Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 040 (Christ Spoke in Infancy)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TATU: FAHAMU KRISTO MUISLAMU
SURA YA SABA: MIUJIZA YA KRISTO NDANI YA QUR’AN

7.2. Kristo aliongea katika uchanga wake


Hii ni miongoni mwa miujiza ya kushangaza ndani ya Qur’an. Qur’an inasema kwamba wakati Mariamu aliporudi kwa watu wake huku amembeba mtoto, walimshutumu kwa uzinzi, wakisema:

“Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu” Ewe dada yake Haruni! Baba yako hakuwa mtu mwovu, wala mama yako hakuwa kahaba.”

Badala kujibu mwenyewe, alimruhusu mwanawe ajibu kwa niaba yake:

“Akawashiria mtoto. Wakasema, Vipi tuongee na mtoto aliye bado mdogo na yupo katika malezi? (Yesu) akasema: hakika mimi ni mtumwa wa Allah, amenipa kitabu na amenifanya nabii. Na amenijalia mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na amenihusia sala na zaka maadamu ni hai. Nimtendee wema mama yangu na wala hakunifanya niwe jeuri na mwovu. Na amani ipo juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakapofufuliwa kuwa hai” (Qur’an 19: 27- 33)

Hii inashangaza kwa sababu kadhaa.

– Hakuna sababu ya maana kwa muujiza huu katika Uislamu, maana miujiza katika Uislamu ni uthibitisho wa utume. Kristo alifanya mengi na zaidi kwa mbali miujiza mingi akiwa mkubwa, hivyo hii haikuwa jambo muhimu la kuthibitisha utume wake. Tunazidi kutambua watoto – mpaka wafikie umri wa utu uzima ( Kwa ujumla inakubalika miaka 15)- hawatakiwi kufanya matakwa ya kidini seuze kuwa mtume.
– Hakuna aliyekuwa na sababu za kumuuliza Maryamu juu ya baba wa mtoto (zaidi ya Yusufu), maana alikuwa kisheria ameshaolewa naye na hivyo ilisadikika kuwa baba yake ni Yusufu. Kwa nini familia yake imtuhumu kwa uzinzi? Katika Agano jipya ni kwa uchache sana inasisitizwa dhana ya ubikira na mimba ya Yesu. Kiukweli watu pekee waliojua juu ya hilo ni mariamu, Yusufu, Zakaria, Elizabeth na Luka. Ubikira na kuzaliwa ilikuwa lazima ya namna Yesu alikuwa nani na haikuwa chanzo cha kuzaliwa kwake na hivyo ubikira haukuwa uthibitisho wa uungu wake.
– Mjadala huu unazua maswali mengi kuliko majibu. Je Allah alitoa maandiko kwa mtoto Yesu, hivyo kinyume na dhana ya uwajibikaji unaoshikiliwa na Uislamu, ikijumuisha msingi wa hakuna anayepaswa kuwa nabii hadi afikie miaka ya utu uzima? Au ilikuwa ikiashiria maisha ya baadaye wakati ambapo Yesu atakuja kuwa nabii? Natumai hii inawezekana lakini haijaonyeshwa na haiko wazi ndani ya Qur’an.
– Kama Yesu aliamuriwa kutoa zakat maadamu wakati wote akiwa hai, je bado anatoa zakat kwa sasa ( Maana Uislamu unafundisha kwamba hajafa na bado yuko hai)? Na aliilipa lini akiwa mtoto?

Habari hii inapatikana katika mojawapo ya vitabu vya Injili visivyo rasmi kikanuni vya Kiapokirifa vilivyoandikwa na wazushi na wanagnostiki Ujuzilio ambavyo havitambuliwi kama vimevuviwa na Mungu. Hivyo ndio kusema huo ndio uliokuwa chanzo cha taarifa hii Qur’an.

Qur’an pia inatuelezea mtoto mwingine muujiza ulifanyika kwake akiwa mchanga bado. Lakini muujiza wa tofauti sana. Muhammad alipokuwa mdogo- Tuliona katika sura ya kwanza- alipata kutembelewa na malaika, akafungua moyo wake, akachukua kitu kidogo cheusi, akausafisha na akafunga kifua chake tena. Tunaambiwa kwamba ilikuwa kwa ajili ya kumtakasa Muhammad. Hata katika Uislamu kuna tofauti baina ya Yule anayefanyiwa muujiza ili kumtakasa na Yule anayetakasa wengine. Hata kama ingawa hakuna ushahidi wa kuthibtisha huu muujiza, lakini inashangza kwamba Uislamu unaonekana kumweka Yesu kwa kumwepekisha na manabii wengine (Ikijumuisha Muhamad).

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 08:06 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)