Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 075 (Has the Qur'an been perfectly preserved?)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
13.1. Imani juu ya kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili

13.1.5. Je Qur’an imehifadhiwa kwa ukamilifu?


Kuhifadhiwa kwa Qur’an ni madai mengine ya uongo ambayo vyanzo vyenyewe vya Kiislamu vinaikanusha. Tunakuta katika vyanzo vingi vya Kiislamu kwamba sehemu za Qur’an ya kwanza zilipotea. Kwa mfano Qurtbi katika mafafanuzi yake anaandika:

“Aisha anasimulia: ‘Sura Ahzab ilikuwa na aya 200 wakati wa uhai wa Mtume lakini wakati Qur’an ilipokusanywa tulikuta kiasi ambacho kinaweza kupatikana tu katika Qur’an ya sasa (ambayo ina aya 73),” (Qurtubi, Mafafanuzi ya Qur’an juu ya Sura Ahzab).

Waislamu wanatoa mfano mwingine wa mabadiliko katika Qur’an katika Hadith ifuatayo:

“Umar b. Khattab aliketi katika Mimbari ya Mtume wa Allah na kusema: Hakika Allah alimtuma mtume na ukweli, na akatuma chini pamoja naye kitabu, na ndani yake aya ya kupigwa kwa mawe ilijumuishwa katika aliyoshushiwa chini. Tuliisoma na kuitunza katika kumbukumbu zetu na tuliifahamu. Mtume wa Allah aliruhusu adhabu ya kupigwa mawe hadi kufa ( Kwa wana ndoa wazinzi) na, baada yake sisi pia tulitoa adhabu hiyo ya kupigwa mawe, Ninaogopa kwamba mda unavyozidi kuyoyoma, watu (Wanaweza kusahau) nakusema : Hatuoni adhabu ya kupigwa mawe katika kitabu cha Allah, na hivyo kupotea kwa kuacha wajibu ulioelezwa na Allah. Kupigwa mawe ni wajibu uliotandazwa chini katika kitabu cha Allah kwa walio katika ndoa wanaume na wanawake wanaofanya zinaa pale ukweli unapobainika, kama kuna mimba, au kuna kukiri (wa hatiya)” (Sahih Muslim)

Na kumbukumbu ya badiliko la tatu katika Qur’an kama ilivyotunzwa na kusimuliwa na Ibn Maja, aliyesema kwamba mke wa Muhammad Aisha alisema:

“Aya ya kupigwa mawe na kumnyonyesha mtu mzima mara kumi ilifunulwa na karatasi ilikuwa pamoja nami chini ya mto wangu. Mtume wa Allah alipokufa, Tulitingwa na kifo chake, na akaja kondoo wa kufugwa na kuila” (Sunan Ibn Majah)

Hivi ni vyanzo vitatu miongoni mwa vingi vinavyoashiria kwamba madai ya kuhifadhiwa kwa Qur’an ni uongo mwingine unaoaminiwa na Waislamu wengi lakini hauungwi mkono na vyanzo vya Kiislamu.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:22 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)