Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 001 (INTRODUCTION)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu

UTANGULIZI


Wengi wetu duniani, bila kujali tunapoishi na uhuru wa historia yetu wenyewe, tunao majirani Waislamu, Wafanyakazi wenzetu, marafiki, and mawasiliano nao. Unaweza kujihisi- Kama wanavyohisi wakristo wengi- Kwamba Uislamu ni nyani mkubwa mwenye uzito wa kilo 900 ambaye huwezi kujadiliana naye. Kitabu hiki ni kwa ajili yako,kama umekuwa Mkristo kwa miongo na wadhifa wa uongozi katika kanisa mahalia au wewe ni Mwongofu mpya asiye na mafunzo ya elimu ya dini yoyote – kwa urahisi una moyo wa kuwafikia Wasilamu ili kuwaleta wa Kristo. Hauhitaji mafunzo mengi; unayohitahi hasa ni ufahamu wa mambo machache yenye umuhimu wa msingi mbayo kitabu hiki kitabu kitatoa mukhtasari wake.

Tutaanza na mchoro wa kijpicha cha historia ya Uislamu, Kwanza kwa kutazama Bara la Uarabuni kabla ya uislamu ili kupata uelewa wa mazingira ambayo Muhammad alipeleka ujumbe wake, kasha kwenda mbele kwenye maisha ya Muhammad (Kijitabu cha 1). Sehemu ya pili inashughulika na Imani na matendo ya faradhi ya Uislamu, ikijumuisha kwa kuonyesha ni kwa jinsi gani kimsingi yanatofautiana na mafundisho ya Biblia (Kijitabu cha 2). Sehemu ya tatu inatoa utambuzi juu ya mambo ambayo Waislamu wanaamini kuhusu Kristo (Kijitabu cha 3). Sehemu ya nne inazingatia magumu ambayo Wakristo wanaweza kukutana nayo wanapowahubiria Waislamu na changamoto ambazo Waislamu wanapaswa kuzishida wanapozingatia kuwa Wakristo, na inaweka mbele ushauri wa jumla kwa Mkristo ( Kijitabu cha 4). Sehemu ya tano inalenga mambo ya kawaida ambayo Waislamu wanatuamia kukataa Injili na namna ya kushughulika nayo (Kijitabu cha 5). Sehemu ya mwisho inakupa kutambua wanayoyapitia waongofu wanapoacha Uislamu, na inakupa njia kadhaa ambazo kanisa inaweza kutumia katika kusaidia Waongofu wanapochukua hatua ngumu ya Kumfuata Kristo (Kijitabu cha 6).

Sehemu ya mwisho inakupa kutambua wanayoyapitia waongofu wanapoacha Uislamu, na inakupa njia kadhaa ambazo kanisa inaweza kutumia katika kusaidia Waongofu wanapochukua hatua ngumu ya Kumfuata Kristo (Kijitabu cha 6)

– Kwa umbali sana ndio tawi kubwa kuliko yote,Ikijumuisha idadi ya 90% ya waislamu wote dunia nzima; na
– ndio ambayo naijua zaidi, nimelelewa katika familia na jamii ya Ki-Sunni na kiukweli nimekuwa mfuasi makini wa madhehebu ya Ki-Sunni katika maisha yangu ya awali.

Ni muhimu pia kukumbuka kwamba ijapokuwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni hutegemea katika mafundisho, tafsiri, na matendo yale yale lakini yanatofautiana kulingana na maeneo tofauti hata kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Hivyo basi hatuwezi kudhania kwmaba kila mtu anayejiita Muislamu kwa pamoja wanaamini namna -haiwi hivyo. TKitabu hiki kinatoa muhtasari wa mafundisho ya Uislamu kama yalivyoendelezwa na maandiko yanayokubalika na mamlaka sahihi, yanayoitwa Qur’an na Sunnah (maneno na matendo ya Muhammad kama yalivyohifadhiwa). Isipokuwa kama ikionyeshwa vinginevyo katika maandishi, Mimi hasa ninanukuu kutoka kwenye Qur’an Tukufu (Iliyotafisriwa na Al-Hilali na Khan). Mkusanyiko huu una majina tofauti kutegemea na aina ya nakala; ambazo zinakubaliwa zaidi kwa ujumla wake kama ndizo za kuaminika (au halisi) kwa Waislamu zinajulikana kama “sahihi”, lakini nifanya marejeo kwa aina nyingine ya mkusanyiko huo kama “Musnad”, na pia kama “Sunna” ambayo ni Kumbukumbu zilizohifadhiwa za mkusanyiko mwingi wa maneno na matendo ya Muhammad. Nitataja nakala mbili za wasifu wa Muhammad (Sirahs) yaliyoandikwa na Ibin Kathir na Ibin Hisham ambazo pia yanachukuliwa kama vuanzo vya kuaminika kwa kuendeleza mafundisho sahihi ya Uislamu

Tafsiri ya Hadith na za Sirahs ni zangu ispokuwa ikionyeshwa vinginevyo. Pale ambapo unukuzi wa majina ya Kiarabu inahitajika, nimeonelea kutumia imla ya Kiingereza ambayo kwa ujumla yanatambulika japokuwa hili saa zinge isifuate uthabiti au kiufundi ziwe sahihi wa unukuzi katika Muundo wa neon. Mahali ambapo hakuna toleo la Kiingereza, nimebuni muundo wa neno mwenyewe.

Mwisho, tafadhali fahamu kwamba kwa shauku kubwa ninaamini kwamba Wakristo Waongofu waliokuwa zamani Waislamu hawapaswi kutengwa kwa namna na yoyote. Sisi Wakristo, hatuna umalaamu wowote wa ziada au mdogo,hatuna wema au ovu kuliko Wakristo wengine waliokolewa kutoka kuzimu na damu ya Kristo. Kuendelea kutuita “Waongofu kutoka Uislamu” badala ya Waaminii inaumiza na ina madhara. Hata hivyo, aina ya vitu vinavyojadiliwa katika kitabu hiki inanilazimu kuwa wazi kipekee kidogo na kutumia neno “Mwongofu Muislamu”.Wengine wanaweza kupendelea maneno mengine, kama vile “Mwamini aliyeacha Uislamu". Nina ombi dogo tu kwako, kwamba mahali ambapo hakuna haja ya lazima ya kipekee kutambulisha imani yao ya zamani, Wataje kaka na dada zetu katika Kristo kama Wakristo, au Waamini, au jina lolote ambayo eneo lenu mnatumia kuwaelezea wale walio katika ushirika wenu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 03, 2024, at 05:30 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)