Grace and Truth

This website is under construction !

Search in "Kiswahili":

Home -- Kiswahili -- 01. Conversation -- 2 Muslims Differ

This page in: -- Albanian -- Arabic? -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- German? -- Greek -- Hausa -- Igbo -- Indonesian -- Kirundi -- KISWAHILI -- Russian -- Somali -- Spanish -- Telugu -- Ukrainian -- Uzbek -- Yoruba

Previous booklet -- Next booklet

01. Mazungumzo na Waislamu kuhusu Kristo

2 - SI KILA MUISLAMU ANAAMINI NA TUFIKIRI SAWA

Unapowafikia Waislamu, ni vyema kufahamu kuwa Waislamu wanaweza kutofautiana sana wao kwa wao. Kuwa na ufahamu kuhusu makundi mbalimbali muhimu ya Waislamu unaoweza kukutana nao kutakusaidia kujiandaa ili kuwasiliana na mtu sahihi kwa wakati sahihi.



2.01 -- Si Kila Muislamu Anaamini Na Tufikiri Sawa

2.02 -- Maendeleo ya kihistoria na uhalisia wa kivitendo

Mtu anayetaka kufahamu mawazo ya ki-islamu, ni vizuri atambue maendeleo ya ki-historia katika maeneo walipoishi Wayahudi na makanisa ya kikristo kwenye bara Arabu na katika nchi zinazozunguka Bahari ya Kati. Uislamu haukutokea hivi hivikutoka hewani, bali uliendelezwa kutokana na mahusiano na wapagani, Wayahudi na Wakristo.

2.03 -- Wayahudi na Wakristo nyakati kabla ya Mhammad

Wayahudi walikuwa wametawanywa pande zote kutokana na utawala wa nguvu wa Rumi katika maeneo mbali mbali ya Siria na mizunguko yake, pia waliuzwa kwenye utumwa walipokan­damizwa baada ya maasi yao miaka 70 na 132/135 baada ya Kristo (B.K.). Jamii za Kiyahudi zilianzishwa katika Asia ndogo, nchi ya Iraki, kwenye bara ya Arabuni, katika Misri, pia na Rumi penyewe.

Kwenye mawimbi ya vita zilizoendelea kati ya nchi za Bahari ya Kati na dola zingine tokea Asia, Wayahudi walioishi mashariki ya jangwa la Siria walipiga vita upande wa Sassanidi dhidi ya Warumi. Kwa msaada wa washirika wao walisimamisha ufalme wa Kiyahudi nchini Yemeni ya kusini, ambapo manemane na ubani zinapandwa; walifanya hivyo kujilinda na ushawishi wa kikristo wa himaya ya Iskanderia ya zamani (Byzantine).

Baada ya Warumi kutawanya maasi ya kiyahudi kule Yerusale­mu na Dameski, Makanisa ya Kikristo yalikusanyika hasa katika miji ya Alexandria, Antiokia, Efeso, Rumi, Edesa na baadaye pia Konstantinopoli. Walieneza Injili Mesopotania, Kushi, Afrika ya kaskazini na Asia ya kati. Wakopti (wananchi wa kushi) walianza kupeleka Injili nchi ya Yemeni ya kaskazini na walijenga ufalme wa Kikristo kwa muda wa miaka makumi kadhaa wakiwa na uaskofu katika Wadi Nadjran. Vita kali zililipuka kati ya ufalme wa kiyahudi kule Yemeni ya kusini na ufalme wa Wakoptiki kule Yemeni ya kaskazini. Pia watumwa wa kikristo kutoka Siria waliuzwa kwenye Hedjaz (sehemu ya Arabuni ambapo kuna mji wa Maka). Wakati ule pia Kanisa la nyumbani mjini Maka lilikusanyika nyumbani kwa Waraqa b. Nawfal. Wakati huu Askofu wa jiji la Sohat, ambayo ni Oman kwa sasa, alikuwa ni mshiriki na mjumbe katika baraza kuu la Maaskofu la Nikea.

2.04 -- Mhammad na “Watu wa Kitabu”

Mhammad (575-632 B.K.) alikuwa amevutwa sana na Wayahudi na Wakristo, kwa sababu walikuwa na kitabu kilichowafunulia siri za enzi za zamani hadi uumbaji wa ulimwengu, na pia lilioagiza maisha yao ya wakati huu kwa njia ya sheria mbalimbali, ndimo liliwatolea matumaini ya mbeleni hadi siku ya kiyama. Mhammad aliwaheshimu Wayahudi na Wakristo akawaita “Watu wa Kitabu” Alitamani kuwa na kitabu kama hicho katika lugha ya Kiarabu. Alijaribu kukusanya habari za kibiblia nyingi kwa kadri alivyo­weza, na kutokana na hayo alitegemea kuunda na kuendeleza dini yake mwenyewe.

Mhammad alikuwa amevutwa sana na Ibrahimu, aliyekuwa Bedui,(Mtuwa kuhama hama) naye aliyekuwa tayari kumtolea sadaka Allah, mwana wake wa pekee (Sura al Saffat 37:99-113). Kwa sababu hiyo Qur‘ani inamtaja Ibrahimu kuwa ndiye Mwislamu wa kwanza (Sura Al‘Imran 3:67).
Musa, kiongozi wa kisiasa na mpatanishi kati ya Allah na watu wake wa agano, anatajwa mara 136 ndani ya Qur‘ani. Yeye alikuwa ni mfano wa kumwongoza Mhammad na wafuasi wake, kwa sababu alikuwa ameunganisha imani na nguvu, dini na serikali ndani ya nafsi yake.

Maelezo kuwahusu mababa wa imani pamoja na Sulemani, pia na maagizo kadhaa kutokana na sheria za Musa, ni mara kumi zaidi ya aya za Qur’an, kuliko habari za yule mtoto mpole wa Mariamu,(Yesu) aliyekuwa mponyaji na mtenda miujiza, pamoja na wafuasi wake. Kila msomaji wa Qur‘ani baada ya muda atajisikia kushurutishwa kuuona Uislamu kama dhehebu la kiyahudi,jambo ambalo linakataliwa kwa bidii na Waislamu.

2.05 -- Ushawishi wa Kanisa la Orthodox katika kuundwa kwa Uislamu

Makanisa ya Orthodox yalikuwa na ushawishi mkubwa zaidi kwa Uislamu kuliko Kanisa la Waroma. Hata hivyo, Wakristo wa Orthodox hawakueneza mafundisho kamili juu ya Kristo kwa Muhammad. Wakati Wakoptiki walipokazia uungu wa Yesu, wakifuata fundisho lao ya Alexandria, Wakristo waliofuata fundisho yaAntiokia, walikazia zaidi upande wa ubinadamu wa Yesu.

Taratibu za ibada za kiislamu zinaweza kufuatiwa nyuma katika ibada za watu wa Orthodox, waliolala kifudifudi wakati wa saumu, juma moja kabla ya Pasaka kwa kuheshimu Utatu Mtakatifu. Neno la “qir’an” katika kanisa la Orthodox wanaotumia lugha ya kiarabu, linamaanisha: kukariri Injili kimoyo-moyo wakati wa misa takatifu. Basi neno hilo linaangaliwa kuwa ndiyo mzizi wa neno “Qur‘an” wala si kinyume chake. Ndani ya Biblia ya ki-asiria neno linalotumika kwa ajili ya wokovu ni “furqan” ambalo linatokea katika Qur‘ani mara nyingi kama ujumbe wa ulio imara zaidi.

2.06 -- Mhammad na tofauti zilizokuwa kati ya Wayahudi na Wakristo

Mhammad alitambua sana mashindano makali na hoja kati ya Wayahudi na Wakristo (Sura al-Baqara 2:113 na penginepo). Kulikuwa na vita vya kikatili sana kati ya falme za Kiyahudi na za Kikristo katika Yemeni ya kusini na kaskazini kwa mamia ya miaka, ambamo pande zote mbili waliwatesa wale walioshindwa kwenye vita vyao. Mhammad aliuon magawanyiko huo kama ni kusudi la Allah, akichokoza mapigano kati ya pande zote mbili katika Hedjaz, ili Uislamu upate nafasi ya kuenea zaidi kati ya maadui hao, waliozidi kudhoofika kutokana na vita vyao. Mhammad akaonekana kama mtazamaji wa kucheka kati yao, ndipo baadaye alipata nafasi ya kuwashinda hao wote.

Wayahudi walimkataa Mhammad kama nabii; walitambua makosa yake ndani ya Qur‘ani wakimkebehi hadharani. Basi akawalaani mara kumi (Sura al-Baqara 2:65-66; al-Ma‘ida 5:60; al-Araf 7:163-166 na kadhalika). Aliwaita kuwa ni adui wa hatari kubwa katika Uislamu (Sura al-Ma‘ida5:82). Aliwalazimisha kabila za Kiyahudi matajiri waondoke na kuhamia pengine, na baada ya muda aliwafanya kuwa watumwa au kuwaua kwa upanga.

2.07 -- Kanisa la Orthodox - mnyororo mrefu wa mateso

Mwanzoni Wakristo walioishi kwenye bara Arabuni walionekana kuwa wapole kati ya maadui wa Waislamu (Sura al-Ma‘ida 5:82). Lakini walipoendelea Kumkiri Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu, basi wakalaaniwa sawa pamoja na Wayahudi (Sura al-Tawba 9:29). Miaka michache baadaye wakafukuzwa kwenye bara Arabuni na Khalifa Umar Ibn al-Kattab. Katika kampeni zake za vita za kuteka sehemu mbali mbali (632-732 B.K.)

Majeshi ya kiislamu yalishinda makao muhimu kuliko yote ya Ukristo wa mwanzoni: Yerusalemu, Alexandria na Antiokia. Miji hii ilifuatwa na Konstantinopoli na Efeso wakati wa mawimbi ya pili ya upanuzi wa Uislamu. Wakristo wengi wa nchi za Magharibi walisahau, waaliacha kwa makusudi au walitambua kimya kimya msiba mkuu huu katika historia ya Kanisa.

Makanisa ya Orthodox mara nyingi yalijaribiwa kwa mateso makuu. Walikandamizwa, waliteswa na kupunguzwa nyakati zote na Uislamu kwa miaka 1.370. Nyakati za maisha ya Mhammad sehemu kubwa ya watu walioishi katika nchi zizungukazo Bahari ya Kati mashariki ya kaskazini na kusini walikuwa Wakristo wa Orthodox, lakini Uislamu ulimeza 90% ya wakaazi wao kwa njia za ushuru nzito mno, makandamizi kadhaa na kudhalilishwa, wakiwafanya kuwa Waislamu kwa lazima. Baki la 10% tu wali­faulu kuwa waaminifu kwake Yesu, mbali na kuhesabiwa raia wa daraja la chini! Waislamu mara nyingi walitumika kama mabwana wanaowatawala hao wachache kwa kupata faida yao tu. Mabaki hao wakati wote hawakuwa tisho au hatari katika uislamu. Kutokana na tabia yao njema Waislamu waliwatazama Wakristo kuwa wapole na wanyonge, walioweza kutishwa kwa urahisi.

Ibada zenye nguvu za kutukuza Utatu Mtakatifu katika Kanisa la Orthodox na kwenye taratibu za uongozi wao iliwasaidia kuvuka magumu hayo. Kwenye nchi zisizokuwa za kiislamu walijiweka chini ya mamlaka iliyotawala, lakini katika unyenyekevu wao mara kwa mara walivutwa kukubali wawe dini ya serikali (Byzantine, Urusi, Ugriki, Serbia n.k.) Waislamu katika serikali zao mara nyingi waliwalazimisha Maaskofu wa Orthodox na viongozi wengine wakikristo wawe watoza ushuru toka kwa wakristo wao kwa ajili ya watawala wa kiislamu. Kama fidia yao walikabidhiwa kiasi cha uwezo wa kuongoza makanisa na mitaa yao. Makanisa ya Orthodox yaliyobakia hadi leo, yakiwa na washiriki millioni 250, ndiyo 14% ya wakristo wote ulimwenguni.

2.08 -- Uislamu na Kanisa la Waroma

Kanisa la Waroma, mbali na mikwaruko zake, linaangaliwa na Waislamu wengi kuwa ni kanisa lenye mamlaka. Linaonekana kwao kuwa na nguvu ya kidini na kisiasa hata baada ya kupotea kwa Utawala wa Kirumi wa magharibi, na baada ya msukosuko dhidi ya matengenezo ya kanisa upande wa Ulaya.

Majeshi ya Mroma Charles Martell yalizima shambulio la kwanza la Waislamu kule Tours, karibu na Paris, Ufaransa (732 B.K.). Vita vya msalaba vya Waroma vilidhoofisha Kanisa la Orthodox walipouteka mji wa Konstantinopoli (1204 B.K.); hadi kupelekea kuanguka kwa ngome kuu ya Ukristo katika mashariki dhidi ya Uislamu, ndipo maeneo hayo yote yakawa mikononi mwa Waislamu mwaka 1453. Baada ya muda si mwingi Waturuki wakafikia mwaka wa1529 malango ya Vienna kwa mara ya kwanza. Nao walipotokea Vienna mara ya pili 1683, kwa bahati kulikuwa na jeshi toka Polandi la Rumi nao wakafaulu kuzuia msukumo wa Waislamu waliokusudia kuchukua Ulaya yote.

Katika karne hizo, baraza kuu la Waroma kuhusu wazushi wa imani walikuwa wamewafukuza mamia ya maelfu ya Wayahudi na Waislamu toka Hispania na sehemu zingine za Ulaya. Kanisa la Waroma na vita vyao vya msalaba pia vilichora picha ya hatari juu ya Wakristo kwa jumla katika kumbukumbu ya ndani ya Waislamu. Mpango wa kiislamu kuwa na serikali ya dini iligongana na mtazamo wa ushindani katika Kanisa la Waroma, ambalo liliwazuia kuenea kwao Ulaya kwa njia ya vita.

Tangu hapo Waislamu wanafikiri kwamba juhudi zote za kikristo za kueneza injili zinakusudia kuanzisha serikali za kikristo. Wanaonea mashaka jitihada ya Kanisa la Waroma ya kuwakumbatia kuanzia mtaguso mkuu wa pili la Vatikani lilipoamua kufunguka zaidi Kanisa lao katika mambo mema kutoka dini zote za ulimwengu. Maneno ya kuvutia ya Papa Yohana Paulo wa pili yanatetea ushirikiano kote ulimwenguni kati ya Waislamu na Wakristo. Lakini hayo yalionewa mashaka, kwa sababu Waislamu wanaamini kwamba Kanisa la Waroma kisiri linakusudia kuanzisha Ufalme wa Kikristo ulimwenguni. Lakini mamlaka ya Mapapa limeshika Kanisa la Waroma katika umoja wa utaratibu maalumu wa kiutawala chini ya kauli mbiu yao ya: “Ufalme wako uje, hapo duniani, kama ulivyo mbinguni. ” - Na idadi ya Waroma jumla yao ni nusu ya Wakristo ulimwen­guni, wakiwa na washirika millioni 950.

2.09 -- Uislamu na makanisa ya ki-protestanti

Makanisa ya ki-protestanti tangu awali yalikuwa „makanisa ya kupambanua“, yaliyojaribu kufanya upya kanisa la Waroma. Walichagua Biblia Takatifu bila mapokeo mengine kuwa ni msingi wao, wakiamini wokovu kwa imani tu, pasipo matendo ya kumpatia mtu haki, na kwa kumtegemea Kristo tu kuwa mpatanishi, wala si mama yake Mariamu.

Makanisa mengi ya ki-protestanti hapo Ulaya katika karne za kwanza baada ya matengenezo ya kanisa, yalikuwa ni makanisa ya maeneo fulani ya watawala. Uamusho wenye nguvu ukafuata baada ya uthabiti na mafarakano na Waroma, ila yakatokeza mwamko mzito wa ki-misheni kwanza Marekani (USA),ndipo Ulaya na Korea. Lakini theologia ya kufuata akili za binadamu tu bila ukaguzi wa mamlaka ya jumla juu ya makanisa, iliwafanya Waprotestanti wengi wenye mawazo ya huru sana (liberal), waanguke katika hali ya huru usio na kicho tena. Makanisa yao mengi ya uhuru yenye jumla ya millioni 600 ya washiriki ni kama sehemu ya tatu ya Wakristo wote ulimwenguni.

Makanisa ya ki-protestanti, yaliyotokea miaka 450 nyuma, yalianzisha namna ya kuwafikia watu kote ulimwenguni kwenye karne za 18 na 19. Walipeleka kwa meli mashine za uchapaji za kwanza katika maeneo ya Mashariki ya Kati wakachapa tafsiri za Biblia katika lugha kadhaa za kiislamu. Pia waliwezesha kunakili Biblia, Qur‘ani, vitabu vidogo vya kikristo na matangazo ya kubandika hadharani. Vituo vya kusaidia watu na shule za ki-protestanti zilitia nguvu kwa malengo yao ya uinjilisti, zote zikiwa na msingi katika Neno la Mungu ambalo limechapwa. Bahati mbaya, shughuli zao za ki-protestanti yaligusa zaidi Wakristo wa Orthodox, na hivyo kuzalisha ushindani wa kudumu wa viongozi wao dhidi ya Waprotestanti.

Waislamu wanawaona makanisa ya Protestanti kwa mashaka, kwa sababu wengi wa washiriki wao wanaangalia Serikali ya Waisraeli kuwa ndiyo wateule wa Bwana. Kwa sababu hiyo Wamisionari Waprotestanti mara nyingi zaidi wanahesabiwa kuwa wapelelezi au ni wasaidizi wa watu wa Agano la Kale.

Waislamu wenye misimamo ya wastani basi wanao maoni tofauti kuhusu Waprotestanti. Shehe fulani wa kiislamu aliuliza: “Kwa nini Waprotestanti walikuwa wa kwanza wa kukanyaga penye mwezi?” Mwenyewe akajijibu kwa swali lake akisema: “Sisi Waislamu tumezuiwa katika kufikiri kwetu na tunashindwa kuendeleza teknologia ya kisasa. Waroma kila wakati inawapasa kuungama makosa yao na wanao hali ya kuvunjika. Waprote­stanti tu wameendeleza roho ya uhuru nao wanatiwa moyo kujaribu mambo yanayodhaniwa kwamba, hayawezekani.” Bidii yote ya kukanusha mipango yake yalikuwa bure. Hata kwa kudokeza kwa marejeo ya kuharibu ya maendeleo ya teknologia hayakubadilisha mawazo yake. Alikuwa na mawazo yake mwenyewe kuhusu viini na shabaha za dini za siku hizi.

2.10 -- Mgawanyiko ya makanisa na mgawanyiko ya Uislamu

Makanisa hayo matatu makuu (ki-orthodox, ki-roma na ki-protestanti) hadi sasa yamegawanyika katika makanisa mengi madogo, majimbo au Sinodi zenye mafundisho na misimamo yao ya pekee, na yanazidi 22 elfu; namba hiyo inatuongoza kutubu, tunapokumbuka sala ya Yesu Kristo: “Ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.” (Yohana 17: 22 b)

Mambo ya msingi yanayounganisha makanisa hayo yote ni mambo matatu ya katekisimo: Sala ya Bwana, Imani ya Nikea na Amri Kumi pamoja na maelezo yao kufuatana na Agano Jipya. Kukiri kwetu kwa Mungu, aliye Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu inahesabiwa kuwa dini ya kuabudu miungu mingi, ambayo ni unajisi usioweza kusamehewa katika Waislamu. Wao hawamkubali Mungu wa Utatu, ila Allah peke yake, asliye mmoja na wa pekee. Nao pia wanakataa kusulubiwa kwa Kristo, uliyo msingi wa imani yetu (Sura al-Nisa 4:157). Uislamu unajihakikishia kuwa ni nguvu kote duniani dhidi ya Ukristo (1.Yohana 2:22-24; na 4:1-5). Mawazo kama hayo yana mizizi ya chini ndani ya Waislamu wote, hata kama hawajielezi wazi. Utamaduni wote wa Waislamu umepenywa na shabaha hiyo iliyo kinyume cha Ukristo.

Yeyote anayetambua mgawanyiko wa makanisa katika maeneo ya Mashariki ya Kati na ulimwenguni kote hatashangaa kusikia kwamba, Uislamu pia hauna umoja. Jinsi makanisa yalivyogawanyika mara elfu, ndivyo na Uislamu unajumlisha vipande vingi vya kubadilibadili vya rangi mbalimbali. Mikondo miwili mikuu imeendelea katika kutokea kwa Uislamu.

2.11 -- Wasunni - mkondo mkuu katika ya Uislamu

Wasunni wanajiona wenyewe kuwa ndiyo wenye uaminifu wa kutunza Uislamu wa asili, kwa sababu wao hawafuati tu Qur‘ani kwa bidii tu, lakini pia wanaiga tabia za nabii wao yaani Sunna katika maisha yao. Baada ya ushindi wa mwisho wa machujo ya kielimu (ya Mu‘tazilites) mwelekeo ulianza kwenda upande wa pili. Uislamu ulipata kuwa dini ngumu, ya kufuata sheria nyingi katika msingi wa Shari‘a. Kutokana na Qur‘ani, na Sunna, mfano wa hoja zao na jumlisho wa shule zao tano za sheria, wao waliunda Shari‘a zao. Waliendeleza sheria zilizoingiza kila eneo la maisha chini zaidi kuliko taratibu za imani ya kiislamu. - Hawa Wasunni wanajumlisha 84% ya Waislamu wote, wakikaribia bilioni moja wa wafuasi wa Mhammad; jumla hiyo ni karibu sawa na wafuasi wote wa Kanisa la Waroma ulimwenguni.

2.12 -- Washia - dhehebu la kwanza la kiislamu

Nyakati za kuundwa Uislamu, wafuasi wa Ali – mwana wa kulea wa Mhammad, ambaye pia alikuwa ni mpwa wake na mkwe - waliachana na Wasunni pamoja na wana wawili wa Ali, ambao ni Hassan na Hussein. Sababu ya kugawanyika haikuwa hoja ya mafundisho kuhusu imani, lakini ilikuwa ni dai ya nasaba ya kupokea uongozi ndani ya dola ya Uislamu. Washia walidai kwamba, Ali na wanawe wangestahili kupokea uongozi wa dola ya uislamu baada ya kufa kwake Mhammad. Shauri hili laonyesha kwamba Uislamu unajielewa kwanza kuwa ni dola, wala si dini tu. Washia waliendelea kumtukuza Ali na wanae wawili karibu kama miungu, nao wakaendeleza mwongozo wa kipekee wa maimamu wao - saba kwa ajili ya kundi moja na kumi na wawili kwa wengine - ambao wanawatii bila kupinga. Dai lao la ayatullah ni ya kupokea uongozi kutoka kwa imamu wao wa mwisho. Washia jumla yao ni 14 hadi 16% ya Waislamu wote ulimwenguni, ni sawa na washiriki millioni 200.

Pamoja na Washia kuna madhehebu mengi ya kiislamu, njia tofauti, desturi, mashirika, kanuni na vyama, ambao hawako tayari kuunganika, bali kila moja inafanya bidii kuimarisha uhuru yake.

2.13 -- Mkondo wa tatu wa kuenea kwa Uislamu

Baada ya mikondo miwili ya Uislamu iliyotangulia kujaribu kupenya Ulaya iliposhindwa (B.C. 732 na 1683) kutokana na majeshi ya kiroma, mkondo wa tatu ukaanza 1973 baada ya kuongezeka kwa bei ya mafuta ya ardhini iliyotokea kwa haraka. Nchi za kiislamu zilizotoa mafuta zikapata kutajirika kiasi kikubwa. Kwa sababu ya mpango wao wa kuchangia asilimia fulani ya faida yao kwa ajili ya kuendeleza elimu na maarifa ya kiislamu, mawazo mengi ya Uislamu wa asili yaliweza kulipiwa. Hassan al-Banna, mwenye kuanzisha umoja wa Uislamu, alisema: “Mwislamu anayesali, kufunga na kulipa kodi yake ya kidini bado sio Mwislamu wa kweli. Ila tu, kama Shari‘a inaongoza serikali ambamo anaishi, basi Uislamu wake umepata kukamilika.” Umoja wake wa Kiislamu uligawanyika katika vikundi zaidi ya 50 karibu katika nchi zote za kiislamu. Wanajaribu kufanya matengenezo ya Uislamu na kuleta nchi za kiislamu zisizofuata sheria chini ya uongozi wa Shari‘a.

Wakati huo huo Wailslamu wa asili walianzisha harakati zilizopangwa kinaganaga, ili kueneza Uislamu kote katika bara kuu zote tano. Misikiti mingi zinachipuka kote kama uyoga. Wakristo wasiojua hukaribisha Waislamu ndani ya mashirika yao ya mapokeo mengi. Hawataki kutambua kwamba, kabla ya hapo hawajaishi Waislamu wengi hivi katika nchi wanapozidi Waprotestanti kama siku hizi! Tunaishi katikati ya vita vyao vita­katifu - pasipo kutambua!

2.14 -- Aina gani ya Waislamu tunakutana nao?

Waislamu hawaishi na kufikiri sawa. Kila mmoja ana nafsi ya pekee. Majaribu yote ya kuwapanga katika namna fulani hairidhishi au sio kweli. Namna sawa ya Mwislamu dhahiri haipo. Vipawa tofauti, mapokeo, elimu na misimamo zimechanganywa ndani ya kila nafsi.Haitafaa kusema juu yao kwa jumla “Waislamu”.Mtu anapotaka kuwaelewa Waislamu anahitaji muda. Inapasa kumwuliza kila mmoja anakotoka, anawaza nini na anavyojisikia, pia na matatizo yake ni nini. Majibu yote ya jumla au ya juujuu yatakuwa na makosa. Kwa lengo la kupata urafiki na Waislamu tunahitaji uvumilivu, ili kupata kuwafahamu. Hilo nalo ni kweli kwao wakipenda kutufahamu sisi. Tukiwa na malengo tuliotayarisha kimawazo tu, lazima tuambatanishe na hali halisi. Mwislamu kwa haraka anaweza kusikia na kufahamu kwamba tunamheshimu na kwamba hatukusudii kupata faida kutoka kwake, bali tunamkubali jinsi alivyo. Injili inaweza kufanya kazi kwa nguvu ya Mungu kama uhusiano wa kuaminiana ume­jengwa kwanza kati yetu. Kuomba kwa uvumilivu ndiyo siri ya baraka ya kudumu.

Mbali na ukweli kwamba, kila Mwislamu pekee yake ni mtu binafsi, aina fulani za namna zao zaweza kuonekana - pamoja na usetiri fulani - kama tabia ya wote au ya kuwaunganisha; kwa hiyo yawezekana kugawa makundi mbalimbali ya Waislamu.

2.14.1 -- Waislamu wahafidhuna, wenye itikadi kali na kumuogopa Allah

Vijijini hadi kwenye Vyuo Vikuu, katika misikiti na kila aina ya kazi utaweza kukutana na Waislamu watakao kuishi kufuatana na Qu‘rani na mapokeo ya mtume. Si wachache bali wengi waliokaririr kimoyomoyo Qur‘ani kwa kiarabu yote au kwa sehemu wakati wa utoto wao. Hivyo wanavaa “miwani ya kikurani”n a kwa hii wanafahamu ulimwengu wao. Mbali na utamaduni ya Qur‘ani na amri za Shari‘a, hakuna mwenendo wa maisha unaokubalika kwao. Wafuasi wa mazoea, dini zingine na wote wanaoabudu sanamu wanahesabiwa kuwa najisi na wamelaaniwa na Allah. Uhalali na uharamu wa vyakula ume­gawa ulimwengu wao katika wala-nguruwe na watu safi. Kununua nyama sokoni ambapo ile Bismillahi haikusemwa wakati wa kuchinja ni kufuru kwa Waislamu wahafidhuna. Hata hivyo, wakishurutishwa kula, basi haitakuwa kosa kwao.

Wale walio na bidii kwa dini yao hawaruhusiwi “kuwaza au kutamka kwa Mateto” juu ya Qur‘ani. Kama utatia mashaka kwa aya moja tu, jengo lote la mtazamo wao wa ulimwengu utaporomoka. Kwa sababu hiyo inawapasa kulinda ukweli wa Qur‘ani na imani yao wakati wowote unapotolewa maoni tofauti. Qur‘ani ndiyo maisha yao. Unaweza tu kuwaeleza habari ya Injili kwao kwa msaada wa maneno ya Qur‘ani, ukiyatumia kwa maana ya Injili.

Ni kitu cha kushangaza kwamba, hata katika wasomi wa Vyuo Vikuu kuna wengi wanaohifadhi desturi na wahafidhuna. Wanapotoka katika vijiji vyao na kuishi mijini na kuona maisha ya siku hizi ya uhuru na yenye dhambi tele, wanaona haya kwa ajili ya watu wao, ndipo wanarudi kwenye mizizi ya utamaduni wao na kuwa Waislamu wenye siasa kali zaidi kuliko walivyokuwa mwanzoni. Wanajaribu kuthibitisha yale yaliyokuwa msingi wa maisha yao na kutetea kwa nguvu ukweli wa Qur‘ani kwa wanadamu wote, na wanafanya hayo kwa nguvu kubwa zaidi.

Wakati wahafidhuna wa Kiislamu wakifaulu kupata elimu na vyeo vya juu ndani ya jamii zao, huwa wanajaribu kutengeneza watu wao kwa njia za amani au pia kwa njia za fujo. Wako hasa katika waumini hao walio tayari kuwaua Waislamu walio huru na wa kisasa, au wanaweza kujiunga na vikundi vya fujo, ili waimarishe taratibu za Uislamu nchini mwao.

Hesabu ya wahafiduna kati ya Waislamu inatofautiana ndani ya nchi na nchi. Wanafikia 15 hadi 35%. Kufuatana na mahesabu ya kiserikali, wakati wa uchaguzi wanafikia tu 10 hadi 20% ya wenye kuchagua. Sehemu kubwa zaidi ya Waislamu wote sio wenye fujo. Lakini Qur‘ani inawaagiza kufuata Shari‘a ndani ya nchi zao za kiislamu kwa vyo vyote vil kabisa!

2.14.2 -- Waislamu huru

Jinsi ilivyo katika nchi zinazoitwa za Kikristo, ndivyo ilivyo zaidi sana ya nusu ya Waislamu ndani ya nchi zao ni aina ya huru, wa kisasa, hawana siasa kali na wenye kupenda amani. Wanafanya kazi zao polepole kwa kuchuma kiasi cha kutosha kulisha familia zao. Hawana nia ya kujibidiisha katika shughuli nyingi. Wanatazamia kujipatia friji, TV kubwa na ikiwezekana hata gari au pikipiki, kwa hayo wanaridhika. Kwa wingi wao dini ni jambo la pili maishani mwao au namna ya kufanya biashara.

Katika maisha ya kila siku, Waislamu huru wanatenda kwa kumcha Allah, kwa sababu yeyote asiyeishi kufuatana na utamaduni ya Uislamu hawezi kuendelea kununua au kuuza. Wengi wanatumia matamshi ya kidini katika mazungumzo yao, wakitetea Uislamu hadharani kwa ajili ya mapokeo yao, pia na kutegemeza utamaduni uliopo. Ikiwa kama mtu mmoja ndani ya familia anabadilisha dini kuwa Mkristo, ataanzisha msukosuko. Kwa ajili ya ulinzi wa jina safi la ukoo mwongofu atachukiwa, atatishwa au kufukuzwa aende nchi nyingine. Hata kwa vyovyote harufu ya uaminifu hafifu kwa Uislamu usichafue jina lao. - Mbali na hayo, washiriki wa ukoo wa hali ya huru wanahudhuria mara chache tu kwenye swala maalumu, au wanaenda tu, ili waonekane. Mara chache wanafungua Qur‘ani si kwa ajili ya kuizingatia. Namna ya wasiwasi kwa ajili ya dini imewakumba Waislamu walio wengi. Hao ni 50 hadi 70% ya wenyeji wote, inategemea maeneo au nchi wanamoishi.

Kwa bahati fahari kwa ajili ya taifa na Uislamu zinaweza kuunganika. Kama ni hivi, dini itategemeza hali ya kujisikia kuwa raia wa taifa hilo, lakini pia kujisikia hivyo itamwimarisha kidini. Hata hivyo, kama nchi ile imefikia uhuru kabisa wa kiislamu, basi Mwelekeo ni wa kutegemea mambo ya maisha tu bila kujali ya kiroho. Kazi, riziki ya kila siku na familia mapema zitachukua nafasi kuliko dini.

Waislamu huru wanapendelea matamshi ya ubora wa ubinadamu ndani ya Qur‘ani na katika utamaduni. Rufuku ya vyakula kadhaa, maagizo kuhusu vita vitakatifu (Jihad), hali ya wanawake katika Q‘urani au hata hukumu katili kwa makosa fulani yanapuuzwa kwa utetezi kwamba, maagizo hayo yalihitajika kwa Wa-Beduini siku za Mhammad. Siku hizi, baada ya kupata maendeleo, amri hizo hazina uzito tena. Watu wenye uhuru huishi kufuatana na Uislamu ambao umekatwa kwa sehemu.

Serikali karibu zote zinajiendea kwenye njia za namna hii. Wao wanaruhusu viongozi wa miskiti kuchunga wajibu binafsi za Shari‘a. Uongozi wote kuhusu Jihad na pia hukumu katili zina­bakia mikononi mwa serikali. Wanajaribu kusikilizana kati ya Shari‘a na amri za haki za binadamu kuhusu mataifa yote, na wanawazuia wale wahafidhuna katika nchi zao. Mashambulio ya kikatili kule Misri au Algeria zinajulikana kuwa ni vita za ndani kwa ajili ya kuhakikisha ufuasi wa Shari‘a kamili. Lakini hayo ni mambo ambayo Waislamu wa mkondo wa huru kwa vyovyote wanajaribu kuzuia kwa gharama zozote katika serikali zao.

2.14.3 -- Wanawake wa Kiislamu

Nusu ya Waislamu ni wanawake! Tusije tukatafakari tu habari za wanaume tunapoongea habari za Waislamu. Wanawake nao wanachukua nafasi muhimu ndani ya Uislamu. Mara nyingi wanaongoza watoto wao ndani ya familia zao, tena zaidi kuliko waume wao.
Hata hivyo, katika Qur‘ani imeandikwa wazi:

Mwanaume si kama mwanamke (Sura Al 'Imran 3:36).

Hilo neno la kweli kabisa ndani ya Uislamu lina msingi kisheria. Qur‘ani inatamka:
Wanaume husimama juu ya wanawake kwa vile Allah amempendelea mbele ya mwenzake na kwa taratibu hiyo wanaume wanatumia fedha zao (kwa ajili ya kupata wana­wake kama bibi arusi) (Sura al-Nisa 4:34).

Mbele ya hakimu ushuhuda wa Mwislamu mwanaume unahesa­bika sawa na ushuhuda wa wanawake Waislamu wawili (Sura al-Baqara 2:282). Katika mashauri ya urithi mwanamke hupokea nusu tu ya mume au mwana wake, dada hupokea nusu ya kaka yake, au binti nusu ya yale apatayo mvulana (Sura al-Nisa4:11 na 176). Kisheria mwanamke thamani yake ni nusu ya mwanaume.

Mwanaume anaruhusiwa kuoa wanawake hadi wanne (Sura al-Nisa 4:3) akiweza kuwapenda wote wanne kwa usawa. Kwa vile wanaume wengi siku hizi hawana mishahara ya kutosha kwa kutunza wanawake wanne na watoto wao, ndoa za mke mmoja inazidi. Basi, wanawake wa mwanaume mmoja wanasumbuka kwa udhilifu na wivu zaidi kuliko tunavyoweza kudhania.

Katika familia ya kiislamu mume anayo haki ya “kufundisha” mke wake. Kama anakuwa mkaidi, anaweza kusema naye katika “hotuba”. Ikiwa anaendelea kuwa mkaidi, anaweza kukataa haki yake ya kike na bado akiendelea kuwa mbishi, anayo haki ya kumpiga hadi atii, ila haruhusiwi kuvunja mifupa yake (Sura al-Nisa 4:34)

Kufuatana na Qur‘ani (hii haimo katika sheria za Uturuki, Misri na Tunisia na nchi zingine chache za kiislamu) mume anayo haki ya kutaliki mke wake kwa sababu yoyote. Baada ya muda wa kungojea miezi 3 au 4 anaweza kumwoa tena, kuachana naye tena, pia na kumwoa tena. Baada ya kutangua ndoa mara ya tatu, huyu mwanamke inampasa kuolewa na mwanaume mwingine. Kama huyu mwanaume naye anaachana naye, mume wa kwanza anaruhusiwa kumwoa tena (Sura al-Baqara 2:229-230). - Mateso ya wanawake yanayoendelea katika nchi zingine za kiislamu yamekwisha kuwa taabu ya ndani sana kuliko tunavyoweza kudhania. - Ni nani aliye na wito mtukufu kusema na wanawake wa kiislamu na kuwapelekea Injili ya uhuru wa kiroho katika msingi wa msamaha kamili na zawadi ya Roho Mtakatifu?

Si vema kwa wanaume wa kikristo kuongea peke yao na wanawake wa kiislamu, ila tu akiwepo mke wake mwenyewe. Basi, wanawake wa kikristo wangepokea huduma hii ambayo haikujaliwa mara nyingi; kwa hiyo wao wangeongea na wanawake na wasichana habari za Kristo na kuwashuhudia jinsi wanavyoendelea na Mwokozi wao kila siku. Wamama wa kiislamu ndiyo wenye kuwalea watoto wao; kwa sababu hiyo kuwapelekea Injili wanawake wa kiislamu, hasa wakina mama, ndiyo huduma bora mno katika malengo ya kuwafikia Waislamu wakati wowote. Taratibu za TV kwa ajili ya wanawake na vitabu kwa ajili yao vilivyoandikwa na Wamama Wakristo zinahitajika kwa lazima. Muda wa kizazi kimoja hapo nyuma wanawake na wasichana wa kiislamu chini ya 25% tu waliweza kwenda shuleni! Siku hizi hesabu yao waliopata masomo imefikia 40 hadi 70% ya wote. Nani kati yenu anatambua hii nafasi bora na kuilinganisha na wito wa Injili.

Wanawake wa kiislamu mara nyingi ni wenye kicho na tabia ya kidini zaidi kuliko wanaume. Inasemekana juu ya Mhammad kwamba, aliwahi katazama ndani ya jehanum na kuona 90% ya wote mle walikuwa ni wanawake, kwa sababu hawakuwatii waume wao kila wakati. Mhammad naye alidai kwamba, alitazama pia ndani ya paradiso. Katika wakaaji mle aliona 10% tu kuwa ni wanawake, kwa sababu waume wachache tu walishuhudia juu ya wake zao kwamba ni wacha-Mungu na ya kutii kila wakati. Ufahamu wa aina hii inawachochea wanawake kushika sana amri za kiislamu zaidi kuliko waume wao, kwa kutegemea kwamba, watapata nafasi ndani ya paradiso katika nafasi zile chache zilizopo kwa ajili ya wanawake.

Ni nani atakayewahurumia wanawake wa kiislamu, na atakayejaribu kwa uaminifu kutafuta njia kutuliza uchungu wao duniani na kwa ajili ya haki katika ulimwengu ujao kwa jina lake Yesu?

2.14.4 -- Vijana wa kiislamu

Nusu ya waislamu wote ulimwenguni ni chini ya miaka 18. Katika nchi chache za kiislamu hesabu hiyo iko chini zaidi, ni miaka 16 tu. Aliye na uzoefu katika kazi za uinjilisti kwa vijana, bila shaka ataguswa sana na jambo hilo! Watoto, vijana na watu wazima wenye umri ndogo wanahitaji mipango zilizo tofauti na zile za watu wazima. Ukweli huo kutokana na mahesabu unadai kutafakari na kupanga kwa upya njia za kuwafikia, pia na kwa ajili ya kuwajulisha watu wanaoombea huduma hii.

Vijana pote duniani wanapenda mchezo wa mpira na mashindano ya magari. Ukisafiri ndani ya nchi za kiislamu, kwa uchangamfu utaulizwa habari ya Beckenbauer, Rummenigge na Schumacher. Pia Becker na Graf wanakuwa na majina maarufu sana kati ya vijana wa Kiislamu.

Vijana wa kiislamu siku hizi hujifunza kusoma na kuandika. Wanatafuta vitabu na magazeti zinazowapendeza. Wana hamu sana ya kuongeza elimu. Wako tayari kujifunza kila jambo. Huwa wanaamini ndani ya sayansi na wanafikiri kwamba, wanaweza kushinda maisha kwa shahada safi. Kwa kuwapatia maandiko ya Neno la Mungu, vitabu au magazeti yanayovuta akili za vijana. Kozi katika shule za Biblia kwa njia ya posta inaweza kutayarishwa kwa urahisi, na kwa njia hii makumi ya maelfu watajiunga katika muda mfupi.

Wengi wa vijana siku hizi hawatafuti habari ya msamaha wa dhambi. Hawatafakari kuhusu maungamo au imani. Ila wanatafuta kuchunguza kila jambo na kila aina ya watu: Yesu, Paulo na Yohana sawa na wakina Marx, Lenin na Mao. Hii kiu ya elimu ni mlango wazi tunaoweza kutumia kuwaonyesha habari ya Injili bila matatizo. Wengi wa hao watafutao elimu wataguswa na kubadilishwa na upendo wa Yesu Kristo, ukiletwa kwa unyenyekevu, upole na amani yake.

Namba ya wasomi wa shule za juu na vyuo vikuu inaongezeka Wana computer au wanapata nafasi kutumia mitandao mahali pa kunywa chai au nyumbani kwa rafiki fulani. Kweli,mengi yasi­yofaa na ya kuchochea mavutano kati ya makundi ya Waislamu, pia na muziki za aina mbalimbali zaweza kusikilizwa kwenye vyombo hivi. Lakini kila awezaye kutengeneza utaratibu wa kiroho unaoweza kusaidia watu wa umri mdogo, mapema atahesabu maelfu watakaotazama ndani ya yale aliyoyatia katika ukurasa wake wa mtandao; nao waangalizi watapatikana pia ku toka nchi za kiislamu zilizofungwa kwa injili. Na yanayotafutwa hasa ni malinganisho ya mambo ya kila siku kati ya Injili na Uislamu, pia na majibu ya kutia moyo juu ya maswali nyeti.

Kuwapatia nyimbo nzuri za Kikristo zikiwa na sauti ya kienyeji pia ni njia bora ya kuwavuta. Nyimbo za kijerumani za zamani au nyimbo za kanisani za kiamerika za kupiga chuku haziwavutii zaidi vijana wa kiislamu.Injili inadai kupelekwa mbele pamoja na sauti za nyimbo kwa namna ya maeneo yale ya muziki ya mipigo mitano au kuminambili. Hapo utaona kwamba, hata wale walio wageni wa mambo ya biblia, nao wataanza kuimba hizo nyimbo mpya. Hali ya kumstahi kwa moyo muimbaji na hofu kwa ajili ya hakimu wa ulimwengu wote bado si ya kikale, ijapokuwa tabia ya mambo ya kisasa ipo.

Nafasi ya kuwafikia Waislamu na Injili haijawa nzuri kuliko siku hizi, kwa sababu nusu ya Waislamu walio na umri mdogo wako wakijifunza kusoma, kuandika na kutafakari; na wengi wao wanawaangalia kwa shauku wale mabingwa wa michezo na teknologia. Msichana wa Wabedouini wa Hadramaut, akiishi ukingoni mwa jangwa kuu ya Rub al-Khali, alipoulizwa katika orodha ya maswali kuhusu aina ya muziki anayopenda, basi akajibu: “Nyimbo za ABBA wa Swedeni”.

2.14.5 -- Waislamu wamechanganyikiwa

Kwa vile kizazi wa siku hizi wa Waislamu wanajifunza kutafakari wazi, basi wanaanza pia kuuliza habari ya mapokeo yao na dini yao kwa shabaha. Madhaifu ya Uislamu yaliyo wazi siku hizi basi, hayafichiki tena kwao wenyewe.

Waislamu wachache wanaoudhika wanauliza: “Kwa nini majeshi ya Waarabu millioni 250 bado hawajaweza kushinda askari za Waisraeli millioni 5 tu katika miaka hii 50 iliyopita? Bila shaka hapo kuna tatizo. Je, shida iko upande wetu?”

Wengine wanadai wakisema: “Neno UISLAMU lina maana muhimu. Mojawapo ni: Kufanya amani! Mbona basi nusu za vita zote duniani zinahusu nchi za kiislamu? Kwa nini sisi tunapelekea nchi zingine machafuko, vita za kiraia, kumwaga damu wala si amani pamoja na maendeleo?”
Wengine nao wanaongeza: “Nchi za kiislamu zinazotoa mafuta ya ardhini zina watu matajiri kuliko kote duniani; lakini zaidi ya 10 za nchi za kiislamu zimo katika nchi zilizo maskini kabisa na zinahesabiwa kuwa chini ya kipimo kile cha umaskini. Kwa nini serikali za kiislamu zilizo tajiri sana haziwasaidii kwa ukarimu Waislamu maskini na wanaoishi taabuni? Na kama wanasaidia kidogo, kwa nini sehemu kubwa ya mali inapotea kwenye daraja za juu za serikali, wakati ambapo kidogo mno inapenya hadi chni kwa wale wahitaji?”

Kuna habari ya dreva Mhindi wa Shekh ya kiislamu kule Arabuni aliyeulizwa: Je, umepata kuwa Mwislamu kwa moyo katika miaka hii kumi na moja ya huduma yako kuwa mlinzi wa mahali patakatifu pao? Huyu dreva akafoka kwa sauti: “Nyamaza! Sitaki kusikia lolote juu ya Uislamu tena. Ungejua ni mambo gani wanayozungumza, wakinywa, na wanayoyatenda wakiwa peke yao, basi usingeniamini.“ Alipoulizwa tena, ni hatua gani angependa kuchukua baada ya kujua hayo yote, basi akajibu: ”Nitaenda kusoma habari za Ukomunisti na pia Ukristo na ndipo nijaribu kulinganisha ni ipi katika hizo mbili itanipatia msingi bora kwa maisha yangu. Nipo nitaifuata hiyo.”

Msomi mwenye kuhitimu chuo kikuu cha Al-Azhar kule Kairo alitaka kukamilisha na kung‘arisha matamshi yake ya kiarabu kati ya kabila za wenyeji wa Arabuni. Maana alifundisha habari ya vitabu vya kufaa fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Riad Wingi wa wanafunzi wake walimpinga kwa sababu alitolea mawazo ya kisasa ndani ya mafundisho yake, na pia badala ya kuvaa kanzu nyeupe alijivisha aina za suruali za ki-magharibi. Wakati ushindani wao ulipozidi na baadhi ya wanafunzi walipomtupia mawe madogo wakati akisomesha, basi akakasirika na kukimbia. Toka darasani akafanya hima hadi makao ya walimu chumbani kwake, ndipo akachukua Qur‘ani na kujaribu kujituliza kwa kukariri sura hadi sura. Mara moja akaacha hayo na kukiri baadaye: “Kwa dakika hizo nikatambua kwamba, ni kitabu hicho kinachotenda kazi kama kizuizi kwenye akili za Waislamu na kukataza hoja zao za kutafakari, pia na uadilifu wao.” Hapo akachukua Qur‘ani na kuikatakata kwa hasira, akakimbia nje kwenye bustani na kujaribu kuchoma karatasi zake.

Walimu wengine waliposikia milango kufungwa kwa nguvu pia na jinsi alivyoendelea kukariri Qur‘ani kwa sauti, walimkimbilia na kumtuliza. Lakini hapo wote wakasimama kimya na kushitushwa kwa kutazama Qur‘ani ilivyoendelea kuteketea. Kila mmoja alijua: Uhalifu huo unadai kwamba, mvunjaji huyu wa sheria achomwe. Hakuna aliyesema neno. Huyu mwalimu alipopata akili, akakimbia chumbani kwake, akachukua fedha na pasporti yake, akaita Taxi na kukimbizwa kiwanja cha ndege na kutoroka mbali na mtego wa kumwua kabla haijafunga juu yake.

Hao watu hawakuwa na uhusiano wowote na Wakristo. Walitambua madhaifu ya Uislamu hata katika hali yao ya kuwa nyuma ya nchi zao na walijaribu kukimbilia hali zao za kufungwa kiakili. Wasomi wa afya, binti za wafalme, Mashehe na Waislamu wa kawaida kabisa, wote hao wamegundua waziwazi mapingano yaliyo dhahiri ndani ya Qur‘ani nao wanatafuta kwa bidii majibu na falisafa bora za maisha. - Sisi basi tumwombe Mungu tuwagundue Waislamu waonao ubatili huo na kujaribu kuwasaidia kabla hawajashikwa na mikono ya watu waliojitenga na dini yao. Inahisiwa kwamba 5% ya Waislamu wote hawaridhiki tena na dini yao na wanao hamu ya kumpata fulani atakayewapa nuru.

2.14.6 -- Wasiomuamini Mungu miongoni mwa Waislamu

Katika utaratibu fulani wa TV msanii maarufu wa kiislamu aliulizwa yeye ni dini gani. Alijibu bila kusita: “Mimi ni wa dini iliyo bora duniani, Uislamu! ” (Sura Al-‘Imran 3:19;110; al-Fath 48:28; al-Saff 61:9 na penginepo).

Alipoulizwa zaidi, kama anaamini kwamba yuko Allah, alijibu: “Hapana, kwa kweli hapana! Imani ya aina hii ni kwa wazee kabla hawajafa, na watoto; lakini sisi ni watu wa kizazi kinachotenda!”Huyu mwandikaji wa habari alishitushwa sana akaendelea kumwuliza, ni jinsi gani atakavyorejea kama Waislamu wakishambuliwa. Huyu mtu akarudisha jibu kwa haraka: “Hapo basi nitakuwa wa kwanza kushika Kalazhnikov (bunduki) na kutetea Uislamu”. Basi bado alijihesabia kuwa Mwislamu ingawa hakuamini kwamba Allah yupo, wala yeye hakusali! Uislamu sio dini tu lakini pia ni utamaduni, serikali na jamii ya desturi moja.

Wakati wa somo la uhusiano kati ya Uislamu na Ukristo kijana wa Uturuki akampinga mwalimu: Uislamu ni wa upole zaidi, nzuri zaidi, ya kibinadamu zaidi na ya kisasa zaidi kuliko yale aliyo­yasikia katika somo lile. Yule kijana wa Uturuki alipokaribishwa kueleza zaidi msimamo wake kwenye chombo cha kupaza sauti mbele ya darasa, basi alisema kwa uchangamfu, ili kutia nguvu msimamo wake. Mapema huyu mwalimu aligundua alikotokea, akakata maelezo yake na kumwuliza: “Je, katika maisha yako uliwahi kufungua Qur‘ani? ” “Hapana” akajibu huyu Mturuki akishangaa kwa swali hilo. Alipoulizwa zaidi, ni mara ngapi ali­shiriki katika sala Mskitini, alijibu kwamba, hajasali wakati wowote! Lakini aliipigania dini yake kwa nguvu. Basi Uislamu ni zaidi ya Qur‘an na sala. Yeye alikuwa ni mmoja wa wale Waislamu wa kisasa waliopoteza imani yao - ila bado wanaupigania Uislamu wasiouelewa.

Mbengali aliye daktari wa wakina Mama, Dr. Nasrin alichochea sahihisho kwa maandishi ya Qur‘an kuhusu hali ya wakina Mama na jinsi wanavyotendewa wasichana katika ndoa. Ilimpasa kutoroka kwenda Sweden, kwa sababu wanaume wa kiislamu walisikia wivu kwa ajili ya haki zao na kwa sababu alithubutu kutia hoja kupitia Qur‘an! Huyu daktari bado anajihesabia kuwa Mwislamu, ingawa alipoteza imani ndani ya maongozi tukufu ya Qur‘an kwa njia ya mambo aliyoyaona maishani na kazini.

Wanasiasa wa kiislamu na wenye daraja ya chuo kikuu waliowahi kuishi ulaya au marekani kawaida ni wenye maswali zaidi juu ya Uislamu. Maisha yao huwa ni tupu, maana walipoteza imani yao pasipo mashaka ndani ya Allah. Ila kwa sababu ya familia zao huwa wanashiriki katika sala wanaporudi nchini walipozaliwa. Kawaida nao wanafunga mwezi wa Ramadhani na kutoa sadaka zao za kidini wazi. Ila moyoni wameenda mbali na sheria za Uislamu, nao wanatafuta kwa upeo wa macho mambo mapya wakati huu wa fataki na vyombo vya kuzunguka angani. Katazo linalokua kwao juu ya Uislamu wa kihafidhuna lilibatilishwa kwa kukutana na wasomi wenye sifa za juu, wajuzi wa teknologia na viongozi wa serikali kadhaa toka mashariki na magharibi, walipotambua kwamba, wengi wa jamii ya wenye elimu na vyeo sio Waislamu, bali wanaishi maisha ya heshima.

Hesabu za Waislamu wasiomwamini Mungu si kubwa, ni kama 1% tu, pengine ni zaidi kidogo katika nchi ambazo ukommunisti inaongoza kwa kupewa nafasi. Wanaweza kutambulikana, kama vile wasosholisti nchini Uturki, kwa mashambulio yao makali katika magazeti na vitabu juu ya Mhammad na Uislamu wake.

2.14.7 -- Mambo ya siri katika ya Uislamu

Utupu wa Waislamu unapembea kama mkono wa saa kubwa unavyopembea kulia na kushoto kati ya msimamo wa asili na shauku ya kutumia nguvu na upande wa pili hali ile inayojificha pasipo imani ndani ya Mungu (Allah). Hali hii inazaa hali ya kutokuridhika, uzuizi na hamu ya kutafuta njia mpya inayoweza kutegemewa. Moja ya njia hizo yaweza kuonekana katika siri za Uislamu na kwa kudharau wanakwenda mbali na Muft wa kiislamu wanaoshika sana sharia na kuchunguza hata vitu vidogo sana, pia na wanasheria wanawaacha.Hao watafutaji wa kweli katika mwenendo wa kidini wamejitenga na mwenendo wa kukaza hali ya kudumisha Miskitini; wakifanya hayo kwa kutawadha jinsi inavoamriwa, pia na marudio ya sala zao zinazo­fisha roho. Wao hawapati chochote pale kinachoweza kuridhisha roho au moyo. Basi wanaenda mbali na Uislamu halali, ndipo wanaungana katika Mashirika ya namna ya ushirikina na kujaribu kuunda aina ya kidini ya kibinafsi na kicho cha kweli kinyume na Qur‘an na maandishi yasiyo ya kiislamu.

Unaweza kukuta ma-Sufi na Tariqas zao mbalimbali nchini Moroko, pia na Sudan, Uturuki na Pakistani. Hata nchini Uchina na Indonesia Uislamu umegawanyika katika matawi ya kisiri na ya kisheria. Kule Moroko unaweza kuona makaburi yaliyopakwa chokaa ya kuheshimu siri fulani, yakiwa juu ya vilima na kwenye barabara kuu. Wanawake wasioweza kuzaa mara nyingine huwa wanasugua tumbo lao kwenye kaburi la mtakatifu fulani, ili ikiwezekana wapate kuzaa. Nchini Sudan darweshi huwa wanarukaruka na kujivingirisha chini vumbini ili kuonyesha shauku yao kwa ajili ya Allah na hali yao ya kiroho.

Kule Misri ma-Sufi mara kwa mara hukaa au kusimama katika duara na kurudia jina la Allah au moja ya sifa zake: “huwa, huwa, huwa ” (ambayo kwa kiarabu ina maanisha “ndiye, ndiye, ndiye”) mara nyingi isiyohesabika hadi mmojawao aingie katika hali ya usingizi mzito au kuanza kuongea katika lugha ngeni. Kule Uturuki msomi aliye wa makundi kama hayo akaeleza: “Tunaongozwa kuita roho, ndipo kuwatuma waende tena baada ya kutuhudumia.” Msichana mmoja alikiri kwamba, shetani huwa anamtembelea kila Ijumaa. Marafiki yake walijaribu kumwambia kwamba anaona ndoto, lakini alieleza kwamba, alipokuwa mgonjwa sana wakati wa utoto baba yake alimpeleka kwa Sufi shehe, naye akamponya kwa msaada wa nguvu za kiroho. Tangu hapo alikuwa anasumbuliwa kila juma kwa kutembelewa na huyu mwovu.

Kule Pakistani kundi fulani liliendesha kijamii hali ya kutafakari sana (taamuli). Mmojawao alipopata kuwa Mkristo, baba wa yule aliyeokolewa akamleta kiongozi wa Muskiti, ili amrudishe kwenye Uislamu mwana wake aliyepotea. Lakini huyu shehe alipo­dhamiria kwa ya kufanya sex kwa huyu aliyegeuka, baba yake alimtupa nje ya nyumba yake yule mwalimu wa Qur‘ani kwa sababu upotovu ya aina hiyo hayakuwezekana kabisa ndani ya familia yake.
Kule Indonesia dini ya kihindi pamoja na roho zao zilizo nyingi, pia imechanganywa na Uislamu ule wa kutafakari sana kwa kadiri kwamba, kwenye sikukuu za vijijini kabila fulani wanaagiza zile roho zionekane na kupigana wao kwa wao hewani. Kumeza chuma au kioo cha taa ya umeme ambazo zinayeyuka wakati wa kumeza, ndiyo mambo yanayotendeka mara nyingi. Sauti za kiume zinasikika zikitokea kwa wanawake, na kinyume pia.

Ma-Sufi hujaribu kumfanya Allah aishi ndani ya nafsi zao na kuwajaza na kule kuwepo kwake. Wengine hujaribu kinyume cha hayo, wamwingilie Allah mwenyewe kwa njia ya kutafakari mno. Kundi lingine tena lina shabaha kupenya ndani ya ulimwengu wa malaika na pepo wabaya “nyuma” ya Allah. Wamefungwa ndani ya madaraja ya kuongezeka ya kupagawa kwa Kwa mazingira ya mazingaombwe.

Kwa vile katika Uislamu Allah yu mbali kabisa na uumbaji wake, basi yeyote asishangae kwamba, Waislamu wenye heshima hujaribu kujenga daraja kwa umbali ule wakifanya mazoezi mengi ya kidini. Bahati mbaya roho zisizo za kikristo zinajimwaga ndani ya utupu huo mkuu. Hesabu ya ma-Sufi katika Uislamu inaendelea kuongezeka. Katika nchi fulani wamefikia 10% hadi 20% ya jumla ya Waislamu, huku wamegawanyika katika makundi kadhaa mengi Wanatheologia wengine wa kiroma wanadai kwamba, hao ma-Sufi wangeweza kuwa daraja bora kati ya Ukristo na Uislamu. Hata hivyo, hawaangalii jambo zito kwamba, wale wanaotafakari sana kidini bado wanategemea haki yao wenyewe na wanafikiri kwamba, hawahitaji kutubu. Kwao Mwana wa Mungu aliyesulibiwa anaendelea kuwa kikwazo. Upole wao unawatenga na ukombozi wake Yesu, uliokamilishwa kwao sawasawa na kwa ajili yetu.

2.14.8 -- Wakombozi katika ya Uislamu

Ma-Sufi waweza kuelezwa kama hua kati ya Waislamu walio­changanyikiwa. Waislamu magaidi wangeweza kuitwa wachuuzi kati yao. Wanalalamika: “Kusali kote, kufunga na kutoa sadaka haifai lolote. Twahitaji kutenda mambo sisi wenyewe. Twatakiwa kutoa sadaka maisha na damu yetu ili kuosha Uislamu na aibu yake na kushinda udhalimu ndani ya jamii ya kiislamu kwa njia ya kigaidi!”

Hassan al-Banna, mwanzilishi wa Undugu wa Kiislamu, yeye alifundisha kwamba, kusali na kufunga haitoshi kwa kuishi Uislamu kwa ukamilifu. Alisisitiza kwamba, Mwislamu wa kweli angeshinda sheria zake hadi awe tayari kuua maadui wa Uisla­mu. Maagizo 100 ndani ya Qur‘an yanawaita Waislamu kushiriki katika mashambulio yenye silaha, hii iwe uthibitisho wa utii wao kiimani.

Undugu wa Kiislamu, ambayo kwa vikali unafukuzwa na serikali ya Misri, sasa umegawanyika katika vikundi zaidi ya 50 vya ukatili vya kutisha. Ayatollah Khomeini upande wa Wa-Shia alikamata mwenge wa Vita Vitakatifu akatuma wapiganaji wake wa kujitoa muhanga kwenye nchi kadhaa kuwa wauaji wa siri, kama vile wauaji wa siri wa zamani za vita vya kukomboa nchi takatifu, ambao walifanya ulimwengu wote kukaa macho.

Hizbollah, Hamas, al-Djihad na makundi mengine wanawafundi­sha wafuasi wao Kujitoa muhanga na ikipasa kufa wenyewe. Qur‘an inafunua kwamba, Allah mwenyewe angeandika imani ya kiislamu ndani ya mioyo yao na kwamba, Allah angewatia nguvu kwa miinuko kama hayo na kuwapa roho ya kwake (Sura al-Mujadila 58:22) Hii ndiyo aya ya pekee ndani ya Qur‘an inayotaja uhusiano kati ya Mwislamu na roho ya Allah! Wafia dini katika Vita Takatifu wanaahidiwa mahali pazuri mno katika paradiso (Sura al-Baqara 2:154; Al ‘Imran 3:157-158, 161-171, 193-195; al-Nisa 4:74; Muhammad 47:4-6 nk.). Itakuwa si ya haki, kama tungewaita hao wapiganaji wanaojitoa muhanga kwamba ni magaidi, kwa sababu wenyewe wanajiona kuwa wakombozi wanaotoa sadaka maisha yao kwa ajili ya ushindi wa Uislamu. Wanafundishwa kwamba, si wao wanaoua maadui wa Uislamu, bali ni Allah mwenyewe. Allah atapiga wanapopiga bunduki kwa kufuta wote walio kinyume cha Uislamu. (Sura al-Anfal 8:17)

Waandishi wa habari kadhaa na wasomi wa utu wema huwaeleza hawa wajitoa muhanga kuwa ni kundi ndogo la washenzi wa mwisho ndani ya Uislamu. Ila wamekosea sana! Maana hao wakombozi ndiyo wa pekee wanaotimiza kikamilifu Qur‘an na kutekeleza maagizo ya Allah kwa gharama yoyote ile (Sura al-Baqara 2:191-193; al-Anfal 8:39; al-Tawba 9:11 nk.). Wenye kujali utu wema na Waislamu wapole wanaitwa waoga na wasaliti kwa Qur‘an. Kufanya amani na wasio Waislamu inasikitisha, isipokuwa kwa muda kama wamepungukiwa hela na silaha au hali halisi ya maisha inawa­shinda.

Mambo gani yametendeka kwa miaka hii 50 iliyopita kule Israeli na maeneo yanayozunguka nchi hiyo kwa vita visivyo vitakatifu vya Waislamu? Hayo yaweza kujaza ma-vitabu. Kuteka ndege au kuziangusha, mabomu mahotelini, kuharibu magari ya mizinga kwa njia ya kujitoa muhanga, na vitisho vya kudumu vinatatiza mishipa ya ufahamu na hayo ndiyo namna za tetemo hizo.

Watalii wa Uswissi walipouawa, kukatwa viungo na wake zao kubakwa karibu na makaburi ya wafalme pale Luxor Misri, wale wakombozi wakilia:“Allahu akbar!” (Allah ni mkubwa!). Sauti kama hii ilisikika kule Indonesia wakati makundi fulani walipo­choma makanisa mamia na kutwaa wasichana wa kichina. Kwenye kisiwa cha Mindanao kule Ufilipino zaidi ya Wakristo 50,000 waliuawa na katika vita vya uhuru na wakombozi wa kiislamu baada ya Vita Kuu ya Pili. Namba kama hiyo au hata zaidi walikufa kule Nigeria ya kaskazini, kwa sababu Wakristo hawakukubali kutii amri za kiislamu, yaani Shari‘a.

Hapo Ujerumani Waislamu wahafidhuna 32,000 walipewa kimbilio, kwa sababu wengi wao wanatakiwa na serikali zao huru za kiislamu. Wakati wowote wako chini ya uchunguzi wa watu maarufu wa kijerumani. Tendo la kuchinja watu ovyo, jinsi ilivyotokea kwenye michezo ya Olympics 1972 kule Munich (Ujerumani), inawezekana tena kutokea wakati wowote. Katika Qur‘an Allah anawachochea waumini halali wote kupigana na kuua maadui wa Uislamu(Sura al-Baqara 2:191-193; al-Nisa 4:89 na 91; al-Anfal 8:39; al-Tawba 9:5 nk.) Wayahudi na Wakristo wanapaswa kupigwa kufuatana na Sura ya Ungamo (Sura al-Tawba 9:28-29) kwa sababu hawaamini ndani ya Mungu wa kweli, hawafuati Shari‘a nao wanashiriki dini ya ukosefu! Uislamu, kwa kufuatana na Qur‘an, ni roho ya uharibifu.

2.15 -- Mwisho, kwa kufupisha habari ndefu kuwa fupi

Yeyote atakaye kutoa injili ya Kristo kwa Waislamu, basi ashinde wazo kwamba, Waislamu wote wanaamini na kuwaza sawa! Yeyote atakaye kuwahudumia lazima asikilize kwanza na kuuliza wanakotoka na wanalofikiri juu ya siasa, dini na jinsi wana­vyoona maisha yao ya mbeleni.

Yeyote anayepungukiwa hekima katika maongezi kama hayo, basi amwulize Yesu amjalie uongozi, ili awaone Waislamu wale, ambao mioyo yao imeandaliwa na Roho wa Mungu. Upendo, uaminifu unadumu kuwa lugha bora unaoeleweka na binadamu wote. Yeye awasaidiaye raia wa kigeni kutengeneza shida zao na maofisi, basi pamoja na hayo anayo nafasi kuwaongoza wapate kuwaheshimu na kuwaelewa Wakristo.

Hatuna sababu kuhofia roho ya Uislamu, kwa sababu baraka za Yesu Kristo ina nguvu zaidi kuliko laana za Mhammad. “Yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia” (1. Yohana 4:4). Pia tusitumbukie haraka bila matayarisho katika mazungumzo na Waislamu, bali tujitayarishe vizuri. Kuna mashi­rika kadhaa walio tayari kuwapa misaada wale wanaokusudia kutumika katika huduma hii kwa vitabu na kozi za kuwaimarisha vizuri kwa kazi hii.

Pia unaweza kupata majibu ya kusaidia kwa makundi tofauti tofauti ya Waislamu ndani ya Agano la Kale, katika Agano Jipya, katika maandishi ya kawaida, hata ndani ya Qur‘an na pia kutokana na uzoefu wa maisha yako. Bwana ndiye awezaye kufungua mlango wa moyo wa Mwislamu fulani na kukujalia neno kwa nafsi hiyo kwa wakati wa kufaa kwa njia ya Roho wake Mtakatifu.

2.16 -- MASWALI

Mpendwa Msomaji!

Kama umejifunza kitabu hiki kwa bidii, bila shaka utaweza kwa urahisi kujibu maswali yafuatayo hapi chini. Kila mmoja atakayejibu 90% ya maswali yote ndani ya hivi vitabu 8 vya mfululizo huu kwa ufasaha, atapokea cheti kutoka kwenye kituo chetu

Mafunzo endelevu
katika njia ya kusaidia kuendesha mazungumzo na Waislamu kuhusu Yesu Kristo

Hii itakutia moyo kwa ajili ya kuendelea katika kumtumikia Kristo.

  1. Zipi zilikuwa dini tatu maalumu zilizotangulia na kuvuta kuan­za kwa Uislamu?
  2. Uhusiano kati ya Wayahudi na Wakristo ulikuwa wa namna gani Arabuni na hasa Yemeni?
  3. Je, tamko la Qur‘an “Watu wa Kitabu” ilikuwa na maana gani kwake Mhammad?
  4. Ni nani ambaye Mhammad alimfikiria kuwa Mwislamu wa kwanza?
  5. Kwa nini Mhammad alimpendelea Musa, wala si huyu mpole Kristo, mwana wa Mariamu kuwa kama mfano kwa ajili yake?
  6. Kwa nini Mhammad alieleza Wayahudi kuwa ni maadui wakubwa wa mwisho wa Waislamu? Na jinsi gani aliwa­shinda?
  7. Lipi katika makanisa matatu makuu ya mataifa lilikuwa na mvuto mkubwa zaidi nyakati za kutokea na kuenea kwa Uislamu?
  8. Kanisa la Magharibi (Orthodox) liliunda picha gani ndani ya mioyo ya Waislamu na kwa nini liliweza kuitwa “Kanisa lililoteseka kwa miaka 1370”?
  9. Kwa nini Waislamu wengi wanaliangalia Kanisa la Waroma kuwa ni kanisa la vita? Jinsi gani unaweza kueleza hayo, unapokumbuka matokeo katika historia?
  10. Kwa nini makanisa ya kiprotestanti hayakuwa na mvuto wowote katika kujengeka kwa Uislamu? Kwa nini Waislamu wanawaangalia Wakristo wa kiinjili kwa mashaka sana?
  11. Makanisa ya kikristo mangapi yaliyojitawala yapo duniani siku hizi na ipi ni kigawanyo ya kawaida kwa ajili ya yote hayo?
  12. Kwa Wakristo wote kimsingi ni jambo gani linalowatofautisha na Uislamu?
  13. Wakina nani ni Wasunni, na jumla yao ni asilimia ngapi ya Waislamu wote wanaofuata mkondo huo wa kwanza wa Uislamu?
  14. Waislamu Washia ni wakina nani, na wangapi wanaofuata kanuni zao?
  15. Ni lini wimbi la tatu la upanuzi wa Uislamu ulipoanza? Jambo gani ni nguvu yao kuisukuma, na jambo gani ni malengo yao?
  16. Kwa nini kila Mwislamu ni tofauti na mwingine yeyote? Jinsi gani tunaweza kufahamu baadhi ya hali wanavyojisikia, mawazo yao, imani yao na matendo?
  17. Zipi ni mambo ya kipekee kwa Waislamu wahafidhuna, na asilimia ngapi ya Waislamu wote wanafuata miongozo yao?
  18. Jinsi gani tunawaweza kuwakabili hao Waislamu wahafi­dhuna?
  19. Waislamu wangapi ni wa kisasa na walio huru,na aina gani ya maisha wanafuata?
  20. Kwa nini kuna mivutano mibaya na hata vita za ndani kwa ndani kati ya makundi ya wahafidhuna na ya kisasa ya serikali za kiislamu ?
  21. Watumishi wa Bwana wangeamua kufanya nini wanapo­tambua kwamba, nusu ya Waislamu wote ni wanawake? Nani ataweza kuwafikia hao?
  22. Shida kubwa ni zipi wanazokabili wanawake ndani ya Uislamu?
  23. Watumishi wa Bwana wangeona changamoto gani wanapo­tambua kwamba, nusu ya Waislamu wote wako chini ya miaka 18, na katika nchi zingine za kiislamu hata chini ya miaka 16 kwa umri?
  24. Jinsi gani tutaweza kufikia vijana na watu wazima wenye umri mdogo katika ulimwengu wa kiislamu ?
  25. Kuna umuhimu gani ndani ya jambo kwamba, 5% ya Waisla­mu wamekata tamaa na Uislamu wao? Yapi ndiyo sababu kuu zakushindwa kwao? Jinsi gani tutaweza kuwatambua wako wapi?
  26. Kwa nini mtu mmoja mmoja anaweza kuamini kwamba hakuna Mungu, na bado kujihesabu kuwa Mwislamu? Je, Uislamu ni zaidi ya dini tu?
  27. Yapi ni sababu kwamba, 10 hadi 20% ya Waislamu wote wamepata kuwa Wameamini katika namna ya ushirikina? Jinsi gani wanatofautiana na Waislamu wengine? Na wana­jaribu kusimamisha nini?
  28. Yapi ni hali bora na fadhili mambo ya maajabu ndani ya Uislamu? Jambo gani linawazuia wasimkubali Kristo kuwa mwokozi wao?
  29. Kwa nini Waislamu magaidi wanajiita “Wakombozi”? Jinsi gani wanaweza kujidai kwamba, wao pekee ndiyo Waislamu waaminifu wa kweli?
  30. Hao “Wakombozi” wanatazamia nini wakifa katika shambulio za kujitoa muhanga?
  31. Lengo kuu ya kijitabu hiki ni nini?
  32. Kwa nini tusihofu kuwafikia Waislamu na Habari Njema?
  33. Zipi ndiyo chimbuko 5 ambamo tunawaweza kugundua majibu ya kusaidia kwa ajili ya kusudi letu la kufanya mazungumzo na Waislamu?

Kila mshiriki katika maswali haya hii anaruhusiwa kutumia kitabu chochote apatacho, pia na kumwuliza mtu yeyote mwaminifu anayemfahamu, anapojibu maswali hayo. Sisi tunangojea majibu yako yakiwa yameandikwa pamoja na jina na anwani yako kwenye karatasi au katika e- mail kutoka kwako. Tunakuombea kwa Yesu, aliye Bwana aliye Hai, aweze kukuita na kukutuma, akuongoze, akutie nguvu, akulinde na kuwa karibu nawe kila siku ya maisha yako mbeleni!

Wako katika utumishi wa Bwana,

Abd al-Masih and his brothers in the Lord

Tuma majibu yako kwa anwani hii:

GRACE AND TRUTH
P.O.Box 1806
70708 Fellbach
GERMANY
or by e-mail to:

info@grace-and-truth.net

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on November 25, 2026, at 03:43 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)