Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 009 (His Childhood)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU MWANZO WA UISLAMU
SURA YA PILI: MAISHA YA MUHAMMAD

2.1. Utoto wake


Baba yake Muhammad alikuwa ni tajiri na anayetoka katika ukoo ulioheshimika wa Hashimu wa mji wa Maka magharibi ya pwani ya Ghuba ya Uarabuni, sehemu ya jamii ya kiutawala wa kabila la Wakureshi, na mama yake alitoka katika kabila la Banu Zahra katika mji wa Madina.Kilometa mia kadhaa Kaskazini. Wakati wa ndoa, kulingana na mila mama yake aliondoka kwao na kuhamia Maka kujiunga na mme wake na familia yam me wake. Japokuwa baba yake Muhammad alikufa kabla hajazaliwa, hata hivyo alizingatiwa Kama sehemu ya kabila ya baba yake.

Kwa wakati wake, na hadhi ya kijamii, utoto wa Muhammad hakuwa kipekee na hali isiokuwa ya kawaida. Kama watoto wengi wa Maka wa umri wake, alipelekwa kulelewa na yaya mlezi. Hivyo miaka yake ya malezi ya utoto ilikuwa nje ya umashuuri wa mji wa Maka, aliishi kwa miaka karibia sita pamoja yaya mlezi wake aliyemnyonyesha pia Halimah al-Sa’diah kutoka kabila Bani Sa’d wa Madina. Kwa kuishi madina alikuwa na muingiliano wa kila siku wa kimaisha na Wayahudi,Kwa wakati huo kulikuwa na kulikuwa na makabila mawili tu makubwa ya Waarabu (Wapagani) Madina, lakini kulikuwa na makabila makubwa matatu ambao walihamia kutoka Mashariki ya kati krine kadhha zilizopita na kuweka makazi ya kudumu Uarabuni, wakishughulika na kazi za biashara na kutengeneza vito vya thamani na madini. Japokuwa alikuwa bado mdogo kwa wakti huu, lakini innawezekana alikuwa na uzoefu na baadhi ya mila za Kiyahudi, ambayo hatimaye vinaweza kutuangazia kufanana sana kwa baadhi ya atendo baina ya wayahudi na waislamu.

Waislamu wanatuhathia jinsi ambavyo malaikawalitakasa moyo wake wakati huu wa makuzi yake. Bukharin a Muslim (Wakusanyaji wawili wa Hadith- maneno ya Muhammad- yanayozingatiwa na kutegemewa zaidi na Waislamu wa Sunni) wanatutaarifu Muhammad alivyoeleza namna malaika Gabriel (Anajulikana kama Jibril kwa Waislamu) alivyotakasa moyo wake ndani ya maji ya Zamzam. Zamzam ilikuwa (bado ipo) ni kisma katika mji alimokulia Muhammad wa Maka, ilikuwa hasa mbali kutoka Madina alikokuwa akiishi wakati huu wa utoto wake pamoja yaya mnyonyeshaji. Inazingatiwa kama ni kisima kitakatifuna Waislamu.

“Paa ya nyumba ilifunuliwa nilipokuwa Maka na Jibril akashuka chini akapasua kugawanya kifua change, kisha akausafisha kwa maji ya Zam zam. Halafu akaleta bakuli iliyonakishiwa kwa dhahabu ndani yake kumejaa hekima, imani anakaputisha yote kifuani mwangu. Kisha akafunga kifunga changu...” (Imesimuliwa na wote Bukharin a Muslim).

Wengine wanasimulia habari tofauti. Mmoja wa masahaba wake wa karibu. Anas ibn malik, kwa mafano, anasimulia kwamba Jibril alikuja kwa Mjume wa Allah alipokuwa akicheza na watoto wenzake wa kiume. Akamshika na kumtupa chini, kasha akafungua kifua chake na kuchukua moyo wake nje ya mwili kutoka katika moyo akachukua pande la damu iliyoganda na kusema: “ hii ilikuwa ni sehemu ya shetani ndani yako” Kisha akaisafisha kwenye bakuli ya dhahabu iliyojazwa maji ya Zamzam. Kisha akairudisha mahali pake kwa pamoja. Vijana wenzake wa kiume wakakimbia kwenda kwa mama yake- ikimaanisha yaya wake na kusema “ Muhammad ameuwawa” wamarejea kwake na rangi yake ilikuwa imebadilika. Anas anasimulia: “Nilikuwa nikiona alama ya mshono katika kifua chake” (tolea hili pia imejuimiswa kwenye Sahih Muslim).

Bado kuna simulizi zingine zinasema kwamba haikuwa Jibril bali malaika wawili. Kama hizi ni simulizi mbili kwa jambo moja au taarifa ya matukio mawili tofauti, lakini wana historia wanasema kwamba mama yake mlezi wa Muhamma(yaya wake Halimah) aliogopa sana na akalazimika kumrejesha kwa familia yake Maka ambako mama yake alimlea hadi kifo chake kwa mda mchache chini ya mwaka mmoja akiwa njiani kutoka kuwasalimia ndugu zake wa Madina. Baada ya kifo cha mama yake,kulelewa kwa Muhammad kuliangukia kwa babu yake, ambaye naye alikufa miaka miwili badaye. Ndipo Muhammad akawa mwana familia wa baba yake mdogo, Abu Talib, aliyemlea kwa pamoja na watoto wake wa kuzaa nane.

Abu talib alikuwa ni kiongozi wa ukoo wa Hashimu,tawi la kabila la Wakureshi wa Maka ambayo baba yake Muhammad alitoka. Alikuwa mfanyabishara kwa taaluma japo kiuchumi hakuwa tajiri sana.( Kwa hakika kuna wakati badaye katika maisha yake, alikuwa na matatizo ya kifedha , hadi hakuweza kuwahudumia watoto wake wadogo) Yeye pamoja na ukoo wake walikuwa ni watu wa kuheshimika sana katika jamii yao na walishika nafsi za uongoz zenye hadhi ya juu. Akiwa na miaka kumi na mbili Muhammad alimsindika Abu Talib kwenye safari ya kibiashara Mashariki ya kati. Huu ndio wakati ambapo Muhammad kulingana mapokeo ya Uislamu- Alipokutana kwa mara ya kwanza na Mkristo. Huko alikutana na mtawa aliyeitwa Bahira, ambaye labda alikuwa ni Mwebonia, Mnestori au Wagnostiki wa Kinasarayo. (Simulizi hii ina taarifa zinazotofautiana). Inasemekana kwamba Bahira alitabiri maisha ya badaye ya kijana Muhammad kwamba atakuja kuwa mtume kwa sababu ya alama ya kuzaliwa aliyoiona kati kati ya mabega ya Muhammad. Baadhi yaWaislamu wanaona alama hii kama ndio mhuri wa utume wake.

Kipi tunachoweza kujifunza, basi, kutoka kwenye simulizi za maisha ya awali ya Muhammad? Kwanza, tunajua kwamba alikuwa na uzoefu na uelewa kwa kiwango Fulani na tamaduni za Wakirsto na Wayahudi, japokuwa inapaswa kukumbuka kwamba Wakristo walioishi maeneo haya walihesabiwa kuwa wazushi. Hii inaweza kueleza kwa nini mafundisho ya awali ya Uislamu yalifanana sana nay a Kiyahudi (na pia kwa nini rejea zake nyingi kuhusu imani ya Kikristo ndani ya Qur’an hazikuwa sahihi). Na pili bika kujali usahihi wa simulizi, inaonekana wazi kwamba Muhammad alijiona binafsi kama mtu aliyengewa kutoka maisha ya utoto, na alikusudiwa ukuu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 06, 2024, at 04:24 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)