Grace and TruthThis website is under construction ! |
|
Home Afrikaans |
Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 068 (Christian beliefs foreign to Islam)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?
Previous Chapter -- Next Chapter 17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA NNE: FAHAMU VIKWAZO VYA KIISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA MBILI: ULINGANIFU MFUPI WA MADA KATIKA BIBLIA NA QUR’AN
12.3. Imani za Kikristo zilizo ngeni kwenye Uislamu
Hii sio orodha pana, lakini inakupa kwa ufasaha wa dhana ya aina ya mjadala unayoweza kuwa nayo. Utakuta unaongea na mtu ambaye ana mawazo yenye nguvu kuhusu mambo unayoyaamini hata bila kujua kwa ufasaha hasa unaamini nini? Tukiweza kumfanya Muislamu kuwaza kwa umakinifu na katika mfufulizo sahihi, hii itakuwa ni hatua kubwa sana ya kuendelea mbele. Kwa mfano, Ukikuta Muislamu akipinga Mkristo kusali bila kutawadha, tunatakiwa tuwarejeshe nyuma na kuongelea maana ya kiroho ya maombi, aina ya maandalizi ya kiroho ya maombi, jinsi gani hiyo ni muhimu kuliko mambo ya nje yanayoonekana. Lazima tuonyeshe umuhimu wa mambo ya rohoni kuliko ya mwilini. |