Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 010 (Mohammed’s first marriage and the call to prophethood)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU MWANZO WA UISLAMU
SURA YA PILI: MAISHA YA MUHAMMAD

2.2. Ndoa ya kwanza ya Muhammad na wito wake wa utume


Vyanzo vya Kislamu vipo kimya kuhusu ya maisha ya Muhammad kati ya miaka kumi na mbili na arobaini, ingawa tuna taarifa ya mambo muhimu mawili katika wakati huu: kwanza ni ndoa yake na Khadija, pili ni kwa dhahiri wito wake wa utume.

Kama kijana wa kiume, Muhammad aliajiriwa na mwanamke tajiri mjane kutoka kwenye familia nyingine ndani wa kabila yake kuwajibika kwa misafara yake ya Kibiashara. Jina lake aliitwa Khadija; Alikuwa ameshaolewa mara tatu na alikuwa na watoto kutoka katika kila ndoa yake. Hatujui kwa nini Muhammad alipewa majukumu hayo katika umri wa mdogo wa ujana hivyo, au kwa nini badaye Khadija aliamua kuolewa naye. Aliomba kuolewa naye akiwa na ishsirini na tani na Khadija akiwa miaka arobaini. Kulingana na vyanzo vingine vya Kiislamu Khadija alipika chakula na kutengenza pombe, akamuita baba yake na watu wengine wa kabila lake, wakala na kunywa mpaka wakalewa. Halafu Khadija akamwambia baba yake “Muhammad bin Abdullah anataka kuniona; nioze kwake”. Hivyo akamuoza kwake, Akampulizia manukato (kwa baba yake) na akamvisha vazi la kimila linaloitwa hullah (Kanzu maalumu inayonakishiwa kwa dhahabu na inavaliwa kwenye matukio maalumu) kama utamaduni wa Maka ulivyo. Ufahamu wake uliporudi, akajikuta amejifukiza manukato na amevaa hullah “Kitu gani kimetokea kwangu? Hiki ni nini?” Akauliza. Khadija akajibu: “Umenioza kuwa mke wa Muhammad bin Abdullah” “Nimekuoza kwa yatima wa Abu Talib?” Akashangaa baba yake, “ la. Haiwezekani kamwe!” “Je hautajisikia aibu kuonekana kama mjinga mbele Wakureshi na kuwambia watu kwamba ulikuwa umelewa?” Akauliza Khadija, Akamng’ang’ania mpaka baba yake akaridhia, licha ya kutokuwa tayari kwa binti yake kuolewa na mwanamme asiye na wazazi, bila matarijio yoyote ya Kifedha. (Ahmad ibn Hanbal, Musnad)

Kumuoa khadija ilimruhusu Muhammad kuwa mda zaidi kwa ajili kujenga na kukuza akili yake, na kutafuta maana katika Ulimwengu wa kiroho. Baada ya mda kidogo tu Muhammad alianza kuona maono. Kwa kuogopa kwamba inawezekana amepagawa na mapepo, akamshirikisha mke ambaye alichukua kwenda kwa binamu yake, Waraqa aliyekuwa Mkristo wa aina ya aliyefuata imani ya kizushi. Kama mtu aliyekuwa na ufahamu juu ya imani kwa Mungu mmoja, na sio mshirikina, Khadija alijua kwamba alikuwa na uwezo wa kufahamu kinachomotekea Muhammad. Waraqa akamwambia Muhammad kwamba maono yake yanamaanisha yeye ni mtume kama ilivyokuwa kwa Musa, na ndivyo mbegu ilivyopandwa na kumwagiliwa katika akili ya Muhammad.

Waraqa alikufa mda mfupi baada hapa,na maono ya Muhammad yakasimama kwa mda. Kwa sababu ya maono yake kusimama, Muhammad alianza kujishakia binafsi na akawa fadhaiko hata alijaribu mara kdhaa kujitupa kutoka juu ya mlima, lakini kila mara Gabriel alimtokea na kumwambia “Hakika wewe ni mjumbe wa Allah” (Bukhari, Sahih). Kwa mjibu wa simulizi zote Muhammad bado hakuwa na uhakika, alihitaji kuhakikishiwa zaidi. Tunazo simulizi nyingi jinsi Khadija alijaribu alivyomshawishi Muhammad kwamba alichokiona ni Malaika sio pepo mbaya. Mojawapo ya simulizi hizo, imehadithiwa na Ibin Ishaq, Mwandishi wa awali kabisa wa wasifu wa Muhammad:

Imepokelewa kutoka kwa Khadija, alimwambiwa Mtume wa Allah, we mwana wa mjomba wangu, unaweza kunitaarifu juu mgeni wako, mara akija kwako? Akasema anaweza,akamwomba amtaarifu akija. Basi wakati Gabriel alipokuja kwake, kama alivyotaka Mtume akamwmabia Khadija, ‘Huyu ni Gabriel ambaye amekuja mara tu kwangu’, Inuka ewe mwana wa mjomba wangu,akasema, cann juu ya paja langu la kushoto’. Mtume akafanya hivyo,na akasma, ‘Je unaweza kumuona?’ ‘Ndio’, akasema. Akamwambia, geuka na kaa juu ya paja yangu ya kulia,’ akafanya hivyi, na akasema, ‘Je unaweza kumuona?’ Aliposema ndio, alifunua umbo lake na akavua hijabu yake huku Mtume akimkalia magotini, kasha akasema ‘Je unaweza kumuona?’Akajibu, Hapana ‘ewe mwana wa mjomba wangu, furahi na kuwa amani moyoni,naapa kwa Allak ni malaika na sio shetani” (Ibn Ishaq- Maisha ya Muhammad)

Hivyo kwa kuonyesha kwamba Yule mgeni alionyesha heshima kwake Khadija na kupotea alifunua ushungi na nywele zaje kuonekana, Amamuaminisha Muhammad kwamba lazima huyo mgeni ni malaika wala sio pepo mbaya ambaye asingeweza kuonyesha heshima hiyo.

Hivyo basi Khadija na Waraqa- kulingana na wana historia ndio walikuwa wa kwanza kuamini kwamba Muhammad ni Mtume na kumshwaishi naye aamini hivyo.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 06, 2024, at 04:28 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)