Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 044 (CHAPTER EIGHT: CHRIST IN ISLAM AS A SERVANT AND MERE HUMAN)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TATU: FAHAMU KRISTO MUISLAMU

SURA YA NANE: KRISTO KATIKA UISLAMU KAMA MTUMWA NA BINADAMU WA KAWAIDA


Ingawa Qur’an kwa kipekee na Uislamu kwa jumla inampa Kristo hadhi ya juu kuliko mtu wingine yoyote, hawachoki kuonyesha mara kwa mara kwamba Yesu ni mtu wa kawaida. Qur’an inasema:

“Haiwi kwa Allah kuwa na mwana, Yeye ametakasika! Anapolihukumia jambo basi huliambia tu: kuwa! Likawa” (Qur’an 19:35).

Sura hiyo hiyo inasema:

“Na wanasemaa ati, mwingi wa Rehema ana mtoto, Hakika mmeleta jambo la kuchukiza sana. Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka na milima kuanguka vipande vipande. Kwa kudai kwao kwamba mwingi wa Rehema ana mwana. Wala hahitaji mwingi wa Rehema kuwa na Mwana. Hapana yoyote aliyeko mbinguni na duniani ila atafika kwa Mwingi wa Rehema kama ni Mtumwa wake tu” (Qur’an 19:88-93)

Hivyo tunaweza kuona ukweli juu ya Yesu kuwa Mwana wa Mungu aliye Mungu kweli na Mwanadamu kweli, ni anathema (laana) kwa Waislamu. Kwa kweli Uislamu unachukulia kwamba hata kujadili tu Uungu wa Kristo na Uwana kwa Baba kuwa Kufuru. Lakini sio sababu pekee inayofanya kuwashirikisha Kweli marafiki zetu na Waislamu tunaowasiliana kuwa ngumu. Kinachofanya hili jambo liwe ngumu zaidi ni Waislamu hawajui hasa kipi hasa Wakristo wanachoamini juu ya Kristo. Wanaamini tu kinachosemwa na Qur’an kuhusu Wakristo wanaamini nini. Na hivi ni vitu viwili vinavyotofautiana sana.

Waislamu hawaelewi – naweza kwenda mbali zaidi kusema hawawezi kuelewa kinachosemwa na Wakristo. Wanaanza kwa kudhamiria kwamba Qur’an ni neno la Allah na hivyo ina usahihi ulio kamilifu. Hivyo Qur’an inaposema Mungu hawezi kuwa na mwana maana hiyo itahitaji kuwa na mke na ndio maana pekee ya kuwa na mwana. Ingawa lugha Kiarabu inatumia neno mwana kumaanisha mahusihino mengi yasio ya ngono, katika mkutadha huu waislamu wamewekewa vikwazo vya kutafisiri dhana ya mwana wa Mungu kwa njia hiyo tu. Ukweli kwamba Qur’an inachukulia dhana ya Mwana wa Mungu vibaya ni muhimu sana, Kwa sababu kama waislamu wangechukulia dhana inayoaminiwa na Wakristo kama ilivyo tu, hii moja kwa moja ingechukulia kwamba Qur’an imekosea. Kama Allah amesema kwamba Wakristo wamesema kwamba Allah ana mwana na mke, basi hilo ndilo linalosemwa na Wakristo! Haijalishi kama kile tunachokiamini ni sahihi au la, maana kwa jambo hili , kukubali kwamba Qur’an imeelewa imani yetu vibaya ni kuikashifu Qur’an. Hivyo ni hatua muhimu sana kumfanya Muislamu kuelewa hasa tunachokiamini, nusu ya vita yenyewe.

Waislamu wanaamini kwamba kusema kwamba Kristo ni mwana wa baba kunamfanya kuwa Mungu- mwenza, ambalo Waislamu wanaamini ni aina ya ushirikina. Hili ni jambo ambalo tungekubaliana na Waislamu kama Kristo angekuwa binadamu wa kawaida; Kweli kuwa na mtu wa kawaida kuwa sawa na Mungu ni ushirikina na kufuru. Pia tunaamini kwamba haiwezekani kabisa kwa mtu wa kawaida kuwa Mungu. Ndio kusema, hatukubaliani wazi na kimsingi kabisa kwamba haya ni mahusihano ya Kristo na baba, kwa sababu tunasema baba na mwana ni kitu kimoja au kama mwandishi wa Waebrania anavyosema “Yeye ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake,” (Waebrania 1:3).

Hivyo tumeona kwamba Waislamu wanaamini (Na lazima waamini), kwamba tunaongelea kuhusu Yesu kuwa mwana wa Mungu, kwamba tunaongelea kuhusu mahusihano ya ngono yanayohitaji baba na mama na hichi ndicho kinachopingwa na Qur' an:

“Yeye ndiye muumbaji wa mbingu na ardhi, Itakuwaje awe na mwana na hana mke? Naye ndiye aliyeumba kila kitu, Naye ni mwenye kujua kila kitu” (Qur’an 6:101)

Waislamu hawaamini kama kuna utoto bila kuwa na mahusihano ya ngono, na Wanazuoni wafafanuzi wa Qur’an wanajenga hoja kukana uwana wa Yesu kwa sababu hii. Tabari, kwa mfano, anasema “ Kwa jinsi gani Allah anaweza kuwa na mwana na hana mke, mwana anaweza kupatikana tu kwa njia ya mwanamme na mwanamke” Hivyo hivyo baidawi anasema “ Kwa Allah kuwa na mwana inamaanisha lazima awe mke aliye sawa na yeye na hilo haiwezekani kwa Allah”

Waislamu wanashangazwa wanapoambiwa kwamba Wakristo hawaamini katika baba, mama, na mwana kwa sababu kulingana na Qur’an huo ndio utatu wa Kikristo:

“Na Mwenyezi Mungu atakaposema; Ewe Isa Mwana wa Maryamu ati wewe uliwambia watu“ Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa miungu badala ya Mwenezi Mungu”?” (Qur’an 5:116).

Baadhi ya Wakristo wanadhani Qur’an inapinga Ukolidayo ambayo ilikuwa na kikundi cha kizushi katika karine za mwanzo kabla ya Uislamu huko Uarabuni ambayo wafuasi wake walimuabudu Mariamu kama mungu mke. Hatujui lolote kuhusu kikundi hiki ispokuwa kile tu kilichosemwa na Askofu wa Salamis wa Kipro, Epifania, aliandika katika mwaka wa 376 BK. Kulingana na yeye. Baadhi ya wanawake katika Uarabuni ambao kwa ujumla ulikuwa wa Kipagani walijumuisha imani za wenyeji pamoja na kumuabudu Mariamu, huku wakitoa keki na mikate kwa wafuasi wao. Hizi keki ziliitwa Coliris (Greek: κολλυρις) na ndio chanzo jina la Ukoliridayo. Lakini uwepo wa kikundi kama hicho unapingwa na Wanazuoni wengi hasa ikizingatiwa kwamba hatuna chanzo kingine zaidi ya Epifania. Kuna dhana nyingi nyingine kwamba mafundisho gani yalichukuliwa na Qur’an. Inaweza kuwa Wamasionia, Wanazarayo, Wamariolitia au wayahudi wa wakati huo. Ni jambo la wazi. Ingawa upinzani wa Qur’an hautokani ma mafundisho sahihi ya imani ya Wakristo ambayo Ukirsto sahihi pia unakataa vyanzo hivyo vinavyotumika na Qur’an. (Kwa mjadala zaidi angalia ukurasa 189 ya The Qur’an in Christian- Muslim Dialogue) Haijalishi kwamba kwa nini Muhammad alikuwa na dhana ya Wakristo kuamini hivyo ingawa Wakristo hawajawahi kuamini au hata kudai Mariamu kuwa mke wa Mungu- hiyo haina umuhimu kwa Waislamu kwa sababu Qur’an inasema kitu kingine.

Sababu moja ya mwisho kwanini Waislamu hawawezi kuamini kwamba Kristo kuwa Mungu ni kwa sababu ya kulingana na Qur’an

“Masihi Mwana Maryamu, si chochote ila ni Mtume,Wamekwishapita Mitume kabla yake, na mama yake ni mwanamke mkweli, Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia tunawabainishia aya, kisha angalia wanavyogeuzwa” (Qur’an 5: 75)

Hivyo kulingana na Qur’an, Kwa sababu Yesu alikula chakula, hiyo inamaanisha alihitaji kwenda chooni, na Allah hawezi kufanya hivyo.

Dhana ya Qur’an kuhusu Yesu inaweza kuwekwa katika mukhtasari kama ifuatavyo:

A. “Hakika Masihi Isa Mwana wa Maryamu, alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu tu, Na neno lake alilompelekea Maryamu, na Roho iliyotoka kwake, Basi muaminini Mungu na Mitume wake, Msiseme, watatu, Komeni na itakuwa heri kwenu” (Qur’an 4:171)
B. “Akasema! (Yesu) Lol, Mimi ni Mtumwa wa Mungu tu, Mwenyezi Mungu amenipa Kitabu, na amenifanya nabii.” (Qur’an 19:30)
C. “Kweli Mfano wa Isa mbele za Mungu ni kama mfano wa Adam: alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia. Kuwa na akawa.” (Qur’an 3:59)

Hivyo msingi wa dhana ya Kiislamu kuhusu Kristo ni kwamba yeye ni mwanadamu ambaye Allah alimtuma kama Mtume kwa ajili ya Wayahudi na kitabu kiitwacho Injili ili kuwasahihisha Wayahudi ambao walikuwa wamekengeuka kinyume na dini yao, na walipotaka kumuua Allah alimyanyua Mbinguni, na siku za mwisho atarudi chini, kumfuata Imam wa Kiislamu, kuvunja misalaba, kuua nguruwe, ataoa , atakufa na kuzikwa karibu na Muhammad. Hawezi kuwa Mungu kwa sababu alikuwa akiomba, akifunga, akila na kunywa na kwa sababu alizaliwa na mwanamke. Hivyo ni kiumbe tu na kiumbe hawezi kuwa Mungu.

Imani ya Kiislamu kuhusu Kristo kimsingi ni tofauti sana na kweli za Biblia. Ni kweli tunakubaliana na mambo mawili lakini tunatofautiana mafafaunuzi yake na uelewa wake.

1. Kristo ni Mtumwa wa Mungu. Biblia inasema Kristo ni nabii, Kuhani na Mfalme na Mtumwa wa Bwana (Isaya 43:10; Wafilipi 2:6-7; Isaya 42:1) Wakristo hawaoni kwamba kuamini kwamba Kristo ni Mtumwa wa Bwana inapingana na Uungu wake. Swali ambalo tunatakiwa kuuliza Waislamu tunaowasiliana nao ni: Kama alichagua kuwa mwanadamu, anapaswa kuwa Mpagani? Kristo kuwa mtiifu kwa baba ni jambo linalomfanya awe mtu sahihi. Uislamu unathibitisha nusu ya wanachoamini Wakirsto na kwa thabiti wakipinga nusu ya pili. Qur’an imewaacha Waislamu na taswira isiyo sahihi ya Kristo, Biblia na Wakristo juu ya wanachoamini. Hivyo Muislamu ana uchaguzi ama atafute zaidi kuhusu Kristo katika Biblia au akatae kujua zaidi kuhusu wasichoambiwa kwenye Qur’an.

2. Yesu ni mtu, ni kitu ambacho Biblia inakisema mara kwa mara tena. Wasichotaka kufahamu Waislamu, ni dhana ya Kristo kuwa Mtu kamili na Mungu kamili. Biblia inasema “habari ya Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa daudi kwa jinsi ya Mwili na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu kwa ya roho ya utakatifu kwa ufufo wafu, Yesu Kristo Bwana wetu” (Warumi 1:3-4), hili halieleweki kwa Waislamu, kwa sababu ya dhana yao ya msingi, kama tulivyotaja hapo awali, kwamba uwana unaweza kuwa wa kibaolojia tu.

Sababu nyingine ni Waislamu wanatumia neno Allah kwa Kiarabu kama nomino (au jina), huku Biblia ikitumia “Elohim” kwa Kiebrania kama nomino ya kawaida ambayo inaweza kutumika hata kwa watu sio Mungu tu. (Kwa mfano Zab 82:1,6, Kutoka 7:1; Kutoka 21:6; Kutoka 22:8-9) Biblia inaitumia kama mamlaka kamili katika mazingira fulani na kwa usahihi inaweza kutafsiria “ Wenye nguvu”. Neno linalotumiwa na Biblia kama nomino sahihi au jina kuhusu Mungu ni “Yahweh” kwa upekee linatumika kwa Mungu wa kweli pekee yake na haiwezi kutumika kwa yoyote mwingine na sio Elohim. Lakini waislamu wanaposikia Wakristo wakisema Yesu ni Mungu, Baba ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu, wanafikiri tunatumia nomino au jina lile lile sahihi kwa wote watatu. Hivyo wanafikiri tunasema kwamba Yesu ni baba na Yesu Roho Mtakatifu, kwa bahati mbaya haiwezi kusaidia pale wakristo wanapojaribu kuelezea utatu kwa kutumia kanuni za kibinadamu kama vile mlinganisho wa kanuni ya maji kufafanua utatu (maji mgando, Maji kioevu na maji mvuke) hiyo inatia nguvu dhana ya modi ambayo na waislamu wanaidhani. Njia bora zaidi ni kueleza tunavyoamini kwa usahihi na ukweli, na kuacha nguvu ya kushawishi kwa Roho Mtakatifu.

Ni muhimu kutambua kuwa kikwazo cha kwanza ni waislamu kukubali kwamba tunachoamini ni tofauti na kile kinachoelezwa kwenye Qur’an. Waislamu walio wengi hawajui kabisa juu ya Imani ya Kikristo au mafundisho ya Biblia, kwa sababu hawajawahi kukisoma au hawaifahamu ama vyote. Waislamu wengi wanaosema wameisoma Biblia wanamaanisha tu kwamba wamepata kitabu kilichoandikwa na watetezi wa imani ya Kiislamu chenye baadhi ya aya za Biblia ndani yake au wana Biblia ili kuangalia baadhi ya aya zilizonukuliwa na watatezi wa Kiislamu. Binafsi njia yangu ya kwanza ya kukutana na Biblia ilikuwa namna hii, Nimepata Biblia kuangalia aya iliyonukuliwa na kutumiwa na mwandishi wa Kiislamu aliyekuwa akikosoa Ukristo. Waislamu wanaamini wamepata agano la mwisho (Kama ambavyo baadhi ya Waislamu wa Magharibi wanavyopenda kuiita Qur’an). Hivyo basi hawahitaji kusoma Biblia. Kwa ajili gani waisome? kwa sababu kama inakubaliana na Qur’an hawahiitaji na kama inapingana na Qur’an hawaiamini. Na unaweza kujikuta ukichukua mda mrefu kwenye dhana hii na Waislamu unaowasiliana nao kabla ya mjadala wa kweli juu ya mafundisho ya Biblia kuanza.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 08:25 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)