Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 017 (AXIOM 4: Belief in the Prophets)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA TATU: NGUZO ZA IMANI

3.4. IMANI 4: Imani katika Mitume


Uislamu unafundisha ya kuwa mitume 144,000 wametumwa kwa wanadamu kote katika historia, japokuwa tunajua 25 tu kati yao (Waliotajwa katika Qur’an). Kila mmoja alipokea ufunuo kutoka kwa Mungu, kama ilivyoonyeshwa juu,waliita watu kufuata kitabu cha mtume aliyetangulia kabla, wangine ni watu maarufu waliotajwa katika historia ndani ya Biblia, lakini wengi wao hawajatajwa. Muhammad alikuwa ni mwisho wa manabii, na Yesu ni wa mwisho kabla ya Muhammad (ndio maana Muhammad kwa dhahiri aliita watu kufuata mafundisho ya Injili). Manabii walitumwa kuwaongoza watu kwa Allah.

Kati ya manabii hawa, 315 wanachukuliwa kuwa ni mitume kama ilivyoonyeshwa juu, mitume walikuwa ni manabii ambao Waislamu wanaamini walivuviwa vitabu vya Mungu.Hivyo basi mitume wote walikuwa manabii, lakini sio manabii wote walikuwa mitume. Waislamu- kulingana na Muhammad- wanadai kuwaaamini wote manabii na mitume.

Waislamu wanaamini manabii wote hawana makosa, ndio kusema wasingeweza kufanya makosa au ubaya. Imani hii kwa haraka inaleta matatizo kwa Waislamu, maana Qur’an kweli ina kumbu kumbu za dhambi za baadhi ya manabii, kama vile Musa kuua, Ibrahimu kudanganya, Daudi kufanya uzinzi, hakuna patano ya dhambi hizi na imani ya manabii kutokukosea, zaidi ya hapo wanakubaliana na anguko la Adam- na eti bado alibaki bila dhambi? Na Muhammad pia inasimuliwa kwamba dhambi zake zilisamehewa- eti na bado alidumu kuwa nabii asiyekosea ambaye hakuwahi kufanya dhambi yoyote ile?

Moja ya sababu inayoleta mkanganyiko huu katika Qur’an na Hadith ni ya kwamba hazitoi taswira iliyo wazi na halisi ya manabii wanaotajwa, na wakati mwingine ujumbe unajipina wenyewe. Mafundisho ya Kiislamu yametofautiana kabisa na maandiko ya kihistoria ndani ya Biblia. Chukulia mfano wa suala la Musa: Qur’an inasema:

“Tukamplekea Musa na ndugu yake wahyi huu: Watengenezeeni majumba watu wenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndio mahali pa ibada, na mshike sala na muwabashirie waumini.” (10:87)

Na mahali kwingine:

“Na farao akataka kuwafukuza katika nchi.Na hivyo tukamzamisha yeye na waliokuwa pamoja naye. Na tukawambia baada yake wana wa Israel: Kaeni katika nchi.Itakapokuja ahadi ya akhera tutakuleteni nyote pamoja” (Qur’an 17:103-104)

Inaonekana kwamba Musa aliwaita Waisrael kubaki Misri na eti Farao ndiye aliyekuwa ajaribu kuwaondoa watoke, na baada ya kuzamishwa, Waisrael walibaki na kukaa Misri. Hii bila shaka ni kinyume kabisa na kilichotokea, haijawahi kuandikwa na mwana historia yoyote wa Kiyahudi wala kuaminiwa na Myahudi yoyote yule. Musa alikuja kuwaondoa Waisrael Misri na sio kuwafanya wabaki na kukaa humo, na Farao ndiye ambaye alikuwa anataka kuwatumikisha Waisrael na sio kuwaondoa Misri.

Waislamu pia wanaamini kwamba kuna manabii watano wanaoitwa “Ulu-ai-Azm” (Wenye nia kali):

"Na tulipochukua ahadi kwa manabii na kwako wewe, na Nuhu, na Ibrahim, na Isa mwana wa Mariamu na tulichukua kwao ahadi ngumu” (Qur’an 33:7)

Waislamu wanafundishwa kuamini manabii wote na kuwaheshimu wote sawa bila kuweka yoyote juu ya mwingine. Qur’an inasema:

“Na mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na mitume wake. Hatutofautushi baina ya yeyote katika Mitume wake.” (Qur’an 2:285)

Hata hivyo hadith nyingi kwa kweli zinaweka tofauti baina ya mitume- nyingi zinamuinua zaidi Muhammad-hazionekani kukubaliana na Qur’an katika jambo hili. Kwa mfano, Muhammad alisema kuhusu yeye binafsi kwamba:

Mfano wangu na wa manabii waliotagulia kabla yangu ni kama wa mtu aliyejenga jengo, akaijenga vizuri akaifanya ni ya kupendeza, isipokuwa kulikuwa na nyufa katika mojawapo ya kona zake (Jiwe kuu la pembeni). Watu wakaanza kuizunguka na kuitamani huku wakisema: Kwa nini tofari moja inakosekana? Mimi ndiye tofari hilo (Jiwe kuu la pembeni) Mimi ni mhuri wa manabii” (Sahih Muslim)

Mfano mwingine umesimuliwa kwa sawia katika Sahihi Muslim:

“Nitakuwa bwana wa wana wa Adam siku ya ufufuo, wa kwanza ambaye kaburi lake litafunguliwa, wa kwanza kufanya maombezi na ambaye maombi yake yatakuwa ya kwanza kupokelewa.”

Uislamu unaofuatwa sehemu mbali mbali duniani hasa katika kaya masikini za mjini na watu wanaoishi vijijini wametoa majina ya ziada katika kumueleza Muhammad ambayo hayajawahi kutolewa kwa mtu yoyote yule. Kwa mfano, kuna majina zaidi ya 200 yameandikwa juu ya ukuta wa msikiti alipozikwa Muhammad, ikijumuisha Roho Mtakatifu, ufunguo wa mbinguni, ishara ya imani, anayesamehe dhambi, mwenye rehema, na bwana wa wana wa Adam. Hakuna kati ya haya majina popote katika Qur’an au hadith ambapo mtume anaitwa hivyo. Waislamu wengine wa madhehebu ya Sufi wanaenda mbali zaidi na kumuita kiumbe wa kwanza, nuru ya kiti cha enzi cha Allah, Mpatanishi, nuru ya zama zote, na mlinzi wa maarifa ya Allah. Simulizi nyingi za miujiza ya Muhammad zinazomsifia Muhammad zilikuja mda mrefu sana baada ya kufa kwake, japokuwa hakuna kumbukumbu yoyote ya miujiza hii katika makusanyo ya Hadith wala katika vitabu vya historia, basi inaelekea vimetungwa badala ya kweli. Nyingi katika hizi ni miujiza inayofanana na manabii kabla ya Muhammad, lakini katika kila suala muujiza na kipaji cha Muhammad kinazidi ya wale waliomtangulia. Mfano katika Uislamu Qur’an inafundisha kwamba Suleiman alikuwa na uwezo wa kuongea na wanyama; katika simulizi za mda mrefu sana baada ya kufa kwa Muhammad, inasimuliwa kwamba sio tu kwamba Muhammad aliongea na wanyama lakini wanyama wakishahadia imani kwake (Wakikiri imani yao kwake), vile vile, wakati Yesu alisema: “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti.” (Luka 19:40), Muhammad alisema “Natambua mawe katika Maka ambayo yalikuwa yakinisalimia kabla sijapewa utume na natambua hilo hata sasa” (Sahih Musilm).

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 04:44 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)