pekee inayohitajika kwa mtu kufanyika kuwa Muislamu.

Waislamu wanasikia ukiri huu zaidi ya mara ishirini kila siku wakati wa adhana, na kila Muislamu binafsi huirudia mara nyingi kila wakati wa sala. Kiuhalisia, inatamkwa mara nyingi kuliko idadi hii maana baadhi ya Waislamu wanatumia ukiri huu kuonyesha hasira, kufadhaika, shukrani, na kadhalika.

Muhammad alisema:

“Nimeamurishwa kufanya vita na watu mpaka waseme: ‘La ilaha illa- llah’ (hakuna apaswaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah). Na kama wakisema hivyo, wasali kama tunavyosali, waelekee Kibla (ka’bah, Maka wakati wa kuswali) na wachinje kama tunavyochinja, ndio damu zao na mali yao vitakuwa vitakatifu kwetu, na hatutaingilia mambo yao isipokuwa ilivyo halali na hesabu yao itakuwa kwa Allah.” (Sahih Bukhari).

Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaelewa neno “watu” kumaanisha kabla ya Muhammad, Wakati wengine wanaelewa neno hilo kumaanisha kila Muislamu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 05:49 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)