Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 015 (AXIOM 2: Belief in angels)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA TATU: NGUZO ZA IMANI

3.2. IMANI 2: Imani katika malaika


Nguzo ya pili kwa Waislamu ya Imani ni kuamini malaika, Wanaamini kwamba, ingawa Qur’an (21:31) inasema kwamba kila kitu kiliumbwa kwa maji “Malaika waliumbwa kwa mwanga, majini yaliumbwa kwa moto na Adam aliumbwa kwa udongo kama inavyobainishwa (ndani ya Qur’an) kwa maana wewe ( aliumbwa kutokana na udongo wa mfinyanzi)” (Sahih Muslim). Malaika wachache ndio wanaotajwa kwa majina ndani ya Qur’an, lakini kwa umoja wao wote, wanazuoni wa Kiislamu wanakubaliana kwa uchache sana juu ya malaika. Hata hivyo, ni ukweli ulio wazi kwamba Waislamu wanafahamu juu ya malaika kwa namna tofauti sana kabisa na ule wa Wakristo; japokuwa kuna baadhi ya matukio yanayosimuliwa kufanana, lakini kimsingi kuna mambo ya kina katika ujumbe na namna yao vinavyotofautiana kabisa. Mojawapo ya mambo yanayofanana ni malaika kupuliza tarumbeta siku ya hukumu kama ilivyo katika kitabu cha Ufunuo; Waislamu wanaamini kwamba malaika aitwaye Israafil kiuhalisia na wala sio lugha ya ishara-atapuliza tarumbeta mara tatu –kuashiria ufufuo wa wafu na mwanzo wa siku ya mwisho.

Malaika wachache wanatajwa ndani ya Qur’an. Jibril (Gabriel) anaheshimika kama miongoni mwa malaika wakuu wa daraja la kwanza. Anaitwa pia roho takatifu, malaika wa ufunuo, na malaika mwaminifu, ingawa kumbuka kwamba hii sio kusema yeye ana hadhi yoyote inayolingana na Roho Mtakatifu wa Biblia.

Baadhi ya malaika hawa waliotajwa kwa majina wana kazi maalumu, kama vile Malik ambaye kazi yake ni mlinzi wa kuzimu. Qur’an inasema:

“Na kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jehanamu. Hawatapumzishwa nayo na humo wataka tamaa. Wala sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu. Na watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe mola wako Mlezi! Naye atasema: Hakika nyinyi mtakaa humo humo.” (43:74- 77)

Malaika wengine wanatambulika kwa kazi zao sio kwa jina, ka ma vile malaika wanaobeba kiti cha enzi cha Allah na malaika wanaotoa roho kwa mtoto mchanga tumboni. Waislamu pia wanaamini kwamba kila mwanadamu amezungukwa na malaika wawili wanaoandika kila kumbukumbu ya kila tendo. Qur’an inasema:

“Wandishi wenye heshima, wanayajua mnayoytaenda.” (Qur’an 82:10-11)

Malaika mwingine wa muhimu katika Uislamu ni Iblis, ambayo miongoni mwa majina ambayo Qur’an inampa Shetani. Kwa kulingana na mafundisho ya Biblia, Iblis wa Qur’an ni malaika muasi. Hata hivyo, mazingira yaliyosababisha anguko lake ni tofauti. Qur’an (2:34 na kundelea) inasimulia jinsi ambavyo Iblis alifukuzwa kutoka peponi wakati ambapo malaika waliamuriwa kumsujudia Adam, Wote isipokuwa Iblis wakasujudu. Iblis alikataa na hivyo akaondolewa kutoka peponi- yeye pamoja na Adam na Hawa waliondolewa- Na Allah akatangaza kwamba daima kutakuwa na uadui baina yao.

Kulingana na wanazuoni wa Kiislamu, malaika ni viumbe walioumbwa kwa mwanga, wakifanya kile tu wanachoambiwa na kamwe hawawezi kumuasi Allah. Hii hata hivyo inatengeneza tatizo kidogo kwa maana Qur’an inasimulia malaika wakimpinga Mungu katika wazo lake kumuumba Adam (Qur’an 2:30).

Kabla ya kufunga sehemu hii, ninataka kwa ufupi kutaja aina nyingine ya viumbe katika Uislamu wanaoitwa Jinn. Hawa wana sura nzima inayowahusu inayoitwa kwa jina lao ndani ya Qur’an (Sura 72). Tofauti na malaika, baadhi ya majini wachache tu ndio wema, wengine ni waovu. Baadhi yao ni Waislamu; wengine wamepotoka kuacha Uislamu na hatma yao ni kuzimu. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaamini katika uwezekano wa kuoana baina ya jinni na mwanadamu lakini wanazuoni wengi wa Kiislamu wanapinga uhalali wake lakini hawapingi uwezekano wake. Matokeo yake, wanazuoni wa mahakama ya sharia za Kiislamu hawatambui mimba kama ndio ushahidi wa kufanya ngono nje ya ndoa (Zinah) kwa sababu inawezekana huyo mwanamke amefanya ngono na Jini bila kujua, au anaweza kiuhalisia ameolewa na jini mmojawao.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 04:31 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)