Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 018 (AXIOM 5: Belief in the Day of Judgement)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA TATU: NGUZO ZA IMANI

3.5. IMANI 5: Imani katika Siku ya Hukumu


Nguzo ya tano ya imani ni kuamini katika siku ya hukumu. Siku hiyo, wanadamu watagawanyika katika makundi matatu: moja litaenda peponi, lingine Kuzimu motoni, na la tatu litakuwa pahala pa kati kati inayoitwa al- Ar’af (Kutohoraishwa- nadharia inayotaka kufanana na ya Wakatholiki ya tohorani (purgatory)). Kutakuwa na uzio (Kizuizi) baina ya pepo na kuzimu motoni na pahala pa kati na inaelezwa kwa kirefu sana ndani ya Qur’an:

Allah atasema Ingieni motoni pamoja na uma zilizopita kabla yenu za majini na watu. Kila utakapoingia uma utawalaani wenzake. Mpaka watakapo kusanyika wote humo, wa miwsho wao watawasema wa mwanzo wao: Mole wetu mlezi! Hawa ndio waliotupoteza; basi wape adhabu ya motoni mara dufu. Atasema: Itakuwa kwenye nyote maradufu,lakini nyinyi hamjui tu. Na wale wa mwanzo wao watawaambia waa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyachuma. Hakika wale wanao zikanusha ishara zetu na wakazifanyia kiburi hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia peponi mpaka apite ngamia katika tundu la sindano. Na hivi ndivyo tunavyowalipa wakosefu. Jehanamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto kujifunika. Na hivi ndivyo tunavyowalipa madhalimu. Na wale wanaoamini na wakatenda mema- hatutamkalifishi mtu yoyote ila kwa kiasi cha uwezo wake- hao ndio watu wa peponi. Wao watadumu milele. Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iwe inapita mito. Na watasema” Alhamdulillah! Kuhimidiwa ni kwa Allah, ambaye aliyetuahidi kufikia haya. Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingelikuwa Allah hakutuahidi. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walileta haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo pepo mliyorithishwa kwa sababu ya mliyokuwa mkiyafanya. Na watu wa peponi watawanadia watu wa motoni: Sisi tumekuta aliyotuahidi Mole wetu Mlezi kuwa ni kweli. Je, nyinyi pia mmekuta aliyoakuahidini Mole wenu Mlezi kuwa kweli? Watasema: ndio! Basi mtangazaji atawatangazia: Laana ya Allah iwapate waliodhulumu. Wale waliokuwa wakizuilia Njia ya Allah na wakataka kuipotosha, nao wanaikanusha Akhera.Na baina ya makundi mawili hayo patakuwepo pazia. Na juu ya Mnyanyuko patakuwepo watu watakao wajua wote kwa alama zao,na wao watawaita watu wa peponi: Asalaam Alaykum, Amani juu yenu! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai. Na yanapogeuzwa macho yao kuelekea Motoni, watasema: Mola Mlezi wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu walio dhulumu. Na hao watu wa Mnyanyukoni watawaita watu wanao wajua kwa alama zao. Watasema: Kujumuika kwenu hakufaini kitu, wala hicho mlichokuwa mnafanya kiburi. Je, hawa sio wale mliokuwa mkiwaapia kuwa Allah hatawafikishia rehema. Ingieni Peponi, hapana khofu wala hamtahuzunika! Na wale wa Motoni watawaita watu wa Peponi! Tumiminieni maji, au chochote alicho kuruzukeni Allah. Nao watasema: Hakika Allah ameviharamisha hivyo kwa makafiri” (Qur’an 7:36-50)

Kueleza taswira hii isiyoeleweka, Waislamu wana mamia ya simulizi zinatoka kwa Muhammad juu ya undani wa pepo, kuzimu motoni na pahala pa kati. Muhammad alisema:

“Allah ndiye Mtukufu na aliye juu, amesema: Nimeandaa kwa ajili wateule wangu vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, hakuna sikio limewahi kusikia wala akili kuwahi kuwaza ispokuwa kwa sehemu ambayo Allah amewaambia” (Sahih Muslim) – Na hii bado imenukuliwa kutoka katika Wakorintho 2:9 na Isaya 64:4- na pia Muhammad alitoa taarifa nyingi kwa undani jinsi siku ya mwisho itakavyoanza. Watu --- “watakutana na Allah (wakati mtakuwa) miguu wazi, uchi, wakitembea kwa miguu na huku hawajatahiriwa” (Sahih Bukhari)

Basi baada ya kupuliza baragumu, mizani itawekwa kwa mujibu wa Qur’an:

“Basi itakapopulizwa baragumu, hautakuwepo na uhusiano baina yao siku hiyo, wala hawatauliza wao kwa wao. Na wale ambao mizani yao ni nzito (Kwa matendo mema), hao ndio wenye kufaulu. Lakini wale ambao mizani yao ni nyepesi- hao ndio walizitia hasarani nafsi zao, wamo katika Jahanamu, watadumu milele yote” (Qur’an 23:101-103)

Waislamu wanatofautiana kuhusu mizani hii kama ni halisi au ya sitiari (lugha ya mfano)

Baada ya hapo kutatokea daraja kati ya peponi na kuzimu. Muhammad anafafanua muundo wa jengo la daraja hilo kwamba:

Kisha Mwenye enzi atawajilia kwa sura tofauti na ile waliyomuona mwanzo, na atasema, “Mimi ni Mola wenu, na watasema, ‘Wewe ni Mola wetu’. Na hakuna atakayezungumza naye isipokuwa manabii tu, kisha itasemwa kwao “ je mnajua ishara yoyote mnayoweza kumtambua naye kwayo? Watasema, Sehemu ya juu ya goti, ambapo Allah atafunua shin yake (sehemu yake juu ya goti), kila muumini atasujudu mbele zake, na hapo watabaki waliokuwa wakisujudu mbele zake kwa ajili tu ya kujionyesha na ili kupata sifa njema. Mmoja kati yao atajaribu kusujudu lakini mgongo wake (mifupa) utakuwa mfupa mmoja (uti wa mgongo) (kama kipande kimoja cha mbao na hawataweza kusujudu). Kisha dajara litaletwa na kutandazwa kote kote kuzimu.”

Alipoulizwa kufafanua namna daraja hilo lilivyo, Muhammad alisema:

Ni daraja linaloteleza ambayo juu yake kuna nguzo na (kulabu kama vile) mbegu ya miiba ambayo ni pana upande mmoja na nyembamba upande mwingine yenye ncha kali zilizopinda. Mbegu kama hizo za miiba zinapatikana Najd na yanaitwa a-s’dan. Baadhi ya waumini watavuka daraja kwa haraka kama kukonyeza jicho wengine kwa kasi kama ya umeme, au kama upepo mkali, au farasi mwenye kasi au ngamia jike. Basi watakuwa salama bila madhara yoyote yale; baadhi watakuwa salama baada kupata michubuko, na wengine wataanguka chini kuzimu (motoni). Na mtu mwingine atavuka kana kwamba anaburuzwa (juu ya daraja),” (Sahih Bukhari)

Tukio linalofuatia ni:

Wakati watu wa peponi wakienda peponi, na watu wa motoni wakienda motoni, kifo kitaletwa na kuwekwa mbele ya pepo na moto. Kisha itachinjwa, na muitaji ataita: Enyi watu wa peponi,Kifo hakipo tena; Enyi watu wa motoni, Kifo hakipo tena; Kisha raha ya watu wa peponi itazidi na huzuni ya watu wa motoni itaongezeka.” (Sahih Muslim)

Haiwezekani kabisa kuweka mpangilio thabiti na ulio fasaha juu ya siku ya mwisho katika Uislamu, maana makusanyo sahihi za Haidth (i.e. ambazo zinaaminika kuwa sahihi zaidi na Waislamu wengi wa Sunni) hazikubaliani, na Wanazuoni wa Kiislamu pia hawakubaliani.

Kuna vitu vingi Waislamu wanaamini lazima vitokee kabla ya siku ya mwisho. Baadhi ya Waislamu wanasema kuna vitu kumi, kwa mjibu wa Hadith moja Muhammad alisema “ haitakuja kamwe hadi muone ishara kumi.” (Sahih Muslim). Aliendelea kutaja ishara:

  1. Moshi,
  2. al-Dajjal (Mpinga Kristo),
  3. Mnyama mwenye kuzungumza,
  4. Kuchomoza kwa jua mahali linapokuchwa,
  5. Kurudi kwa Isa mwana wa Mariamu (i.e.Kurudi kwa Yesu, ambaye ataoa kabla ya kufa),
  6. Ya’juj na Ma’juj (Gog na Magog),
  7. Maporomoko makubwa ya ardhi: moja mashariki, ya pili magharibi na nyingine katika Ghuba ya Uarabuni, na
  8. Moto utazuka kutoka Yemeni na kuwasukuma watu hadi mahali pao pa kukusanyika. (Sahih Muslim)

Taarifa kwa undani za kila mojawapo ya ishara hizi kumi zimetoelewa kupitia makusanyo ya Hadith mbali mbali na Maelezo ya ziada ya Qur’an, Lakini inaleta mkanganyiko namna ya kusoma kwa mpangilio. Nyingi katika hizo zinahusiana na ujio wa mara ya pili ya Kristo ambayo inapaswa kutokea kabla ya siku ya hukumu; kwa mujibu wa Uislamu atakuja kuvunja misalaba, kuuwa nguruwe, kuoa na kisha kufa na kuzikwa pembeni mwa kaburi la Muhammad.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 04:55 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)