Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 039 (Christ Created)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TATU: FAHAMU KRISTO MUISLAMU
SURA YA SABA: MIUJIZA YA KRISTO NDANI YA QUR’AN

7.1. Kristo aliumba


Kristo anasema katika Qur’an:

“Ya kwamba nakuumbieni kutoka udongo kama sura ya ndege;kisha nampuliza anakuwa ndege, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu” (Qur’an 3:49)

Hivyo Qur’an inamwelezea Kristo kama muumbaji; inashangaza kwamba Qur’an inasema Kristo aliumba kwa kutumia udongo bidhaa hiyo hiyo ndiyo aliyotumua Allah kumuumba Adam katika Qur’ an:

“Na amemuumba mtu kwa udongo wa mfinyanzi” (Qur’an 55:14)

Mtazamo kwamba Kristo anafanya hivyo “kwa idhini ya Mungu” inafanana sana na kile alichokisema Kristo kwenye Agano jibya:

“Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, Amin nawambia, Mwana hawezi kutenda mwenyewe ila lile ambalo amwona baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, ndio ayatendayo mwana. Kwa kuwa baba ampenda Mwana, na humuonyesha yote ayatendayo mwenyewe, hata kazi kubwa kuliko hizo. Maana kama awafufuavyo wafu na kuwahuisha, hivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao” ( Yohana 5:19-21)

Tofauti ni kwamba wakati Injili inabainisha umoja wa Utatu na kwamba Kristo alikuja kufanya mapenzi ya baba, Qur’an haifafanui muujiza huo bali inataja muujiza huo wa kuumba katika orodha ya vitu alivyofanya Kristo. Kusema kwamba aliyafanya kwa idhini ya Mungu havihusihani na haviwezi kuthibitisha kwamba Kristo asingeweza kuwa Mungu isipokuwa anakuwa mtu wa kawaida tofauti, Kwa Wakristo hawawezi kusema kwamba mapenzi ya Kristo ni tofauti na mapenzi ya baba- Kiukweli mapenzi yao lazima yawe mamoja tu!

Hivyo tunabakiwa na ukweli huu: Zaidi ukiacha Allah, hakuna yoyote mwingine aliyepewa sifa ya kuwa muumbaji zaidi ya Kristo ndani ya Qur’an.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 08:03 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)