Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 043 (Christ fed the multitude)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TATU: FAHAMU KRISTO MUISLAMU
SURA YA SABA: MIUJIZA YA KRISTO NDANI YA QUR’AN

7.5. Kristo alilisha makutano ya wingi wa watu


Inaonyesha kama jambo la kawaida? Nina uhakika umeshasoma habari ya Yesu kulisha watu elfu tano katika Yohana sura ya 6. Qur’an hasimulii habari hii bali iliyo tofauti.

“Waliposema wanafunzi, Ewe Isa bin Maryamu! Je Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni waumini. Wakasema: Tunataka kukila chakula hicho, na nyoyo zetu zitue, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe miongoni mwa wanao shuhudia, Akasema Isa bin maryamu: Ewe Allah, Mola Mlezi wetu! Tuteremshie chakula kutoka mbinguni, ili kiwe siku kuu kwa ajili ya mwanzo wetu na mwisho wetu, na kiwe ni ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanaoruzuku." (Qur’an 5:112-114)

Nina uhakika unaweza kuona kufanana kwa habari hii na ile ya Biblia, katika maono ya Petro kwenye Matendo 10. Inawezekana kabisa Muhammad alisikia habari mbili tofauti kutoka utoto wake na kuzichanganya. Kwa habari hii ni muhimu na ina maana gani katika Qur’an yenyewe hivyo tunapaswa kwenda kwenye mafafanuzi ili kujua vile Waislamu wenyewe wanavyoamini juu yake. Wanahusisha taarifa mbali mbali kuhusu kuombea meza ya chakula kwa Yesu kutoka kwa Mungu; Nyingi hazikubaliki na wanazuoni lakini zinaaminiwa na Wasilamu wengi wa kawaida. Mfafanuzi mmoja anasimulia namna Yesu alivyowaomba waisrael kufunga kwa siku thelathini. Walipofanya hivyo wakamrudia na kumwambia wanasikia njaa; Wakamuomba Yesu kama anaweza kumuomba Allah kuwatumia chakula kutoka mbinguni. Hivyo Yesu akavaa matambala, akakaa juu ya majivu na kisha kuomba. Malaika wakaja pamoja na meza na juu yake kulikuwa na mikate saba na samaki saba na wakawaleta mbele ya watu na wote wakala na kushiba (Ibn Kathir, Qur’an Commentary juu ya 5:112-115).

Miujiza inafafanua tabia za mitume katika Uislamu, inashangaza kwamba isipokuwa Muhammad, kama Allah alivyosema ndani ya Qur’an kwamba hatafanya muujiza wowote kwa sababu vizazi vilivyopita kabla yake walikataa kuamini miujiza iliyotendwa na na mitume waliotangulia.(Japo Qur’an inachukuliwa kama muujiza na kuna baadhi ya miujiza ambayo inasemekana kutendwa na Muhammad lakini vinatokana na vyanzo visivyoaminika na simulizi za watu kama tulivyoona huko juu). Hakuna mtume mwingine yoyote wa Kiislamu anayesogelea kwa ukaribu wa miujiza aliyofanya Kristo. Hii inampa hadhi ya juu kuliko mitume wengine. Wakati huo huo, hata hivyo baadhi ya miujiza aliyofanya haimpi taswira nzuri. Chukulia kwa mfano kuwageuza watoto wasio na hatiya kuwa nguruwe, inayopingana hata mafundisho ya Kiislamu ya Manabii kutokuwa na dhambi.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 08:15 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)