Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 022 (PILLAR 2: Salat (prayer))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA NNE: NGUZO ZA UISLAMU

4.2. NGUZO 2: Salat (sala)


Sala katika Uislamu sio kama vile tunavyofikria sala katika Ukristo. Katika Uislamu, sala ni mpangilio wa vitendo vilivyoelekezwa rasmi, ni muenendo, maneno, yanayoambatana na uhuru mdogo sana wa namna inavyotakiwa kufanywa. Kuna kanuni nyingi zinatakiwa kufatwa kabla na baada ya sala, saa inayotakiwa sala kufanyika kwa siku, na pia mda ambao sala hairuhusiwi kufanyika (kwa mfano Waislamu hawaruhusiwi kusali wakati wa mawio na machweo ya jua). Kanuni za msingi zimetolewa ndani ya Qur’an au Suna za mtume (Sunnah); ingawa, mahali ambapo kunakosekana taarifa kwa undani na kwa uhalisia wa kipi kifanyike, Waislamu wanafuata tafsiri maalumu ya mmojawapo ya tafsiri sahihi za fikra nne za maimamu wakuu wanne ambayo iliasisiwa miaka 300 baada kifo cha Muhammad.

Kabla ya kusali, Waislamu wanatawadha, wakiosha mikono yao, uso, kichwa, na miguu.Tendo hili la kutawadha linaitwa wuudhu. Kama hakuna maji safi, wanaweza kufuata namna hiyo hiyo ya kutawadha kwa kutumia vumbi au mchanga. Kutawadha kunaelezwa ndani ya Qur’an, lakini haifafanuliwi kwa undani wa kila kitu, hivyo basi kuna tafsiri tofauti ya jinsi inavyotakiwa kufanyika.Kwa kweli, sio kwamba tafsiri nne za fikra za wanazuoni wakuu wanne wa Sunni zinatofautiana ni namna gani kutawadha kuwe, lakini waliofuata mawazo yao pia wanatofautiana katika tafsiri zao na hivyo imesababisha kuwepo kwa njia nyingi za kutawadha.

Kwa jumla yake inakubalika, Kwa mujibu wa kumbukumbu ya matendo ya Muhammad, Kutawadha kwa mara moja inaweza kudumu hadi sala inayofuata, hasa hata kwa sala kadhaa zinazofuata.Isipokuwa akitoa upepo (akijamba), akienda haja (chooni), au akipata jereha ambapo itatakiwa kutawadha tena. Baadhi ya Wanazuoni wa Kiislamu pia wanasema kwamba kula au kunywa chochote kisichokuwa maji pia inaondoa udhu,na hivyo Muislamu atatakiwa kutawadha tena wakila au kunywa kati ya sala moja na nyingine. Endapo watajamiana (Kufanya tendo la ndoa), udhu hautoshi kabla ya sala bali Waislamu wanatakiwa kujitakasa kwa kuoga mwili mzima kabla hajasali.

Baada ya kutawadha- inategemea tafsiri ya madhehebu gani wanafuata-wanasali kuelekea Maka. Mara wanapoanza, hawaruhusiwi kuzungumza au kuangalia pembeni, na wakifanya basi inatangua sala na wanatakiwa kuanza upya. Kama udhu umetanguliwa, basi wanatakiwa kutawadha upya kabla hawajarudia sala hiyo.

Kuna sala tano zilizoelezwa za faradhi za kila siku (alfajiri, adhuhuri, alasiri, magharibi, na insha), Zinaweza kusaliwa na mtu akiwa peke yake au wakiwa katika kundi, na zinaweza kusaliwa popote (sio lazima iwe msikitini au chumba kilichotengwa kwa sala tu) ilimradi waelekee Maka. Zinajumuisha vitendo vilivyokaririshwa, utamkaji wa maneno ya kurudiwa rudiwa, wakiongeza na kusoma sehemu ya Qur’an (ndefu au fupi) wanayochagua wao.

Kwa kuongezea, kuna aina nyingine za sala katika Uislamu kama vile “siku ya kukusanyika” (Ijumaa), Siku kuu za Kiislamu au Eid (mbili kwa mwaka), mazishi,kiangazi (kuombea mvua),kupatwa kwa jua na mwezi, vita, hofu, na kadhalika, Tena, kuna maneno na matendo yaliyoamuriwa kwa ajili ya kila moja wapo ya sala hizi. Kwa mfano, sala ya mazishi haina kusujudu. Wakati kwa sala ya Ijumaa, ina mahitaji ya ziada; lazima ifanyike na kundi la watu angalau wasiopungua 15- au 40 kwa mujibu wa baadhi wa wanazuoni wa sharia- inafanyika mda wa adhuhuri ya siku ya Ijumaa tu. Lazima ijumuishe hutuba.Katika baadhi ya nchi za Kiislamu, hutuba hizi zinaunganishwa kuwa moja, na lazima iandikwe kabla (kuthibitishwa), kwa kawaida na wizara ya mambo ya dini au taaisisi ya kidini katika nchi husika, ingawa jambo hili limejitokeza kwa siku za karibuni katika jitihada za kujaribu kuzuia ufurutu ada (Imani kali au ugaidi).

Kwa wanawake walio huru, mavazi wakati wa sala lazima yafunike miili yao yote ikijumuisha kichwa wakati wa sala, lakini wanaweza kuacha wazi nyuso zao na mikono. Wanaume (wote watumwa na walio huru) na wanawake wanaweza kuvaa mavazi yanayovuka kwa kufunika magoti. Ndio kusema, Uhalisia unatofautiana miongoni mwa Waislamu namna wanavyotafsiri na kimaelezo; japo kinadharia hakuna shida kwa Muislamu mwanamme kusali akiwa kifua wazi ilmradi tu amefunika eneo la kitovu hadi kuvuka eneo la magoti, hii itakuwa ni kashfa kwa uma wa Kiislamu wa leo! Na ukweli kwamba Waislamu wa kike watumwa wanaweza na inakubalika kusali bila nguo ya juu ni ukweli usiofahamika karibia na Waislamu wote, hata na wasomi waliobobea, na tuone mfano mwingine: Katika Uislamu sio tu inaruhusiwa kusali huku umevaa viatu, Lakini hasa iliagizwa na Muhammad aliyesema:

“Kuweni tofauti na Wayahudi, salini mkiwa mmevaa makobazi au viatu.” (Sunan Abi Dawud)

Hata hivyo leo ulimwengu mzima haikubaliki kwa Waislamu kusali huku wamevaa viatu na wakati wote wanavua viatu kabla ya kusali.

Yote haya yanafanya sala ya Kikristo kuwa jambo isiyoeleweka kwa Waislamu. Wazo kwamba tunaweza kutumia maneno yetu wenyewe, kusali mahali popote, kuimba nyimbo wakati wa ibada- haya yote yanaonekana kuwa mambo mageni kwa Wasilamu. Tutafanya vizuri sana kukumbuka hili kwa sababu Waislamu hawataelewa tunachomaanisha pale tunaposema tusali!Tunaweza kudhani eti kwa sababu tunatumia maneno yale yale , basi tunamaanisha kitu kimoja kumbe kwa uhalisia tunaongelea kitu kinachotofautiana na ngeni kwa Muislamu ambaye hawezi kuwa na mawasiliano binafsi na Allah katika kile tunachokiita sala.

Ingawa sio mojawapo katika nguzo za Uislamu, kuna aina ya sala inayoitwa D’ua ambayo haina maelezo ya kivitendo namna ya kuifanya na inaweza kufanywa na mtu binafsi. Hii inaweza onekana kufanana na dhana ya sala katika Ukristo, lakini bado sio jambo binafsi na kwa upeo wa jumla inatofautiana sana na mawasiliano binafsi na Mungu katika sala kama tunavyoelewa inatakiwa kuwa.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 05:58 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)