Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 016 (AXIOM 3: Belief in the existence of the books of which God is the author)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA TATU: NGUZO ZA IMANI

3.3. IMANI 3: Imani katika uwepo wa vitabu ambavyo viliandikwa na Mungu


Waislamu wanaamini kwamba Mungu aliandika vitabu 315 (Kama Muhammad alivyofundisha na ikasimuliwa katika Hadith). Kila mojawapo kilishushwa kwa wanadamu kupitia mtume na zama zake. Hata hivyo, ni mitume wanane waliopewa vitabu wametambuliwa ndani ya Qur’an. Nao ni:

‒ Musa, ambaye kwake ilifunuliwa Torati,
‒ Daudi, ambaye kwake ilifunuliwa Zaburi
‒ Isa (Yesu), ambaye kwake ilifunuliwa Injili
‒ Muhammad, ambaye kwake ilifunuliwa Qur’an,

Na wengine wanne ambao hatuambiwi chochote juu ya vitabu vyao:

‒ Adam
‒ Sethi
‒ Idrisa (kwa ujumla wake inaaminika ni Henoko wa Agano la kale)
‒ Ibrahimu

Mitume wengine 307 waliobaki na vitabu vyao hawatajwi kwa majina wala vitabu vyao ndani ya Qur’an wala Hadith, hatuna taarifa yoyote juu yao wala mitume wengine waliowapokea kwa kufuata baada yao. Hii imefanya kuwe na uvumi mwingi inayohusu utambusliho wa mitume hawa. (Baadhi ya Waislamu wanaamini kwamba mmojawao inaweza kumjumuisha Farao Akhenaten, Kwa mfano). Kila kitabu kilipaswa kifuatwe hadi kitabu kingine kifunuliwe badala yake ndio cha awali ikome kufuatwa. Ikifikia hapo basi ufunuo mpya unachukua nafasi ya ufunuo zamani. Muhammad inasimuliwa kwamba ndiye wa mwisho, hivyo hakutakuwa na ufunuo zaidi tena wa kubatilisha Qur’an.

Leo hii Waislamu wengi wanaamini Qur’an tulivyo nayo sasa ni ile ile aliyokuwa nayo Muhammad, na ni neno la Allah lisiloumbwa, la milele. Hata hivyo, sio Waislamu wote wanaokubaliana na hili wakati wote. Miaka mia mbili baada ya kifo cha Muhammad kulikuwa na mjadala wa wanazuoni wa Kiislamu uliochukua takribani miaka 18 inayohusu asili ya Qur’an (“Mihnat khalq al- Qur’an” au shida kuhusu uumbaji wa Qur’an) Wanazuoni wa Kiislamu kote katika himaya ya Kiislamu ya wakati huu walikuwa na mawazo yanayokinzana. Waislamu waliojitambuslisha kwa mataifa yao zaidi walisema kwamba Qur’an sio ya milele; badala yake iliumbwa na Allah na haikuwa kitu cha muujiza. Waislamu wa madhehebu ya Sunni kwa upande mwingine waliamini kwamba Qur’an ni neno la milele la Allah, isiyoumbwa, na ni muujiza. Makhalifa (Watawala wa Kiislamu) waliegemea upande wa wanazuoni wanaoegemea utaifa zaidi, hivyo wanazuoni wa madhehebu ya Sunni wengi waliuwawa, walichapwa viboko,au kufungwa. Mjadala huu kimsingi ulimalizika wakati ambapo Khalifa Mutawakkil alipobadilisha maoni yake na alipoamuru kugeuzwa kwa fundisho hii.

Vipi kuhusu Torati, Zaburi na Injili? Muhammad inasimuliwa kwamba alisema “Msiwaamini watu wa kitabu, wala kutokuwaamini” lakini semeni ‘Tunamwamini Allah na yaliyofunuliwa kwetu, na yaliyofunuliwa kwenu” (Sahih Bukhari). Hata hivyo, Waislamu wanaamini kwamba Qur’an pekee ndio iliyotunza uhai wa usahihi na ufasaha wake na kubaki na asili yake ile ile, ila vitabu vingine maandiko yake yameharibiwa. Tutarejea badaye kwenye mjadala huu, lakini kwa sasa tuonyeshe kwamba lawama kama hiyo-vile vile ilivyo haina ushahidi wowote- pia haina mantiki katika ubora wake. Waislamu wanadai kwamba Biblia imeharibiwa, bila ushahidi wowote, madai yanayofanana na haya, yanatolewa na Waislamu wa madhehebu ya Sh’ia kwamba Waislamu wa madhehebu ya Sunni wameiharibu Qur’an. Katika madai yote haya: Ni ushahidi gani mnayo kuthibitisha madai yenu haya? Na kama Allah hakuweza kulinda mafunuo yake ya awali, kipi kinatufanya kudhani anaweza kuilinda Qur’an?

Tunaweza kuendelea kuwaza ya kuwa imani yao juu ya Injili ya asili ya Isa (Yesu) yaweza kuwa hatua nzuri pa kuanzia mjadala na Waislamu. Kwa bahati mbaya, karibu kila kitu kuhusu Injili katika Uislamu ni yenye matatizo, kuanzia na jina. Neno Injili linatokana na neno la Kiyunani “ευαγγέλιον” (euangelion). Tatizo la neno hili lenye asili ya Kiyunani.Qur’an inasema kwamba: “Na hatukumtuma mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake” (Qur’an 14:4). Inasema pia Yesu alitumwa kwa wana wa Israel, na tunauliza kwa nini mtume wa Kiyahudi atumwe na kitabu cha Kiyunani. Suala lingine ni Waislamu wanaamini kwamba Injili nne katika Agano Jipya sio Injili, na hivyo basi havijavuviwa na Mungu. Na bado kama tutakavyojadilli katika sura inayofuata, wanadai kwamba Agano jipya ina unabii juu ya Muhammad. Kwa nini hili ni la muhimu, maana hawaamini Agano jipya kuwa ya kweli! Isipokuwa wanaamini tu baadhi ya aya ziizotawanyika za Biblia, Wakikubali chochote wanachofikiri kinapatana na Uislamu na kukataa chochote kisichokubaliana na Uislamu. Ingawa Mtume Paulo anakataliwa karibia na Waislamu wote kama mdanganyifu na muongo, lakini Muhammad alichukua baadhi ya maneno ya Paulo katika 1 Wakorintho 2:9 na kuzifanya kama sifa za Allah kama tutakavyoona badaye.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 04:38 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)