Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 038 (CHAPTER SEVEN: CHRIST'S MIRACLES IN THE QUR'AN)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TATU: FAHAMU KRISTO MUISLAMU

SURA YA SABA: MIUJIZA YA KRISTO NDANI YA QUR’AN


Ingawa Kristo si nabii pekee katika Uislamu kufanya miujiza, inasitahili kuangazia hadith za Qur’an kuhusu miujiza yake na namna zinavyoongeza ufahamu wetu namna ambavyo Waislamu wanamuona. Baadhi ya miujiza inayohusishwa kwa Kristo ndani ya Qur’an pia ipo katika Injili (Kuponya vipofu, kufufua wafu) lakini mengine haipo; baadhi hata huonekana kama isiyo na maana yoyote, kama kutengeneza ndege kutoka udongo. Hii inawezekana kutokana na Muhammad alitegemea mapokeo ya simulizi za mdomo isiyoandikwa na baadhi ya vyanzo vya taarifa visivyo sahihi. Baadhi ya miujiza hiyo isiyopatikana katika Injili inapatikana katika vitabu vya Kikristo visivyo kanuni yaani Apocrypha na simulizi za maadishi ya nyuma katika karne ya pili hadi ya nne kama vile Injili ya Uchanga ya Thomas, Injili ya Kikoptiki ya Wamisri, Injili ya mazazi ya Mariamu, Historia ya Yusufu seremala na Injili ya uchanga ya Siria, na kadhalika.

Ni kwa namna gani Muhammad alikuja kujua hizi hadith?Ni sawa, tumeshaeleza baadhi ya mawasiliano yake ya awali na Wayhudi na Wakristo ( Wengi wao wenye kuamini uzushi) mawanzoni mwa maisha yake, na ya kwamba miongoni mwa watu waliohusihana naye kwa wakati huo ni Waraqa, binamu yake Khadija aliyekuwa akitafsiri Injili ya Kiebrania (Inayoaminika kuwa Injili ya Waebonia). Watu wa wakati wa Muhammad walimshutumu kwa kujifunza kutoka kwa wengine, na kiuhalisia Qur’an inathibitisha hili kwa kusema:

“Hakika tunajua kwamba wanasema, yuko mtu anayemfundisha, Lugha ya huyo wanayemsema ni ya kigeni, na hii (Qur’an) ni lugha ya Kiarabu bayana” ( Qur’an 16:103).

Zingatia kwamba Qur’an inasema kwamba mtu anayemfundisha Muhammad ni Mgeni, kama inavyoeleza kwamba watu wa Maka walimshutumu kwa kujifunza kutoka mtumwa kutoka Rumi. Pia na wana historia wa Kiislamu wameandika kwamba Wakureshi walijenga upya Al-kaba wakati wa kabla ya Muhammad hajatangaza utume wake, wakamtumia seremala wa Kikoptiki aliyeitwa Bakhum kusaidia katika ujenzi (Encyclopaedia of Islam) hivyo ingekuwa rahisi kwa Muhammad kuweza kusikia hadith zilizosimuliwa na Wayahudi au Wakristo, wasafiri, au watumwa katika miaka ya 40 kabla hajadai utume wake.

Hapa kinachofuata ni mjadala kwa ufupi kuhusu miujiza mikuu inayohusishwa nayo Kristo katika Uislamu. (Ingawa kuna baadhi ya miujiza midogo haijatajwa):

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 12:39 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)