Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 023 (PILLAR 3: Sawm (fasting))
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA PILI: FAHAMU IMANI NA MATENDO KATIKA UISLAMU
SURA YA NNE: NGUZO ZA UISLAMU

4.3. NGUZO 3: Sawm (kufunga)


Nguzo ya tatu ya Uislamu ni kufunga. Wakati wa mwandamo wa mwezi wa Ramadhan, katika mwezi wa tisa ya kalenda ya Kiislamu, kula, kunywa, na kufanya tendo la ndoa haviruhusiwi kuanzia mawio na machweo ya jua, Hii inaweza kuwa saa tisa za majira ya baridi hadi saa 15 za majira ya joto, hata hivyo hili utofautiana sana kwa kulingana na maeneo ya kijiogografia.

Kila Muislamu mtu mzima ambaye hana zuio la kidini anatakiwa kufunga. Dharura za haki zinajumuisha sababu za kiafya kama vile kisukari, pia na sababu zingine zinazohitaji matibabu yanayopitia kinywa, Kunyonyesha ambapo kufunga kutahatarisha afya ya mama au yaya wake, mimba,na kadhalika. Ingawa Waislamu hawatakiwi kufunga kama wana dharura za haki, lakini wanazuoni wengi wanawashauri Wasilamu kuendelea mbele na kufunga kama wanaweza, hata kama kiuhalisia walitakiwa kutokufunga.

Kuna mazingira ambayo kufunga kumeharamishwa; Waislamu wanawake wameharamishwa kufunga wakiwa katika hedhi, kwa mfano, kama watafunga basi haitahesabika kama funga, ingawa wanaweza kulipa funga baadaye wakimaliza siku za hedhi. Watu wengine ambao inakubalika kwao kutukufunga ni wanajeshi walioko vitani na wasafiri. Wasiofunga wanapaswa kulipia siku walizokosa kufunga baada ya mwezi wa Ramadhan na punde mazingira yaliyosababisha wasifunge yatakapobadilika, kabla ya Ramadhan nyingine. Ikiwa mazigira yanayosababisha kutokufunga kwao ni ya kudumu, au haijabadilika hadi Ramadhan nyingine, basi Musilamu anapaswa kulipia funga hiyo kwa kumlisha mwenye kuhitaji kwa kulingana na idadi ya siku alizokosa kufunga.

Ikiwa Muislamu hatafunga, au akavunja kufunga bila dharura ya halali kwa kula, kunywa kwa makusudi au kufanya tendo la ndoa wakati wa mchana katika mwezi wa Ramadhan, basi watachukuliwa kama wakosefu na watatakiwa kulipia kosa lao kwa kufunga siku sitini mfululizo kwa kila siku waliokosa kufunga au kwa kumwachia huru mtumwa au kuwalisha watu sitini wenye kuhitaji (Sahih Muslim, 2599).

Funga ya namna hii pia inatumika nje ya Ramadhan kuashiria majuto au kulipia dhambi. Kwa mfano, ikiwa Muislamu atavunja kiapo basi watatakiwa kufunga kwa siku tatu (Qur’an 5:89), Kumuua Muislamu mwenzake kwa bahati mbaya basi atatakiwa kufunga kwa siku sitini (Qur’an 4:92), na kutangua talaka itatakiwa kufunga kwa siku sitini (Qur’an 58:2-4).

Siku hizi, Ramadhan imechukua mkondo wa sherehe za mwezi mzima katika jamii nyingi za Kiislamu.Vitu vingi vya kufurahisha, bei ya vyakula hupanda mwezi huu. Na katika nchi nyingi za Kiislamu, saa za kazi hufupishwa, na shughuli nyingi zinahama kutoka kufanywa mchana na kufanywa usiku. Katika baadhi ya nchi, mighahawa yote hufungwa wakati wa mchana, na nchi zingine zina sheria za kuadhibu yoyote anayekula na kunywa hadharani bila kujali ni Muislamu au la, au kwamba wana dharura ya kidini ya kutokufunga au la. Adhabu hutofautiana kwa wengine wanalipa faini kama ilivyo katika nchi ya Brunei, hadi kifungo cha gereza kama ilivyo katika nchi ya Pakistan. Sheria kama hizo hazina misingi kutoka katika vyanzo vya Kiislamu, Ingawa na katika yote, zinalenga unafiki maana sheria hizo zinakaza sana hali ya kuonekana hadharani ya kwamba kila mtu amefunga.

Wakati wa Ramadhan, Waislamu wanakuwa na hasira na ghadhabu za ghafla, hasa katika mazingira ya joto- kitu ambacho ni kitendawili maana lengo kuu la funga hii ni kulea au kuzidisha hali ya utakatifu na kujidhibiti. Kufunga imekuwa zaidi ni jambo la desturi ya kijamii kuliko tendo la kidini kwa wengi. Katika baadhi ya nchi za kiislamu, sheria za Ramadhan zimekuwa za upuuzi na hazina maana inayoweza kuleta hadhi kwa yoyote Yule. Kwa mfano, wakati wa Ramadhani huko Misri hairuhusiwi kumuuzia kilevi raia wa Misri bila kujali kama ni Muislamu au la (Misri ina kiwango cha juu ya idadi ya Wakristo japo kuwa kwa takwimu ya idadi ya watu ni wachache), Lakini eti inaruhusiwa kuwauzia wageni wasio raia wa Misri bila kujali dini zao. Hivyo Mkristo raia wa Misri wakati wakipata chakula pamoja na raia wa Saudi Arabia ambaye ni Muislamu wakati wa Ramadhan; Mkristo atazuiwa bia, huku Muislamu wa Saudia atauziwa. Katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), sheria zimekuwa zikibadilika kila mwaka. Kwa miaka ya hivi karibuni Kunywa kilevi imeruhusiwa kwenye mighahawa na kumbi za starehe za usiku lakini eti kupiga muziki kumekatazwa. Kama ambavyo unaweza kuwa unajua, hakuna kitu maalumu cha kukataza kilevi wakati wa mwezi wa Ramadhan kwa sababu kutumia kilevi ni haramu miezi yote ya mwaka mzima; makatazo na sheria namna hii zinawekwa na serekali ili kuridhisha hisia za kidini za wananchi kuliko uhalisi wa kufuata imani ya Kiislamu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 09, 2024, at 06:04 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)