Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 086 (Marriage)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA SITA: FAHAMU WAONGOFU KUTOKA UISLAMU
SURA YA KUMI NA NNE: SHIDA ZA KIJAMII WANAZOKU TANA NAZO WAONGOFU WAPYA

14.2. Ndoa


Kama Muongofu anaishi katika nchi yenye Waislamu wengi, Inakuwa ngumu sana kuwa na familia mpya kama ni wanaume na kama ni wanawake haiwezekani kabisa. Hii kwa sababu nchi hizi zina sheria za kutaka kila mtu asajili dini wakati wa kuzaliwa na kama alisajiliwa Muislamu basi haiwezekani kabisa kubadilisha dini. Kulingana mafundisho ya Kiislamu (ambayo ni sheria kwenye nchi nyingi zenye Waislamu wengi). Mwanamme wa Kiislamu anaruhusiwa kumuoa Mkristo au Myahudi, lakini Muislamu mwanamke anaruhusiwa kuolewa na Muislamu tu. Ikitokea Muislamu mwanamme ameongoka na kuwa Mkristo Kiimani lakini kwenye Usajili wa kisheria bado ni Muislamu, anaweza kumuoa Mkristo, hata hivyo taarifa zake rasmi bado zitamtambua kama Muislamu, na kama ana watoto watalelewa na kusomeshwa kama Waislamu. Mwanamke hata hivyo hana uchaguzi huo wazi kwake, na kwa kweli anaweza kujikuta anashindwa kukataa ndoa zinazopangwa na kulazimishwa na familia, na kufanya isiwezekane kuishi maisha kama Mkristo.

Baadhi ya makanisa wanajaribu kutataua tatizo hili kwa kutambulisha waongofu wapya kwa kila mmoja kwa mtazamo wapange kuoana. Japo hili inaweza kuonekana kama jambo nzuri- na katika mazingira mengi ni suluhisho nzuri, haijaenda bila magumu yake. Familia hii itaanza maisha bila urithi wa dini wala tamaduni maana wote wameacha utamaduni wa Kiislamu kuingia Kwenye utamaduni wa Kikristo ambapo wao ni wageni. Kwa hiyo wanatakiwa kutengeneza utamaduni na mila mpya wao wenyewe, Wanaanza upya bila msaada wa kifamilia, Kanisa linahitaji kufahamu hili, liweze kuwa kanisa linalokaribisha, na kutoa mkono wa msaada pale inapohitajika.

Baadhi ya nyakati za furaha sana katika utamaduni wa kanisa zinaweza hasa kuzua hisia za huzuni kwa Waongofu. Nyakati kama Chrismas na Pasaka, ambapo kanisa na familia hukusanyika pamoja, kusherehekea, huweza kuwa nyakati ambazo Waongofu hukumbuka kwamba hawana familia ya kusherehekea pamoja nao. (Na inatokea sana kwa muongofu ambaye hajaingia kwenye ndoa).

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 02:54 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)