Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 028 (CHAPTER SIX: CHRIST IN ISLAM)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TATU: FAHAMU KRISTO MUISLAMU

SURA YA SITA: KRISTO KATIKA UISLAMU


Uislamu unamtambua Kristo kama mmojawapo wa Manabii wakuu watano. Jina lake kwa kiarabu katika Uislamu ni Isa, ambayo inawezekana imetokana na jina la Kiyunani kuliko Kiebrania au Kiaramaiki. Kwa upande mwingine Wakristo Warabu wanamuita Yasuu inayotokana na Jina lake kwa Kiebrania Yeshu’a. kulingana na Uislamu kristo ni Kiumbe wa kawaida, Mtume (nabii aliyeleta ujumbe wa Mungu, Injili kama ilivyoonyeshwa juu) kwa wana wa Israel na aliyetabiri ujio wa Muhammad. Qur’an inamuita kama Al-Masihi Isa (Masihi au- Kristo -Yesu) au Mwana ya Mariamu. Katika kitabu hiki natumia cheo cha Kristo ambayo Wakristo na Waislamu humuita hivyo na napenda kwamba wewe pia utahitajika kufanya hivvyo katika mazungumzo ya awali na Waislamu kwa ajili ya kuepuka kutumia jina ambayo Wakristo Waarabu hawaitumii na pia kuepuka jina lenye utata Kitheolojia huku kutokutumia Jina ambalo Waislamu wanalipinga. Kutumia jina linalokubalika pande zote linaweza kusaidia mazungumzo kuendelea Ingawa (Kama itakavyoonekana wazi kwenye mjadala ) hatukubali kwamba Kristo wa Kiislamu ni huyo huyo Kristo wa Biblia.

Biblia inamtaja Kwetu Kristo kama Mungu aliyetwaa utu, Mwokozi, Mkombozi. Na hakuna mahala popote –katika Agano la kale au Jipya- ambapo Biblia inamtaja kama mwanadamu wa kawaida tu; Yeye ni wa kuabudiwa, Ndiye wa kuokoa watu wake. Mtheolojia C.S. Lewis anavyotuonyesha hoja hii katika kitabu chake cha Mere Christianity:

"Ninajaribu kuzuia jambo la kijinga ambalo watu husema mara kwa mara juu yake: Nipo tayari kumkubali Yesu kama Mwalimu mzuri wa maadili lakini Sikubaliani na madai yake kwamba yeye ni Mungu.. Hilo ni jambo moja ambalo hatuwezi kusema. Mwanadamu wa kawaida tu ambaye atasema maneno aliyoyasema Yesu hawezi kuwa mwalimu mkuu wa maadili. Atakuwa aidha ni mwendawazimu- kwa kiwango ambacho cha mtu kusema yeye ni yai iliyopigwa- ni Shetani kabisa wa kuzimu. Lazima ufanye maamuzi kwamba aidha huyu mtu alikuwa- na ni –Mwana wa Mungu ama kichaa au jambo lingine baya zaidi. Unaweza kumkemea kama mjinga au kumtemea mate kama mjinga na kumuua kama jini au kuanguka miguuni pake na kumuita Bwana na Mungu, laakini tusije na wala kuunga mkono upuuzi wa yeye kuwa mwalimu mkuu aliye mwanadamu tu. Yeye hajaacha hilo dai kuwa wazi kwetu, na hakudhamiria yeye kujulikana hivyo pia."

Kama Lewis anavyosema, mtazamo wa Kristo kuwa binadamu wa kawaida aliye mwalimu ni kuunga mkono upuuzi, ambayo sio jambo la wazi kwetu, Lakini bado hivi ndivyo Waislamu wanavyomuona Kristo. Uislamu unamuona Kristo kama mmojawapo wa manabii wakuu, mtenda miujiza, mwalimu mkuu, asiye na dhambi lakini ni mwanadamu wa kawaida tu. Uislamu unapinga ukuhani wa Kristo, Kusulubiwa kwake, Uungu wake. Hili tu inatosha kuzifanya Biblia na Qur’an kupingana kabisa, lakini Kristo katika Uislamu ni mada iliyo ngumu inayotoa nafasi ndogo ngumu sana kufikia hitimisho ya muafaka.

Kristo ametajwa katika Qur’an zaidi ya mara 90, na kila tunapomzumgumzia Kristo mawazo ya Waislamu yatakuwa kama ilivyoonnyeshwa hapo juu. Kwa Waislamu, Qur’an saa zote inakuwa sahihi bila kujali inapingana na nini. Muislamu mmoja msomi aliwahi kuniambia kwamba kama kuna aya katika Qur’an inayopingana na mantiki, sayansi, uzoefu binafsi, uthibitisho wa Kisayansi, historia, ataendelea kuamini hiyo aya ya Qur’an na kukataa hayo mengine. Hii inamaanisha kila kunapotokea kupingana kati ya Kristo katika Uislamu na Kristo wa Biblia, Waislamu watakataa moja kwa moja mtazamo wa Kibiblia.

Kwa Jinsi gani Uislamu unamtazama Kristo? Bila kujali ukweli kwamba Uislamu unapinga nafsi ya Kristo kama inavyoelezwa katika Biblia. Lakini Qur’an imempa hadhi Kristo na tabia ambazo hajapewa yoyote ikijumuisha na Muhammad mwenyewe. Ingawa baadhi ya vitu anavyopewa Kristo pia wamepewa manabii wengine- kama vile miujiza, kama Qur’an inavyotoa kwa Musa pia- lakini Kristo ametengwa kwa kuwa na hizo sifa zote kwa pamoja. Sura hii itatazama njia tisa ambazo Kristo anatajwa kwa kutofautiana kabisa na manabii wengine katika Uislamu. Kisha sura mbili zinazofuata zitaangazia zaidi kwa undani Miujiza ya kristo inavyoelezwa ndani ya Qur’an, na kisha Uislamu kupinga asili ya uungu wa Kristo.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 12:18 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)