Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 003 (Nomadic pagans)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU MWANZO WA UISLAMU
SURA YA KWANZA: DINI KABLA YA UISLAMU

1.1. Wahamaji Wapagani


Wakazi wengi walioishi Uarabuni kabla ya Uialsmu walikuwa wafugaji wahamaji, waliofanya kazi katika vitengo vya kikabila zilizogawanyika katika koo ndogo ndogo. Walikuwa ni Washirikina, walioabudu miungu kadhaa wengi. Hawakufuata kwa umadhubuti dini moja badala yake kila familia, ukoo, au kabila waliabudu miungu yao wenyewe huku miungu mingine ikiabudiwa na makabila mengine pia lakini mengine yakiwa maalumu kwa makabila husika tu. Kila tunachokijua kutokana maisha ya Uarabuni kabla ya Uislamu inatokana na vyanzo vya Kiislamu pekee. Kwa kweli, tuna uelewa mdogo sana maana hakuna historia iliyoandikwa wakati huo inayoeleza mda halisi, na hivyo vyanzo vuchache tunavyotegemea (Kitabu cha sanamu na Hisham Ibn al-Kalbi Kutoka Iraq na Tabia ya Ghuba ya Uarabu na Abu Muhammad al-Hasanal-Hamdan) ambavyo viliandikwa miaka mia kadhaa baadaye. Matokeo yake, Uelewa wetu una utata na haujakamilika na mara kwa mara ukijipinga na kutofautiana. Kwa mafno,hatuelewi sana kuhusu miungu iliyoabudiwa kabla ya Uislamu maana tunakosa simulizi za hadith zilizoandikwa na kuhidhiwa ambazo tumezitumia kuelezea miungu ya dini zingine. Inaonekana wazi kwamba eneo hili lilikuwa na miungu ambayo waliwaabudu. Mojawapo wa miungu hiyo aliitwa Allah, Ambaye yaonekana alichukuliwa kama ndiye mungu mkuu na baadhi ya jamii hizi japokuwa sio kama Allah wa Uislamu, alikuwa na uzao ambao pia waliabudiwa kama miungu pia. It is possible that this concept of a supreme god originated with the Christian and Jewish communities. Inawezekana kwamba dhana ya Mungu mkuu asili yake imetokana na jamii za Wakristo na Wayahudi. Nadharia nyingine hata hivyo inapendekeza kwamba jina na neno Allah kawaida ilikuwa wadhifa tu au ufafanuzi ambao ungeweza kutumika kwa yoyote katika miungu mingi iliyokuwa ikiabudiwa wakati huo. Baadhi ya sanamu hizi yaliabudiwa kama waamuzi walio kati yao na mungu mkuu na waja waaminfu waliojiona hawasitahili kuhuishana naye moja kwa moja. Sanamu zingine ziliaminika kwamba zilikaliwa ndani yao na roho iliyowekwa na mungu mkuu, hivyo yoyote ambaye angwawabudu kwa usahihi maombi yake yangejibiwa na roho hiyo iliyo ndani yao.

Wakati jamii ya wahamaji waliabudu huku wakihama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, dini ya wakazi walioweka makazi katika miji yalichukua mfumo wa kisasa zaidi na waliabudu kwenye madhabahu yaliyowekwa wakifu kwa miungu yao. madhabahu hizi nyingi zilijengwa katika muundo wa mchemraba (Kaabas), na ilikuwa mahali pa kuufanyia hija mara kwa mara, Wakati walipotoa kafara na walizunguka zunguka (kutembea huku wakizunguka miungu mawe) wakizitoa. Kulikuwa na kaabas nyingi sana wakati huo- ngalau makumi kwa uchache- yaliyotawanyika katika ghuba ya Uarabuni. Hija katika hizi Kaabas zilifanywa na Waarabu vyote katika majira maalumu na majira mengine yasio maalumu. Walikuwa wakitoa kafara, wakitoa zawadi nakuweka wakifu kwa sanamu zao. Sanamu ziliaminika kwamba ni watakatifu (Hakuna mapigano yaliyoruhusiwa jirani na mahali pao), na Waabudu walipaswa kutoa kwa ajili kuwatuza waliokuwa wakiziangalia sanamu hizi. Kaabas hizi ziljengwa kwa jiwe jeusi; Mawe haya yaikuwa aidha ya volikano au kimondo (Wanazuoni wa Kiislamu wanatofautina kuhusu maoni yao juu ya hili); nadharia ya kimondo inakubalika zaidi kwa sababu kitu kinachohehsimika sana kwa kuzingatia ilivyopatikana-Ikizungukwa na mwanga, ikianguka kutoka ngani (mahali ambapo Allah-mungu mkuu muumbaji kama ilivyonyeshwa mwanzoni aliaminika kuishi). Na pia tunajua kwamba hakukuwa na mlipuko wa Volkano wakati huo tena miaka maelfu mengi sana katika eneo hili, hivyo basi maelezo ya mlipuko wowote ungelikuwepo basi simulizi zake zingesimuliwa na kuhifhadiwa kupitia idadi ya watu wengi kwa vizazi vingi baadaye hivyo uwepo wa jambo sio la kuaminika wala halina uhakika, kama tunavyotambua kila mahali duniani kwamba ibada yoyote iliyohusishwa na mlipuko wa volikano ikijumuisha fujo za matambiko, mifano yake ambayo hatuna kumbukumbu yoyote katika bara la Arabu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 03, 2024, at 05:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)