Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 076 (Is the Qur’an superior to other scriptures because they all have been changed, while the Qur’an alone has been preserved?)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
13.1. Imani juu ya kutunzwa kwa Qur’an na kuharibiwa kwa Biblia ya asili

13.1.6. Je Qur’an ni ya juu na bora zaidi kuliko maandiko matakatifu mengine maana mengine yote yamebadilishwa, huku Qur’an pekee imehifadhiwa?


Madai haya kwamba Qur’an ni ya juu na bora zaidi kuliko maandiko mengine matakatifu na kwamba mengine yote yamebadilishwa kwa udogo ni madai tofauti kwa sababu ni laumu juu ya kuharibika kwa maandishi ya vitabu kwa kiwango ambacho hatuwezi kujua tena hivi vitabu vilikuwa vinasema nini mwanzo kwa asili. Madai haya hayaungwi mkono kivyovyote na ushahidi wa Maandishi ya kale, Maanidko ya Biblia, au hata na ya Qur’an. Biblia kwa uwazi inaweka kuhifadhiwa kwa neno Mungu katika mikono ya Mungu mwenyewe na sio kwa wanadamu:

“Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno ya Mungu wetu litasimama milele” (Isaya 40:8).
“Kwa maana naangalia neno langu ili nilitimize” (Yeremia 1:12)

Daudi anasema katika Zaburi:

“E Bwana, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele” ( Zaburi 119:89)

Kristo anasema katika Injili:

“Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie.” (Mathayo 5:18)
“Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”. (Mathayo 24:35)
“Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.” (1 Petro 1:25)

Pia tuna onyo la wazi kutoka kwa Mungu kwa watu wake:

“Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri Na hukumu niwafundishazo, Ili mzitende; mpate kuishi Na kuingia Na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wa baba zenu. Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu, niwaamuruzo” (KumbuKumbu 4:1-2)

Na onyo hili limerudiwa katika kitabu cha Ufunuo:

“Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki” (Ufunuo 22:18-19)

Pamoja na ahadi zote hizi na maonyo haya, hakuna namna mwamini angeweza hata kutafakari wazo ya kubadilisha neno moja na kama Muislamu akisema walioibadilisha hawakuwa waamini, halafu Waamini wangewezaje kuruhusu itokee bila kufanya lolote juu yake? Kinachoshangaza hapa Qur’an yenyewe haidai kubadilishwa kwa maandishi ya Biblia. Kinyume chake Qur’an inasema:

“Hakika sisi tuliteremsha Taurati yenye wongofu ndani yake na nuru, ambayo kwayo manabii walio wanyenyekevu na wacha Mungu Waliwahukumu Wayahudi, ndivyo walivyofanya wakuu na marabi wao kwani walikabidhiwa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake, Basi msiowaogope watu bali niogopeni mimi.Wala msibadilishe aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa kwa aliyoyateremsha Allah, basi hao ndio makafiri. Na humo tuliwaandikia ya kwamba roho kwa roho, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio na jino kwa jino kwa majeraha ya kisasi. Lakini atakayesamehe basi itakuwa ni kafara kwake. Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Allah, basi hao ndio madhalimu.Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati. Na tukampa Injili iliyomo ndani yake wongofu na nuru inayosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati na wongofu na mawaidha kwa wacha Mungu. Na wahukumu watu wa Injili kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyoyateremsha Mungu ndani yake basi hao ndio wapotofu. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, kitabu hiki kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika vitabu ili kuyalinda. Basi hukumu baina yao Kwa aliyokuteremshia Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha haki iliyokujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemuwekea sheria yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka angewafanyeni nyote uma mmoja. Lakini ili kukujaribuni kwa aliyokupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, naye atakuja kuwaambieni yale mliokuwa mkihitalifiana” (Qur’an 5:44-48, Tafsiri ya Arberry).

Tunagundua vitu vichache katika sehemu hii ya Qur’an:

  • Kulingana na Qur’an Allah ametuma Torati na Injili ambamo ndani yake kuna muongozo na nuru.
  • Ilitolewa kwa manabii, wakuu na marabi kuitunza.
  • Kristo amethibitisha Torati iliyokuja kabla yake.
  • Wote, Wayahudi na Wakristo wanaombwa kuhukumu kulingana na yale waliopewa.
  • Qur’an inaithibitisha Injili na inasema inailinda.
  • Maneno ambayo Arberry anayatafsiri kama “ndani yake kuna muongozo na nuru” kiukweli yana utata katika Kiarabu kulingana muundo wa maneno (Kiukweli maneno yenyewe hayana kitenzi). Hata hivyo, katika kujaribu kwamba hilo huwenda lilikuwa la kweli zamani, Injili kwa sasa imeharibiwa. Baadhi tafsiri za kisasa za Kiislamu zinasema “ Ndani mwake ilikuwa na mwongozo na nuru au ndani mwake kulikuwa na muongozo na nuru kwamba zilikuwepo lakini kwa sasa hazipo tena tafsiri ambayo haiungwi mkono kivyovyote na maneno ya Kiarabu yaliyotumika. Hata kama tukichukua tafsiri ya nyuma bado haiifanyi aya kuwa imara au thabiti. Kulingana na maneno ya Qur’an, Kristo alithibitisha yaliyokuwa kabla yake, na Muhammad akathibitisha yaliyokuwa kabla yake, kama tuna maandiko yoyote kutoka wakati wa Muhammad au Kristo basi tuna maandiko yaliyothibitishwa. Kama maandiko wakati wa Muhammad hayakuwa sahihi, basi madai ya Qur’an ya kuthibitisha ni uongo na pia inamaanisha kwamba Qur’an ilishindwa kulinda maandiko matakatifu. Kwa sasa tunayo Biblia kabla ya Kristo kwenye magombo ya bahari mfu makumi ya maelfu ya maandishi ya Biblia katika makala za zamani kabla ya Muhammad

Katika hatua hii Waislamu kwa kawaida huonyesha baadhi tofauti za maandiko na kudai kwamba zinathibitisha hoja zao, lakini hiyo sio sababu kivyovyote. Kuna tofauti ya kuwa na tofauti katika maandiko na kutokuelewa kinchochesemwa na maandiko husika. Kwa mfano, Tukisema “Yesu Kristo” na “Kristo Yesu” hiyo itahesabika kama tofauti lakini hakuna anayefikiri eti kwamba hatujui kinachosemwa. Na zaidi Qur’an Inawataka wayahudi na Wakristo kuhukumu kulingana na walivyo navyo. Inakuwaje sasa Qur’an kuwataka wahukumu kwa kutumia kitabu ambacho inasadikiwa kwamba kimeharibika? Tunasoma mahali kwengine ndani ya Qur’an:

“hatukutuma kabla yako ( Muhammadd) ila ni wanaume ambao tuliowapa wah’yi (ufunuo), Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui” (Qur’an 16:43)

Qur’an hivyo inawaambia watu kuwauliza Wayahudi na Wakristo juu ya mambo ambayo hawajui. Inamwambia hata Muhammad kuwauliza kama ana shaka:

“Na ikiwa una shaka katika yale tuliyokuteremshia, basi waulize wasomao kitabu kabla yako” (Qur’an 10:94)

Je tunapaswa kuamini kwamba Qur’an inamwambia Muhammad awaulize watu wa kitabu (Wayahudi na Wakristo) kama anayo shaka na wakati huo huo inawashutumu kwa uharibifu?

Siko hapa kujaribu kuthibitisha ukweli wa Biblia kutoka kwenye Qur’an, Najaribu kutofautisha kile kinachodaiwa na Uislamu kwenye kumbukumbu zao za asili za mwanzo na kile wanachoamini kwa ujumla wao. Jambo geni ni kwamba shutuma hizi ziliibuka miaka mamia baada ya kifo cha Muhammad. Uislamu wa Mwanzo na Waislamu waliwalaumu Wayahudi kuchukua maneno nje ya maudhui yake kwa kupindisha ndimi zao ili kufanyia mazaha dini ya kweli (Qur’an 4:46).Hawakudai kwamba Wayahudi walibadilisha maandiko yenyewe. Hii sio dai ambayo inadaiwa leo, na hata hivyo hii ni kawaida katika maandiko yoyote yale; ambapo kwa sababu yoyote ile unakutana na mtu anajaribu kupotosha maana halisi ya maandiko, Jibu ni kusoma maandiko yenyewe ili kupata maana yake halisi. Hii inafanywa na wote Waislamu na Wakristo Wazushi na baadhi ya madhehebu. Lakini kubadilisha kinachosemwa na maandiko hii haipatikani popote kwenye vyanzo vya asili vya Kiislamu.Qur’an haisemi kwamba Wayahudi na Wakristo waliandika chini chochote kile ndani ya vitabu vyao mambo ambayo hayajafunuliwa na Allah; inachokisema ni kwamba walitunza siri (Qur’an 2:77) na kuficha ushuhuda (Qur’an 2:140),wakapindisha kitabu kwa ndimi zao (Qur’an 3:78), na wakasahau sehemu ya ujumbe (Qur’an 5:13). Hivyo tunaona kwamba Qur’an haiwashitaki Wayahudi na Wakristo kwa kubadilisha na kuharibu maandiko yao bali katika kutamka kwa kinywa au kwenye kutafsiri lakini sio Maandiko yenyewe. Hata wanazuoni wa Kiislamu wanakubaliana na hili. Kwa mfano, Ar-Razi anaandika:

“Kubadilisha ina maanisha kutafisri isivyo sawa maandiko, kutumia tafsiri ya uongo, kuchukua maneno kinyume na nje ya maudhui, kuchukua neno nje ya maana yake ya kweli,Na ndio kitu kilekile wazushi wanafanya na hii ndio maana sahihi ya kuharibu.”

Shutuma za kuharibu maandiko bila ushahidi hayawezi hata kupewa uzito au kuchukuliwa kwa umakini. Sio shutuma kinyume na Biblia tu kama Waislamu wanavyoweza kufikiri, bali ni kinyume na Qur’an pia, maana Qur’an inadai:

“Hakuna mtu anayeweza kubadilisha maneno ya Mungu” (Qur’an 6:34),

Na Qur’an inadai kwamba Biblia kama ilivyofunuliwa ilikuwa hasa neno la Mungu! Na Qur’an kama tulivyoona, inasema kwamba ilitumwa kama mlinzi wa vitabu (5:48), inayomaanisha:

  1. Allah alishindwa kuilinda.
  2. Wayahudi na Wakristo waliweza kuharibu maneno ya Allah na hakuweza kufanya lolote juu yake.
  3. Muhammad alishindwa kutunza hata nakala moja ya Biblia ambayo ilikuwepo wakati wake kama tunavyoambiwa katika hadith: “Kundi la Wayahudi walikuja na kumualika Mtume wa Allah kwenda Quff. Hivyo akawatembelea katika shule yao. Wakamwambia: Baba yake Qasim, mmoja kati yetu amezini na mwanamke; hvyo toa hukumu juu yao. Hivyo wakamtolea mto ambapo Mtume wa Allah akakaa juu yake na kusema: Leteni Torati. Ikaletwa. Kisha akatoa mto pembeni yake na kuweka Torati juu yake kisha kusema: “Ninaamini katika wewe na kwa Yule aliyekufunua” (Sunan Abi Dawud ‒ 4449).
  4. Waislamu baada ya Muhammad walishindwa kutunza nakala ya Kitabu ambacho kilikuwa kinapatikana wakati wao na ambacho Muhammad alikiapia.

Kimsingi shutuma hii inaweka lawama kwa kila mmoja. Pia inahitaji baadhi ya maswali kujadiliwa, kwa kutaja tu, Lini dai la kuharibiwa kwa Biblia ilitokea? Ngoja na tuangalie kwanza swali la Kwanza. Na hapa tuna mambo yanayowezekana matatu:

  1. Katika wakati wa kuandikwa kwake- Ikimaanisha kwamba Wakati wa Musa na Yesu. Uwezekano huo unaangamiza dhana ya uabii katika Uislamu maana inakubali kwamba manabii wenyewe hawakuwa watu wa kuaminika (Kama Uislamu unavyofundisha). Inamaanisha pia kwamba Allah alishindwa kmchagua hata nabii mmoja wa kuaminika, na Qur’an ni kitabu cha uongo kwa kudai kwamba manabii hawakuwa na dhambi na pia walikuwa watu wa kuaminika.
  2. Kitabu kilibadilishwa wakati fulani kati ya Yesu na Muhammad. Chaguo hili pia haiwezi kusimama katika uchunguzi maana tunazo nakala maelfu kutoka wakati huo na tuna magombo ya bahari mfu yenye tarehe za Kabla ya Yesu. Inamaanisha pia kwamba Muhammad na Waislamu walishindwa kufanya waliyopewa na Qur’an kulinda maandiko.
  3. Ilitokea baada ya Muhammad. Tena haiwezi kufanya kazi kwa Sababu zile zile: Uwepo wa maandishi, uwepo wa tafsiri kuto Ka lugha mbali mbali.

Chaguo pekee liliopo ni kwamba kuharibiwa kwa maandiko haikuwahi kutokea, maana haiungwi mkono na ushahidi na inapingwa na ushahidi ulio mwingi kinyume chake.

Sasa na tuzingatie swali kwamba nani anayetarajiwa kwamba alibadilisha Biblia. Uislamu hautoi jibu kwa jambo hili, hivyo ngoja tuangalie uwezekano.

a) Wayahudi: Kama Wayahudi walibadilisha maandiko kwa ajili kukana au kubadilisha unabii wa Yesu au Muhammad, kwa nini Wakristo wa karne ya kwanza hawakusema chochote kuhusu hilo? Kinyume chake Wakristo waliwashutumu Wayahudi kwa mambo mengi sana lakini la kubadilisha maandiko sio moja yao: Mtume Paulo anasema:

“Ambao ni Waisrael, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa Torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake.” (Warumi 9:4)

Kanisa la kwanza lilitegemea Agano la kale. Kristo aliposema:

“Mwayachunguza maandiko,kwa sababu mnadhanikwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndio yanayonishuhudia.” (Yohana 5:39),

alikuwa akiongelea juu ya Agano la Kale. Na aliposema Petro:

“Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi” (2 Petro 1:19),

alikuwa akiongelea juu ya Agano la kale; Alipoandika Luka:

“Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayanchunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.” (Matendo 17:11),

alikuwa akiongelea juu ya Agano Kale.Kwa kweli ambapo Agano Jipya inaongea kuhusu Maandiko, mara zote huongelea Agano la Kale. Na bado tuna unabii mia tatu katika Agano la Kale juu ya Kristo; Wayahudi wanakanusha maana ya maandiko haya au wanajaribu kuyafafanua vinginevyo lakini bado yamo katika kitabu chao.

Mwisho kama wayahudi walibadilisha kitabu chao kwa nini waliacha matendo ya aibu ya baba zao wa zamani ndani yake? Linganisha unachosoma katika Agano la Kale na unachosoma kuhusu Muhammad katika maandishi ya Kiislamu, na utaona tofauti. Waandishi wa KIislamu wanajaribu kwa nguvu kukana au kuondoa chochote kinachoweza kuaibisha na kusisitiza sifa na kusitahili kwa matendo kwa kiwango cha kuremba. Kwa nini Wayahudi wasingefanya hivyo hivyo kwa kulinganisha na yale yaliyoandikwa katika Biblia juu ya dhambi za manabii na maovu ya wafalme ya Yuda na Samaria?

b) Wakristo: Labda Wakristo walibadilisha Biblia. Lakini kama ndivyo, kwa jinsi gani Wakristo na Wayahudi wawe na Agano la kale ile ile moja huku ingawa wanatofautiana maana yake? Na kama walifanya, Kwa nini Wayahudi wa karne ya kwanza wasingewaumbua na kuua dini mpya katika uchanga wake? Walifanya hiyo katika lugha gani? Katika Kiebrania, Kiaramaiki au Kiyunani? Inakuwaje maandiko yaliyokuwepo kabla ya Ukristo yanakubaliana na yale tuliyo nayo baada?

c) Wote: Labda wote Wayahudi na Wakristo walifanya hivyo kwa pamoja. Sawa, ni lini walipatana kufanya hivyo je ni kabla ya Ukristo kuanza? Hiyo haiwezekani, kwa sababu tunayo karibia Agano la Kale lote zenye tarehe za miaka ya mamia kabla Ukristo kuanza katika magombo ya bahari mfu. Kwanini Himaya ya Rumi haikuwaumbua Wayahudi na Wakirsto na hivyo kumalizana na maadui wake wote kwa pamoja?

d) Mataifa yote ya dunia: Hii kimsingi ndio uwezekano pekee unaobaki kama tutakubaliana na Waislamu kwamba maandiko ya Biblia yalibadilishwa kwa kiwango ambacho hatuwezi kujua nini kilikuwemo ndani yake kwa asili. Kila taifa duniani kabla ya Uislamu na kwa lugha zote popote yalipokuwa walikuwa na nakala ya Biblia na hivyo yalikubaliana kubadilsha baadhi ya aya ya kitabu cha Wayahudi na ya vitabu vya Wakristo na kuongeza baadhi ya aya, ili kumkana nabii atakayekuja karne nyingi zijazo. Walipaswa kukubaliana kuandika upya maandiko ya kale na tafsiri zake, wachome vitabu halisi vya asili, kisha wasiandike au kusema neno lolote kuhusu walichokifanya. Uwezekano huo wa kipuuzi ndio pekee waliobaki nao Waislamu, na sababu ya wao kufikiria hivyo ni kwa sababu ndivyo hasa alivyofanya Uthman na Qur’an kama tulivyoona juu.

Hivyo basi kwa sababu hiyo ndio historia ya Qur’an, Waislamu wanafikiri ndivyo ilivyo pia kwa vitabu vingine. Lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya Qur’an na Biblia.

  1. Qur’an ni lugha moja, imeandikwa kwa miaka 23 mahali pamoja na mtu mmoja. Biblia kinyume chake iliandikwa zaidi ya miaka 2000 na watu arobaini kwa lugha tatu na katika mabara zaidi ya tatu.
  2. Qur’an ni kitabu kinachohusu jamii moja ya watu (Waislamu), ambapo Biblia inahusu jamii ya watu tofauti ambao hawaku- kubaliani kila mmoja kuhusu maana yake wala ni nini.

Mwisho, ingawa tunakubaliana na Waislamu juu ya hitaji ya kuwa na Maandiko yasio na makosa, Haileti maana kwamba Uislamu unafundisha kutenguliwa kwa dini zingine. Basi hata Kama tuna Maandiko halisi ya asili, Bado Waislamu wangedai (Kama wanavyofanya) kwamba ilitenguliwa (Kufutwa na kubadilishwa) na Qur’an.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:37 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)