Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 070 (Belief in the preservation of the Qur’an and the corruption of the original Bible)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO

13.1. Imani juu ya kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili


Madai ya Waislamu juu ya mada hii yanakuja kutoka katika namna tofauti lakini kimsingi ni kama ifuatavyo:

  • “(Qur’an) ilikaririwa na Muhammad kisha ikaamuriwa kwa Masahaba wake, na kuandikwa chini na waandishi, ambao wali- iangalia kui-hakiki wakati wa uhai wake. Hakuna hata neno katika sura zake 114 imewahi kubadilishwa kwa karne zote hizo” (Baraza la Kiislamu la Australia – Fahamu Uislamu na Waislamu (Jarida), Novemba 1991)
  • “Hakuna kitabu kingine duniani kinachoweza kulingana na Qur’an…. Cha kushangaza kuhusu kitabu hiki cha Allah ni kwamba kimebaki bila kubadilishwa, hata nukta, kwa zaidi ya miaka zaidi ya elfu moja na mia nne…. Hakuna tofauti ya maandishi yanayoweza kukutwa ndani yake. Unaweza kuangalia hili mwenyewe kwa kusikiliza usomaji wake kutoka kwa Waislamu wa maeneo tofauti ya dunia” (Zayed Bin Sultan Al Nahayan Taasisi ya huduma za kijamii, Misingi mikuu ya Uislamu, Abu Dhabi, UAE: 1996, ukurasa wa 4)
  • “Tofauti na Maandiko matakatifu yaliyotangulia Qur’an imetunzwa bila kubadilishwa katika asili yake ya matini ya maandishi ya Kiarabu kutoka wakati kufunuliwa kwake, kama alivyoahidi Mungu ndani yake. Historia imeshuhudia kutimilika kwa ahadi hiyo, kwa maana kitabu cha Mungu kinabaki hadi leo vile vile kama ilivyofunuliwa kwa Muhammad na kusomwa naye. Punde ikakaririwa na masahaba wake na kutunzwa kwenye kumbu kumbu na masahaba wake wengi, Ikarithishwa kwa namna ile ile kwa maelfu ya Waislamu kutoka kizazi hadi kizazi hadi leo hii... Kuna toleo moja tu ya Qur’an; maneno yale yale yaliyofunuliwa yanaendelea kusomwa, kukaririwa, katika lugha yake ya Kiarabu na Waislamu kote Duniani” (Saheeh ya Kimataifa, Ondoa shaka yako juu ya Uislamu, majibu 50 kwa maswali ya kawaida, Saudia Aarabia, Dar Abul- Qasim, 2008, ukurasa 28-29)

Madai haya ya Waislamu yanaweza kuchemshwa chini kwamba:

i) Muhammad alikariri Qur’an wakati wa kufunuliwa kwake.
ii) Muhammad pale pale aliiamuru Qur’an kwa masahaba wake walioiandika chini bila kuihariri.
iii) Kumekuwako na toleo moja tu ya Qur’an.
iv) Nakala zote za Qur’an zinafanana na hakuna tofauti.
v) Qur’an imehifadhiwa kwa ukamilifu.
vi) Qur’an ni ya juu na bora zaidi kuliko maandiko matakatifu mengine maana mengine yote yamebadilishwa, huku Qur’an pekee imehifadhiwa.

Haya madai ya kukuza yamezoeleka sana miongoni mwa Waislamu, iwe ni Wanazuoni au Waislamu wa kawaida; Kimsingi ni matangazo ya kuuza viawanja tu na hayawezi kubaki imara ukifanyika uchunguzi wowote kuyachunguza. Kabla hatujaangalia Biblia inasimama wapi dhidi ya vigezo hivi, Ngoja tuangazie Qur’an yenyewe tuone kama kuna kutosimama katika jambo moja kwenye madai haya.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:06 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)